Kuvunjwa Moyo Kupya: Watu wa Gaza Wanakufa kwa Baridi Baada ya Kuachwa Kuteswa na Mauaji ya Halaiki kwa Miaka Miwili!
- Imepeperushwa katika Kitengo cha Wanawake Afisi Kuu ya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Maafa yanayoikumba Palestina inayokaliwa kwa mabavu yanaendelea bila kukoma. Tangu kuanguka kwa Khilafah, ambayo mtawala wake aliwahi kutamka, “Palestina ni ardhi iliyonyweshwa kwa damu ya mababu zangu, na iwapo Khilafah itaanguka, mtaichukua bila malipo,” uvamizi wa Waingereza (ulioitwa Mamlaka) uliibadilisha. Na hadi leo, umbile la Kiyahudi linaloikalia kwa mabavu, lililoundwa na Uingereza na kuungwa mkono na nchi za Magharibi kwa mali yake yote, vifaa, ujuzi na uwezo wake wote, linaendelea kuwaua watu wa ardhi iliyobarikiwa, likiwafanyia ukatili vijana na wazee, na kuwatishia wafungwa kuwaua na kuwanyonga, huku ulimwengu ukitazama. Limeizingira Gaza kwa miaka mingi, likiishambulia bila kuchoka kwa ukatili usiofikirika, na kusababisha mauaji ya zaidi ya watu elfu sabiini. Na ulimwengu wa Kiislamu, pamoja na majeshi yake na wanazuoni, hutazama na kuona kama vipofu wanavyofanya, na husikia vilio vya wanawake waliofiwa kama viziwi wanavyosikia!



