Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon

H.  6 Rabi' I 1447 Na: H.T.L 1447 / 04
M.  Ijumaa, 29 Agosti 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kinachoitwa “Tamasha za Hisia” (Zambo) jijini Tripoli ni Jaribio la Kulionyesha Jiji lisilo na Hisia zake kwa Ummah

Kwa hivyo Zisusieni na Komesheni utoaji Leseni Kwazo!
(Imetafsiriwa)

Kwa ukaidi wa wazi wa hisia za Umma na maumivu yake, na kwa ukaidi wa wazi wa Tripoli, jiji la elimu na wanazuoni, na licha ya kutolewa kwa tamko kutoka kwa Kamati ya Utunzaji wa Familia katika Dar al-Fatwa jijini Tripoli na Kaskazini kuonya juu ya njia hii hatari kwa jamii, ambapo ilikuja katika taarifa: “Kamati pia inatahadharisha juu ya hatari ya tamasha, sherehe, filamu, na mipango ambayo imejitokeza hivi karibuni katika jiji letu na ambayo yanaathiri maadili na akhlaki, na ambayo hutumiwa kupitisha ujumbe potovu chini ya kauli mbiu za kisanii au kithaqafa, katika jiji linalojulikana katika historia yake kama jiji la elimu na wanazuoni, na kama ngome ya maadili ya kweli na kitambulisho kinachounganisha. Kamati inasisitiza kwamba kuilinda jamii kutokana na hatari ni jukumu tunaloshirikiana pamoja: linaanza na familia na jamaa, kwenda hadi kwa walimu, na wanazuoni, na pia linajumuisha asasi za kiraia, manispaa, na wanasiasa, kufikia hadi kwa watoa maamuzi katika ngazi ya serikali…”

Taarifa hiyo ilizitaka pande zinazohusika - Wizara ya Elimu, Wizara ya Habari, na manispaa – kucheza dori yao katika kukabiliana na matukio haya, kwa kufafanua wazi kwa maneno yaliyoelekezwa kwa manispaa: “Kupinga utoaji leseni wa shughuli yoyote, tamasha, au sherehe ambayo inakinzana na maadili ya watu na utamaduni wao halisi...” Lakini pande husika zinafanya kama zinashambulia dhidi ya taarifa hiyo ya Kamati ya Familia katika Dar al-Fatwa, na kuziba masikio yao kwa vilio vya Waislamu mjini Gaza, majeraha na njaa zao, na hata nchini Lebanon ambayo umbile halifu la Kiyahudi linakiuka. Je, haikuwa sahihi zaidi kwa manispaa kwa jumla, na hasa manispaa ya Tripoli, kuhitimisha uunganisha matukio na manispaa katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu na Gaza yake iliyojeruhiwa, na kutafuta njia zilizopo za kutoa misaada na usaidizi kwa watu wetu huko, badala ya kufanya tamasha za densi na kuimba, kana kwamba mahitaji yote ya watu wa Tripoli yametimizwa na hakuna kitu chochote kilichosalia isipikuwa burudani ovu?

Tunatambua kwamba nyuma ya mwelekeo huu wa mara kwa mara kwa Tripoli na watu wake kuna dhamira ya ufisadi na ubadilishaji tabia ya jiji na watu wake kuanzia ngazi za juu za kisiasa nchini. Na kauli ya Mbunge Najat Saliba kuhusu mpango uliotayarishwa kukabiliana na itikadi kali jijini Tripoli (na nje ya Tripoli) ni ushahidi bora zaidi.

Enyi Watu wa Tripoli, Mashekhe wake, Wahubiri wake, Watukufu wake, na Waislamu ndani yake: Dori yenu ni kubwa katika kukomesha jambo hili na yale yanayoweza kulifuata, kwa kupaza sauti zenu kutoka kwenye mimbari na mikusanyiko yenu yote ili kususia tamasha hili na mfano wa matamasha haya potovu. Na dori yenu ni kubwa zaidi katika kuthibitisha kwamba nyinyi ni Ummah mmoja unaougua huko Palestina, Lebanon, Syria na Sudan. Je, inajuzu kwetu kuonekana kana kwamba tunacheza densi juu ya majeraha ya Ummah na maumivu yake?!

Na kwa Manispaa ya Tripoli: Tumewajua tu nyinyi kama wana wa mji huu unaomilikiwa na uhalisi wake, na kiasili mnawakilisha tabia yake na tabia ya watu wake, na matamasha ya densi na uimbaji si katika tabia yake. Tripoli ya al-Sham ilikuwa na ingali ni mwenyeji wa kila mtu ambaye anaugua maumivu licha ya maumivu yake mwenyewe, kwa hivyo musiimbe leo kando na wimbo wake, na sitisheni utoaji leseni wa tamasha.

Tunatambua ugumu wa dhurufu kwa kuzingatia hali hii ya kisekula iliyoenea nchini Lebanon na kanda, lakini pia tunatambua na tuna uhakika kwamba katika Ummah huu kumesalia kheri nyingi. Lakini kheri hii haizingatiwi wala haionekani katika uhalisia wake isipokuwa ikiwa kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَأُولَٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ * وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ تَفَرَّقُوا وَاخْتَلَفُوا مِن بَعْدِ مَا جَاءَهُمُ الْبَيِّنَاتُ وَأُولَٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ]

Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu. Na hao ndio walio fanikiwa. Wala msiwe kama wale walio farikiana na kukhitalifiana baada ya kuwafikia hoja zilizo wazi. Na hao ndio watakao kuwa na adhabu kubwa.” [Surat Aal-i-Imrān: 105].

Na tunacho kuitieni ni wito wa kheri, na kuamrisha mema, na kukataza maovu; wito wa umoja juu ya yale ambayo hayana ikhtilafu ndani yake, na hakuna mgawanyiko. Na nyinyi, enyi watu wa Tripoli, mashekhe wake, wahubiri wake, Waislamu wake, vigogo wake, na manispaa yake, mnastahiki mwitikio huu kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Basi kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu:

[وَاللَّهُ مَعَكُمْ وَلَن يَتِرَكُمْ أَعْمَالَكُمْ]

Na Mwenyezi Mungu yu pamoja nanyi, wala hatakunyimeni malipo ya vitendo vyenu.” [Surat Muḥammad: 35].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Lebanon

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
Address & Website
Tel: 009616629524
http://www.tahrir.info/
Fax: 009616424695
E-Mail: ht@tahrir.info

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.