Watu Wapendao Uislamu wa Nchi Wameukataa Mkataba wa Julai, ambao umejengwa juu ya Msingi wa Usekula na Demokrasia Batili ya Magharibi, Na Wanataka Mkataba wa Madina uliojengwa juu ya Msingi wa Imani yao Safi ya Kiislamu
- Imepeperushwa katika Bangladesh
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mnamo 17 Oktoba 2025, kipote cha wanasiasa wenye uchu wa madaraka nchini humu walitia saini ‘Mkataba wa Julai - suluhisho la kisiasa lililoandikwa kwa kuzingatia imani potofu za kidemokrasia ya kisekula na mfumo wa Wakoloni makafiri wa Magharibi hasa Marekani-Uingereza, na kuweka mfano mwengine wa kuchukiza wa usaliti kwa Uislamu na Waislamu, na utiifu kwa nchi za Magharibi. Mfumo huu wa kisekula wa kibepari uliotungwa na wanadamu umefeli katika nchi zote duniani. Jambo hili ni la kweli mithili ya mwangaza wa mchana kwamba, mfumo huu wa ukandamizaji unalinda maslahi ya tabaka tawala, mabepari wachache na wakoloni wa Magharibi, na kuwanyonya watu wengi zaidi. Mnashuhudia kwamba kizazi cha vijana (Gen-Z) katika nchi nyingi wanaasi tabaka tawala la kibepari moja baada ya jengine na kuwaangusha watawala.
 
			



 
  
  
  
  
  
  
  
  
 