Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  1 Muharram 1443 Na: 023 / 1443 H
M.  Jumatano, 02 Februari 2022

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

 Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir Chazindua Kampeni ya Kimataifa: “Khilafah: Yenye Kuhakikisha Hadhi, Usalama na Haki za Kisheria za Wanawake”

(Imetafsiriwa)

Mwezi wa Rajab unaashiria kumbukumbu ya kutisha ya kupotea kwa Khilafah zaidi ya miaka 100 iliyopita katika kalenda ya Hijri. Dola hii inayoongoza inayotawala kwa Uislamu siku zote ilisimama kama mlinzi wa hadhi, usalama na haki za kisheria za wanawake katika ardhi za Kiislamu na kwengineko. Kufuatia kuanguka kwa Khilafah, maisha ya wanawake katika eneo hili na wanawake wa Kiislamu kote duniani yaligubikwa na aina zote za ukandamizaji na dhulma, mateso na ufukara chini ya mifumo na tawala zilizobuniwa na mwanadamu – kuanzia tawala za kidemokrasia hadi za kidikteta - ambazo zilivunja heshima yao, kushindwa kuwapa usalama wa kimwili na wa kifedha, na hazikujali chochote kuhusu haki zao za kisheria walizopewa na Mungu. Ukataji tamaa na kutapatapa vikawa ndio hadithi ya maisha yao kwa kukosekana kivuli na ulinzi unaotolewa na Sheria na Mfumo wa Mwenyezi Mungu (swt).

Kuna njia ya kutoka katika jinamizi hili hai ambalo mamilioni ya wanawake wa Kiislamu wanakabiliana nalo kote duniani, na hiyo ni kusimamisha tena Khilafah kwa njia ya Utume ambayo Mtume (saw) aliitaja kuwa ni walinzi na ngao ya Waislamu. Hata hivyo, kuna hofu nyingi, mashaka na maswali leo kuhusu dola kama hiyo inamaanisha nini kwa wanawake na hadhi na haki zao. Hofu na mashaka hayo yanatokana na uwongo wa karne nyingi, upotoshaji na mashambulizi ya serikali za kikoloni za Magharibi, waandishi, vyombo vya habari na watetezi wa haki za wanawake kuhusiana na jinsi wanawake wanavoamiliwa chini ya utawala wa Kiislamu unaoendelea kuenezwa hadi leo. Hadithi na uwongo huo ziliundwa kwa makusudi na kuenezwa na watawala wa kikoloni mtawalia na wafuasi wao ili kuiangamiza Khilafah na baadaye kuzuia kurudi kwake, kwa lengo la kudumisha na kuendeleza ushawishi wao wa kikoloni na udhibiti wa siasa na rasilimali za ardhi za Kiislamu.

Kwa hivyo Rajab hii, Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir, kimezindua kampeni ya kimataifa ya kushughulikia hofu, mashaka, na maswali haya kuhusu hadhi ya wanawake chini ya utawala wa Kiislamu. Kampeni hii yenye kichwa, “Khilafah: Yenye Kuhakikisha Hadhi, Usalama na Haki za Kisheria za Mwanamke,” inalenga kuwasilisha ufahamu wa wazi na dira ya jinsi maisha ya halisi yatakavyokuwa kwa wanawake chini ya kivuli cha dola ya Khilafah kuhusiana na haki zao, dori na muamala kama inavyothibitishwa na nususi za Kiislamu, na kudhihirishwa na utawala wa Kiislamu huko nyuma, mbali na uwongo na upotoshaji wa wasomi wa mashariki na wa kikoloni. Muhimu zaidi, tutajaribu kueleza jinsi kanuni, sheria, taasisi, miundo na nidhamu za Khilafah zitaweza kutatua kivitendo matatizo mengi ya kisiasa, kiuchumi, kimahakama, kielimu, kiafya na kijamii ambayo wanawake wanakabiliana nayo leo na kwamba mifumo yote iliyotungwa na mwanadamu, ikiwemo demokrasia - Mashariki na Magharibi - imeshindwa kutatua.

Tunatumai kwamba mtafuatilia na kuunga mkono kampeni hii muhimu inayolenga kufuta uwongo, kuvunja khofu, na kuwasilisha ukweli wa nafasi ya wanawake chini ya Khilafah ili tuweze kugeuza kukata tamaa kuwa matumaini na kusimamisha dola ambayo itamaliza jinamizi lililo hai linalowatesa mamilioni ya wanawake leo na kujenga mustakabali angavu, wenye uadilifu zaidi, salama na wenye hadhi kwa wanawake wa Umma huu wa Kiislamu.

﴿وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُم فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَلِكَ فَأُوْلَئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [An-Nur: 55]

#ReturnTheKhilafah  #YenidenHilafet
 #الخلافة_101 #أقيموا_الخلافة  

Dkt. Nazreen Nawaz

Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.