Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  4 Sha'aban 1443 Na: 1443 H / 14
M.  Alhamisi, 17 Machi 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Enyi Watu, Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh, Inawaalika Kuhudhuria Kongamano Lijalo la Mtandaoni kwa Anwani: “Je, Kweli Tuko Huru?”
(Imetafsiriwa)

Kama mnavyojua, katika bara hili, baada ya miaka mia mbili ya mapambano dhidi ya unyonyaji na ukandamizaji wa ukoloni wa Uingereza, Pakistan na India ziliibuka kama Dola huru mnamo tarehe 14 na 15 Agosti 1947 mtawalia. Baadaye mwaka wa 1971 Bangladesh iliibuka kama Dola huru. Lakini mfumo wa Kisekula wa Kirasilimali wa Kimagharibi bado ungali unaendelea kupitia watawala vibaraka, wanasiasa wafisadi, na wasomi wanafiki.

Hakika, tumeingia kwenye ukoloni mamboleo, matokeo yake, ukombozi wa kweli ambao watu wamekuwa wakiupigania kwa zaidi ya miaka 250 bado haujapatikana. Uingiliaji kati wa wakoloni haswa Amerika-Uingereza katika nyanja zote za maisha yetu yakiwemo masuala ya kisiasa na kiuchumi unaongezeka kila uchao. Watu sasa wanalazimika kuvumilia masaibu makubwa kwa sababu ya ukandamizaji wa kiuchumi na kisiasa wa watawala wa kisekula. Kutokana na hali hizi, Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh inajibu swali "Je, kweli tuko huru" kutoka kwa mtazamo wa kisiasa na kiuchumi katika kongamano lijalo la mtandaoni litakalotangazwa na Al Waqiyah TV mnamo tarehe 18 Machi. Tunatoa wito kwa kila mwananchi mwenye ufahamu, haswa wasomi na wanasiasa wenye ikhlasi wa nchi hii kujumuika na kongamano hilo, kujihusisha na majadiliano, na kupeleka ujumbe mbele zaidi kwa nia ya kupata ukombozi wa kweli na kujiacha huru kutokana na minyororo ya ukoloni mamboleo. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

 (إِنَّ اللَّهَ لاَ يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّى يُغَيِّرُوا مَا بِأَنفُسِهِمْ) “Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo naf- sini mwao.” [Surah Ar-Ra'd: 11].

Mitandao ya Matangazo ya Kongamano:

ALWAQIYAH.TV

Facebook.com/alwaqiyahtv.en

YouTube.com/ALWaqiyahTV

Tarehe na Wakati: Ijumaa, 18 Machi, 2022 3:30 pm BST

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.