Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
| H. 12 Jumada II 1447 | Na: H 1447 / 17 |
| M. Jumatano, 03 Disemba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mauaji ya Pilkhana Yalikuwa Njama ya India ya Kudhoofisha Jeshi la Nchi hii - Ripoti Hii ya Tume Huru ya Uchunguzi ya Kitaifa Imethibitisha Ukweli ambao Hizb ut Tahrir Iliuwasilisha kwa Taifa kwa Ujasiri Miaka Kumi na Sita Iliyopita.
Tunatoa Wito Tena kwa Watu Kuwa Macho dhidi ya Mpango wa Marekani wa Kudhibiti Jeshi Letu
(Imetafsiriwa)
Tume Huru ya Kitaifa ya Uchunguzi iliyoundwa na serikali ya mpito kuhusu mauaji ya Pilkhana, na kusababisha vifo vya maafisa 57 wenye sifa nzuri, yaliyotokea katika Makao Makuu ya BDR mnamo Februari 25 na 26, 2009, imetoa ripoti yake ya uchunguzi. Uchunguzi umethibitisha kuhusika kwa Hasina na washirika wake Tapas na wengineo katika kutekeleza njama ya India ya kudhoofisha jeshi la nchi hii. Tunataka sana adhabu ya haraka kwa wahalifu hawa waliohusika katika tukio hilo na kutangazwa kwa India kama dola adui. Lazima mukumbuke kwamba chama cha kisiasa chenye busara na ikhlasi, Hizb ut Tahrir, kilikuwa cha kwanza kuleta ukweli huu kwa ujasiri kwa taifa (mnamo 28 Februari 2009, toleo lililotolewa na Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh lilikuwa na kichwa: “Kulaani dhidi ya njama ya India ya kuharibu jeshi letu na BDR, na kutochukua hatua kwa serikali”). Matokeo yake, njama hii ya Hasina msaliti ilikatizwa mapema, na msingi wa kuanguka kwa Hasina uliwekwa mara moja. Mara tu baada ya mkasa huu wa kuhuzunisha wa Pilkhana, hatukuwatambua tu wapangaji wakuu na malengo yao, lakini pia tulisimama kama ngao kwa maafisa hao waaminifu wa jeshi, ambao serikali ya kidhalimu ya Hasina iliwaita wanamgambo baadaye. Matokeo yake, serikali iliyoanguka ya Hasina iliweka marufuku isiyo ya haki kwa chama cha siasa kisicho na vurugu cha Hizb ut Tahrir na kuendelea kuwakandamiza na kuwatesa viongozi na wanaharakati wake. Lakini sisi, tukipuuza udhalimu na ukandamizaji wa Hasina aliyeanguka sasa, tuliwataka watu kusimama dhidi ya kukamatwa, kutoweka, mauaji na kufutwa kazi kwa maafisa wenye ikhlasi wa kijeshi na serikali ya Hasina, na watu waliitikia wito huu kwa shauku (mnamo 7 Januari 2012, kichwa cha toleo tulilotoa kilikuwa: “Enyi Waislamu! Laanini dhidi ya utekaji nyara unaoendelea, kukamatwa na kufutwa kazi kwa maafisa wenye ikhlasi wa jeshi la nchi hii na msaliti Hasina kwa amri ya Marekani-India”).
Wakati huo, Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) na la Uingereza Scotland Yard yalihusika katika uchunguzi ili kuwasaidia wachunguzi wa ndani katika kuchunguza mauaji hayo, na kwa mashirika haya yenye viwango na utaalamu wa kimataifa, kufichua siri ya mauaji haya hakika haikuwa jambo gumu. Hata hivyo, walificha tukio hili kwa sababu Hasina alikuwa kibaraka wa Uingereza na India ndiyo mlinzi wa kikanda anayelinda maslahi ya Marekani na Uingereza katika eneo hili. Zaidi ya hayo, Marekani ilikubali mageuzi haya kwa sababu kuondolewa kwa maafisa wenye vipaji na waaminifu kutoka jeshini kulikuwa muhimu ili kutekeleza mlinganyo mpya wa mahusiano ya Marekani na India (kuitazama Bangladesh kupitia macho ya India). Tungependa kuwakumbusha watu kwamba sura ya Wamarekani imebadilika katika dhurufu zilizobadilika, lakini hakukuwa na mabadiliko katika mahusiano ya Marekani na India. Tunaonya tena kwamba Marekani inataka kutumia tukio hili kuhujumu ari ya jeshi letu na inatamani sana kuanzisha udhibiti wa jeshi letu. Kwa kusudi hili, imehusisha genge lake la vibaraka katika propaganda dhidi ya jeshi. Kwa nini serikali ya mpito ya sasa, iliyozaliwa kutokana na Mapinduzi ya Julai, na ambayo iliingia madarakani kwa kutegemea matarajio ya watu ya mabadiliko ya kweli, haijaondoa marufuku isiyo ya haki iliyowekwa kwa Hizb ut Tahrir na Hasina aliyeanguka? Kwa hivyo, je, imebadilisha tu barakoa na mwonekano wake, lakini njama hiyo inaendelea? Kwa kweli, machozi ya mamba na upinzani dhidi ya India na vyama vya kisiasa vilivyotii Amerika kuhusu mauaji ya Pilkhana si kitu chengine ila ni udanganyifu wa kupata manufaa ya kisiasa. Kwa sababu wanafahamu vyema uhusiano wa Marekani na India na wanalazimika kufuata mipaka iliyowekwa na bwana wao mkoloni kafiri.
Enyi Watu! Hizb ut Tahrir, chama cha kisiasa ambacho hakiwadanganyi watu wake, kinafanya mvutano wa kifikra na kisiasa ili kuukomboa Ummah wa Kiislamu kutoka kwa makucha ya dola za kikafiri za kikoloni. Na tunasema tena kwa lugha iliyo wazi - ni kupitia kusimamishwa kwa Khilafah kwa njia ya Utume iliyoahidiwa na Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake (saw) pekee ndipo nchi hii itakapokombolewa kutoka kwa Kafiri Mkoloni Marekani-Uingereza na wapambe wao wa kieneo - Umbile la Kiyahudi na Hindutva India, Insha'Allah. Kwa hivyo, harakati hii itaendelea hadi lengo linalotarajiwa la uasi mkubwa yaani ukombozi wa kweli wa watu litakapopatikana, na tunawataka watu kubaki wameungana chini ya uongozi wa Hizb ut Tahrir. Mwenyezi Mungu (swt) amesema:
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَكُونُوا مَعَ الصَّادِقِينَ]
“Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na kuweni pamoja na wakweli.” [Surah At-Tawbah: 119].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Bangladesh
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Bangladesh |
Address & Website Tel: +88 01798 367 640 www.ht-bangladesh.info |
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd |