Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
| H. 28 Jumada I 1447 | Na: H.T.L 1447 / 12 |
| M. Jumatano, 19 Novemba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mauaji Mapya Yatekelezwa na Umbile Halifu la Kiyahudi katika Kambi ya Ain Al-Hilweh!
(Imetafsiriwa)
Katika muktadha wa kile ambacho Amerika inaendesha katika suala la amani na uhalalishaji mahusiano nchini Lebanon na eneo hili—ambapo kiuhalisia ni kusalim amri na kujisalimisha—umbile halifu nyakuzi la Kiyahudi, pamoja na silaha za Marekani, risasi za Ulaya, mikono ya Kiyahudi, na ushirika rasmi wa Waarabu, lililipua uwanja wa michezo na klabu ya michezo katika kambi ya Ain al-Hilweh katika mji wa Sidon kusini mwa Lebanon mnamo Jumanne, 18/11/2025. Mashahidi kumi na tano waliauwawa katika shambulizi hili la kikatili, na makumi ya watoto na raia walijeruhiwa, katika shambulizi baya linalothibitisha uhalifu wa umbile la Kiyahudi na uadui wake dhidi ya Waislamu.
Ujumbe muhimu zaidi unaelekezwa kwa mamlaka ya Lebanon, ambayo haijakoma katika enzi hii kuzungumzia kuhusu mazungumzo na amani na umbile la Kiyahudi, ikidai kwamba ndiyo suluhisho pekee la tatizo la Lebanon nalo, huku mamlaka hii ikifuatilia kuondoa silaha kutoka kwenye kambi na nje yake, na uratibu wake unaonekana pamoja na Amerika na umbile la Kiyahudi kupitia kile ambacho kimejulikana kama “utaratibu”! Na licha ya yote yanayojitokeza katika njia hii, umbile la Kiyahudi linatupilia mbali kila makubaliano au uratibu, kwani idadi ya wale waliouawa na kujeruhiwa katika operesheni za mauaji kwa kutumia droni na mashambulizi ya mabomu baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano mnamo tarehe 27/11/2024 ikizidi elfu moja. Na hili hapa umbile halifu linaendelea na mauaji yake, likifanya mauaji dhidi ya vijana katika umri wao wa muhimu katika Kambi ya Ain al-Hilweh kwa kisingizio kwamba walikuwa wakipata mafunzo kulishambulia! Kisha linatangaza, bila kusita, vitisho kwa maeneo mengine na mashambulizi katika maeneo mengine kusini mwa Lebanon!
Shambulizi la umbile hilo kwa shabaha ya aina hii, na katika kambi za Lebanon, linaweza kuashiria njama ya kufungua tena faili la kambi za Wapalestina kwa njia ya uhalifu. Tunaionya mamlaka ya Lebanon na pande zinazofuatilia kuhusu matokeo ya kutembea njia hii au kuanguka katika mitego yake.
Ewe mamlaka ya Lebanon, je, hii ndiyo amani na mazungumzo? Je, hili ndilo umbile mnalotafuta nalo amani na uhalalishaji mahusiano?!
Kwa kuzingatia mauaji haya, tunathibitisha yafuatayo:
Kwanza: Kushambuliwa na kutishiwa kwa usalama, na uharibifu wa nyumba juu ya wakaazi wake, ni ugaidi na uhalifu wenyewe, na ni miongoni mwa aina mbaya zaidi za ufisadi ardhini.
Pili: Kuwatetea wanaokandamizwa na kuondoa uvamizi kutoka kwao ni faradhi ya kisheria. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
[وَمَا لَكُمْ لَا تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاءِ وَالْوِلْدَانِ الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْ هَٰذِهِ الْقَرْيَةِ الظَّالِمِ أَهْلُهَا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ وَلِيّاً وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ نَصِيراً]
“Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhaalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anaye toka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka kwako.’” [An-Nisa:75].
Tatu: Kuzuia uvamizi hakupatikani kupitia kulaani, kama dola zinazofanya kazi leo, ikiwemo Lebanon, wala kwa kuomba msaada kwa dola kubwa, kwani ndizo mzizi wa maradhi na mateso, wala kwa kutafuta msaada kutoka kwa Umoja wa Mataifa, kwani tangu kuanzishwa kwake umekuwa na uadui kwa Uislamu na Waislamu.
Nne: Lau ardhi za Waislamu zingekuwa, kama Mwenyezi Mungu alivyoamuru, dola moja, Ummah wa Kiislamu ungeinuka dhidi ya mtu yeyote anayesubutu kushambulia shubiri yoyote ya ardhi zetu au raia yeyote wa dola hiyo. Hatima ya wavamizi itakuwa kama hatima ya wale waliokabiliwa na Khalifa wa Waislamu al-Mu‘tasim wakati mwanamke mmoja alipomlilia baada ya kushambuliwa, kwa hivyo akafungua Amuriyya kwa ajili yake.
Tano: Kuibuka wingi wa dola katika ardhi za Kiislamu juu ya magofu ya Khilafah ya Uthmani, ambayo iliwahi kuziunganisha; kuanzishwa kwa dola hizi juu ya utaifa wa kijahiliya; kutukuzwa kwa katiba zilizotungwa na wanadamu; kuundwa kwa mipaka bandia; na kutabanniwa kwa bendera za kijahiliya badala ya bendera ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw)—yote haya yaliwawezesha maadui kutenga kila nchi peke yake bila msaada wowote kutoka kwa dola zengine kwa kisingizio cha kutoingilia mambo ya wengine. Hii ilisababisha udhaifu na udhalilifu tunayoishi leo.
Ni wakati sasa wa Waislamu kuungana na kuregesha Khilafah yao, ambayo kupitia kwayo upo wokovu wao pekee—ule unaolinda ardhi na watu, kuwaangamiza maadui, kuubeba Uislamu duniani, na kuwatoa watu kutoka kwenye giza la ukoloni na ubepari hadi kwenye nuru ya Uislamu, na kutoka kwenye dhulma ya waja hadi kwenye uadilifu wa Mola Mlezi wa waja, Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Lebanon
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Lebanon |
Address & Website Tel: 009616629524 http://www.tahrir.info/ |
Fax: 009616424695 E-Mail: ht@tahrir.info |