Rais wa Lebanon Atoa Wito wa Kuidhinishwa Haraka kwa Mpango wa Trump wa Gaza!
- Imepeperushwa katika Lebanon
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Enyi Watu wa Lebanon, Enyi Watu wa Palestina, Enyi Umma wa Uislamu: Rais wa Lebanon alitoa wito wa kuidhinishwa haraka kwa mpango wa Trump wa kusimamisha vita mjini Gaza, akijua kwamba ni mpango wa kufikia maslahi ya umbile la Kiyahudi, ambalo limeshindwa kulazimisha kupitia nguvu ya silaha, kama vile kujisalimisha kwa mujahidina, kuachiliwa huru kwa wafungwa wa Kiyahudi na malengo mengine. Ili kufikia malengo haya kwa umbile halifu kupitia ujanja wa Trump.