Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
| H. 27 Jumada II 1447 | Na: H 1447 / 036 |
| M. Alhamisi, 18 Disemba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kuvunjwa Moyo Kupya: Watu wa Gaza Wanakufa kwa Baridi Baada ya Kuachwa Kuteswa na Mauaji ya Halaiki kwa Miaka Miwili!
(Imetafsiriwa)
Maafa yanayoikumba Palestina inayokaliwa kwa mabavu yanaendelea bila kukoma. Tangu kuanguka kwa Khilafah, ambayo mtawala wake aliwahi kutamka, “Palestina ni ardhi iliyonyweshwa kwa damu ya mababu zangu, na iwapo Khilafah itaanguka, mtaichukua bila malipo,” uvamizi wa Waingereza (ulioitwa Mamlaka) uliibadilisha. Na hadi leo, umbile la Kiyahudi linaloikalia kwa mabavu, lililoundwa na Uingereza na kuungwa mkono na nchi za Magharibi kwa mali yake yote, vifaa, ujuzi na uwezo wake wote, linaendelea kuwaua watu wa ardhi iliyobarikiwa, likiwafanyia ukatili vijana na wazee, na kuwatishia wafungwa kuwaua na kuwanyonga, huku ulimwengu ukitazama. Limeizingira Gaza kwa miaka mingi, likiishambulia bila kuchoka kwa ukatili usiofikirika, na kusababisha mauaji ya zaidi ya watu elfu sabiini. Na ulimwengu wa Kiislamu, pamoja na majeshi yake na wanazuoni, hutazama na kuona kama vipofu wanavyofanya, na husikia vilio vya wanawake waliofiwa kama viziwi wanavyosikia!
Kwa miaka chini ya kuzingirwa, na miaka miwili chini ya mashambulizi ya mabomu ambayo yamewaua watoto na waume zao, wanawake wa Gaza walivumilia, bila nusra yoyote, na kuonyesha ujasiri na ushujaa usio na kifani. Hata leo wanaendelea kuteseka, wengine ni kina mama wa mashahidi, wengine wake wa mashahidi, wengine mama wa watoto waliokatwa viungo, wengine wakiwa na wapendwa wao waliopotea chini ya vifusi, na wengine wakiwa na waume waliofungwa ...
Na baada ya ule usitishaji mapigano unaodhaniwa, ambao ulithibitisha kuwa haukuwa chochote zaidi ya ahadi tupu, wasuluhishi, watawala, na wapatanishi wanaendelea kula njama dhidi ya Gaza. Sio tena usaliti au kutochukua hatua tu; ni ushirikiano wa moja kwa moja. Wanadumisha mzingiro huo, wakizuia mahitaji ya kimsingi kuingia Ukanda wa Gaza, na kubaki bila kuitikia maombi ya kila siku ya wanaume, wanawake na watoto wa Gaza. Kwa kuwasili kwa msimu wa baridi kali, Ukanda huo umebadilika kihalisi na kuwa ziwa kubwa, lakini lile lililojaa miili inayotetemeka na mabaki ya magunia ya unga yaliyokusudiwa kutumika kama makaazi ya muda—magunia ambayo ulimwengu unaamini yanatosha kuwapa watu joto! Ziwa lililojaa machozi ya watoto wanaotetemeka kutokana na baridi kali, na machozi ya kina mama na baba wanaoomboleza wakilia kwa kukata tamaa, wasio na uwezo wa kuwalinda watoto wao kutokana na baridi hii mbaya.
Enyi Ummah, ambao Mtume (saw) alisema:
«مَا آمَنَ بِي مَنْ بَاتَ شَبْعَانَ وَجَارُهُ جَائعٌ إِلَى جَنْبِهِ وَهُوَ يَعْلَمُ بِهِ»
“Bado hajaniamini mimi yule anayelala akiwa ameshiba na jirani yake ubavuni mwake ana njaa, naye anajua.” Watu wa Gaza, katikati ya moyo wa ulimwengu wa Kiislamu, wana njaa na kiu, na hata wanakufa kutokana na baridi. Hadi sasa roho 14 zisizo na hatia wakiwemo watoto 6 zimeangamia kutokana na baridi kali iliyosababishwa na dhoruba na mvua kubwa iliyopelekea takriban nyumba 15 kuporomoka katika vitongoji mbalimbali vya mji wa Gaza. Timu za ulinzi wa raia bado zinajibu mamia ya miito ya kuomba msaada. Ziliongeza kuwa mahema zaidi ya 27,000 ya watu waliohamishwa yamefurika, kusombwa na mafuriko ya ghafla, au kuraruliwa na upepo mkali.
Watu wa Gaza wanapiga walia: “Hamukutuokoa kutokana na mashambulizi ya mabomu yasiyokoma, basi je mutatuokoa tusife kutokana na baridi kali?” Sisi katika Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir tunapaza kilio cha kuomba msaada kwa umma huu usioweza kufa: “Je, sio wakati sasa kwenu kulivua vazi lenu la udhaifu, kuinuka, na kuregesha izza yenu ya zamani? Gaza imeanza safari ya hadhi, hivyo kwa nini mlikata mikono yake ili kutokamilisha safari hiyo?!”
Haya ni maombi ya msaada kwa watu wa imani, na mashahidi wa Gaza wamo katika rehema ya Mwenyezi Mungu, basi musiiangushe Gaza tena, isije rehema ya Mwenyezi Mungu ikakupiteni na kwenda kwa wengine!
[إِنَّ فِي هَذَا لَبَلَاغَاً لِقَوْمٍ عَابِدِينَ]
“Hakika katika haya yapo mawaidha kwa watu wafanyao ibada.” [Al-Anbya 21:106]
Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info |