Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  28 Jumada II 1443 Na: 1443 H / 022
M.  Jumatatu, 31 Januari 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Warohingya Wakimbia Moto hadi Motoni; Ni Dola ya Khilafah pekee Ndio Itakayowaokoa na Kuwaregeshea Haki zao
(Imetafsiriwa)

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) liliripoti moto mkali katika kituo cha matibabu cha COVID-19 katika kambi ya Cox's Bazar nchini Bangladesh, ambayo huhifadhi wakimbizi wanaokimbia kutoka Myanmar, mnamo Jumapili alasiri, 9/1/2022. Shirika hilo la Umoja wa Mataifa lilisema, katika ukurasa wake wa Twitter, kwamba hakuna aliyejeruhiwa kutokana na moto huo uliozuka, lakini lilibainisha kuwa moto huo uliathiri maelfu ya wakimbizi wa Rohingya, na kusababisha uharibifu mkubwa kwa sehemu za kambi hiyo kubwa zaidi ya wakimbizi katika duniani, ambayo inajumuisha karibu wakimbizi 900,000.

Kambi ya Cox's Bazar imeundwa kwa vijumba vya  mianzi na turubai, na kuifanya iwe rahisi kushika moto, na kuongeza mateso na hofu ya wakimbizi.

Ikumbukwe kwamba hii si mara ya kwanza kwa kambi hii kukabiliwa na hatari hii na nyinginezo. Mnamo Machi 2021, nyumba 10,000 zilichomwa moto na angalau watu 45,000 walilazimika kuyahama makaazi yao. Mafuriko makubwa ya monsoon mnamo Julai 2021 yaliathiri wakimbizi 46,000 na kusababisha maporomoko makubwa ya ardhi.

Ndugu na dada zetu walikimbia kutokana na uonevu wa wahalifu wa Myanmar. Walikabiliwa na vita vya kikabila kwa kuchomwa moto vijiji, kuuawa na kunyanyaswa; jambo ambalo mamlaka ya Myanmar inakanusha, ikidai kuwa wanapambana na Waislamu wenye misimamo mikali. Kwa hakika, inatafuta, pamoja na chuki na uadui wake kwa Uislamu na Waislamu, kuwaangamiza watu hawa na kuwaritadisha waliosalia kutoka kwenye Dini yao.

Ndugu na dada zetu walikimbia kifo, wakitumaini kuokoka na kuishi kwa usalama, lakini serikali ya Bangladesh haikuwapa hilo, kwa hiyo wakawa kama wale waliotafuta kimbilio dhidi ya joto kali ndani ya moto! Wanaishi katika nyumba zinazotishiwa na moto unaoteketeza nguo zao na mianzi, na hauwalindi kutokana na baridi na mafuriko ya msimu wa baridi. Ni nyumba, kama ambaye si nyumba! Ni kuwahadaa tu watu, kwani serikali hii haifurahii uwepo wao katika ardhi yake, na mara nyingi imeeleza kuwa ina nia ya kuwafukuza na kuwaregesha Myanmar, licha ya hatari ya maisha yao, haswa baada ya kampeni kikatili ya kijeshi iliyoanza dhidi yao mnamo Agosti 2017, ambayo iliwafanya watishiwe na kutokuwa salama.

Hali ya wakimbizi Waislamu nchini Bangladesh na kwingineko inadhihirisha njama za serikali zilizopo katika nchi za Kiislamu pamoja na maadui wa Waislamu. Wakimbizi hawa walizikimbia nchi zao kwa kuogopa kifo, wakituhumiwa kwa misimamo mikali na ugaidi, kuishi maisha ya unyonge na ukandamizaji katika nchi walizokimbilia. Walipoteza usalama, utulivu, na makao. Walikimbia kuokoa maisha yao, wakitumaini kwamba watapata hifadhi katika serikali hizi, lakini matumaini yao yalikatika na moto walioukimbia ukawafuata, na hofu, kupuuzwa na kifo kikawafuata.

Enyi Umma wa Kiislamu: Hawa ni kaka na dada zetu, ambao walidhulumiwa na wahalifu. Wakawahamisha, wakawatiisha, na wakawadhoofisha, hivyo wakakimbia pamoja na Dini yao wala hawakuibadilisha. Walitafuta usalama katika serikali hizi, lakini walikatishwa tamaa. Je, kimbilio hutafutwa kutoka kwa watu kama hao?! Ni vibaraka wanaofuata upotofu wa wahalifu na mbinu zao na wanashirikiana nao kuwagandamiza Waislamu na kuipiga vita Dini yao.

Enyi Umma wa Kiislamu: Hawa ni ndugu zetu wanaoteseka, basi unyonge huu utaendelea hadi lini? Mpaka lini maadui wa Mwenyezi Mungu watawakandamiza watoto wenu na hali nyinyi mmenyamaza kimya? Basi inukeni na mkukute vumbi la udhalilishwaji kutoka kwenu, naapa kwa Mwenyezi Mungu, hili halikubaliki kwenu, kwa sababu Mwenyezi Mungu (swt) amewafanya kuwa Umma bora uliotolewa kwa watu.

Sisi katika Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir tunatoa wito kwa kila mwenye ikhlasi kutoka kwa watu wenye nguvu na ulinzi kunusuru ulinganizi wetu wa kuregesha hukmu kwa yale yote aliyoteremsha Mwenyezi Mungu (swt) na kuregesha Dola ya Khilafah ambayo kwayo peke yake dhulma itaondolewa kutoka kwa kila Muislamu mwanamume na mwanamke na kutoka kwa wote wanaoishi chini ya kivuli chake. Tunawalingania wanachuoni wa Umma huu kunusuru neno la Mwenyezi Mungu ili liwe juu, kutekeleza wajibu wao. Enyi warithi wa Mitume, rekebisheni hali ya Ummah wenu na pazeni sauti zenu dhidi ya watawala wenu, linganieni umoja wa Ummah wenu na kurudi kwa mamlaka yake.

Tunamuomba kila Muislamu mwanamume na mwanamke kufanya kazi pamoja nasi katika kuinusuru Dini hii na kuifanya kuwa yenye kutawala duniani ili tuwanusuru ndugu zetu kila mahali.

Hatutawaondolea dhulma na ukandamizaji, udhalilifu na umasikini wanaoupata, isipokuwa dola isimamishwe upya kwa ajili ya Waislamu inayowahami na kuwaepusha na kila uvamizi.

Tuwamuomba Mwenyezi Mungu (swt) aviunganishe viungo vilivyotawanyika vya Umma huu, aunusuru, na aregeshe utukufu na fahari yake haraka zaidi.

 (وَكَانَ حَقّاً عَلَيْنَا نَصْرُ الْمُؤْمِنِينَ)

“...Na ilikuwa ni haki juu yetu kuwanusuru Waumini” [Ar-Rum: 47]

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.