Afisi ya Habari
Wilayah Misri
H. 26 Muharram 1447 | Na: 1447/04 |
M. Jumatatu, 21 Julai 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kuitelekeza Gaza ni Doa katika vipaji vya Nyuso Zenu Enyi Wanajeshi wa Kinana na muhimu zaidi, ni Swali kutoka kwa Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama
(Imetafsiriwa)
Kila siku, mtoto mjini Gaza hufa kwa njaa, au mzee hupumua pumzi yake ya mwisho bila dawa, au mwanamke hufunga macho yake kwa mara ya mwisho kwa maumivu yasiyoweza kuvumilika kutokana na kiu au njaa. Kila saa mbingu hutokwa na machozi, mawe yanapiga kelele, na ardhi inawalaani wale waliowaacha peke yao. Hii ndiyo Gaza... Gaza, ambayo imezingirwa si tu kwa mipaka na vifaru, bali na uzio wa usaliti uliosukwa na viongozi wa majeshi, watawala wa khiyana, na kimya cha Umma wao.
Kinachotokea Gaza leo sio tu janga la kibinadamu, lakini uhalifu kamili, unaofanywa mbele ya macho na masikio ya ulimwengu unaodai kuwa wa kistaarabu, na kwa majeshi ambayo Umma umefadhili kwa mali yake na kujilisha kutokana na njaa yake ili waweze kuwa ngao na upanga wao ila tu kwao kutulia tuli bila kuteteleka, kana kwamba yale yanayotokea Gaza hayawahusu, au kana kwamba watu wa Gaza sio Umma wao wenyewe!
Enyi majeshi ya Ummah: je, sio wakati sasa wa damu yenu kuchemka kwenye mishipa yenu? Enyi mnaovaa vyeo vyenu na medali zenu vifuani mwenu kumbukeni kwamba dunia hii, pamoja na nyadhifa zake zote, mishahara na vyeo vyake vyote, itatoweka mara moja: wakati wa kufa usioweza kuahirishwa, muda mtakaposimama mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, bila viatu na mkiwa uchi, siku ambayo haitakufaeni mali wala hadhi, wala vyeo vyenu wala medali zenu hazitakusaidieni, wala sheria au katiba zilizotungwa na mwanadamu hazitakushufaieni.
Bali mtaulizwa kuhusu Gaza, na watu wake waliochinjwa, kuwekwa njaa, na kuteswa huku mkiwa na uwezo wa kuwasaidia, lakini hamkufanya hivyo!
Siku hiyo itakuja, na kila askari katika majeshi ya Misri, Jordan, Uturuki, na Pakistan ataulizwa: Kwa nini uliwatelekeza ndugu na dada zako huko Gaza? Kwa nini uliwaacha watoto wao wafe kwa njaa? Kwa nini uliwaruhusu wazee wao waangamie kwa kiu? Je, hukuwa na silaha? Je, hukuijua njia? Je, hukuwa na imani iliyobaki moyoni mwako?
Yanayotokea Gaza ni mtihani halisi, mtihani wa majeshi, mtihani wa imani, mtihani wa uanaume, na mtihani wa imani. Hakuna wakati mtakatifu zaidi kuliko wakati askari anapoinua silaha yake katika kuwanusuru kaka na dada zake, na hakuna wakati mtukufu zaidi kuliko pale kizuizi cha udhalilifu na utiifu wa kipofu kwa madhalimu kinapovunjwa. Wakati huo ndio ule unaoandika izza na kurekodiwa katika kitabu cha Milele, sio wakati ambapo saluti zinatolewa kwa maadui wa Ummah kwa itifaki za kijeshi!
Enyi wanazuoni, wahubiri, wanafikra, na vijana wenye ikhlasi: Msifikirie kuwa hamhusiki. Kukaa kimya ni uhalifu, na kuwa kimya juu ya kutelekezwa kwa Gaza ni kushiriki katika uhalifu. Andikeni, hubirini, kemeeni, unganisheni Ummah na sababu yake, na uunganisheni majeshi kwenye dori yao ya kweli. Ukumbusheni Ummah kuwa watoto wake wanachinjwa huku ukisalia kimya. Wakumbushe majeshi kwamba bado wana nafasi ya kuokolewa, nafasi ya mwisho ya kutupilia mbali udhalilifu, kuvunja minyororo, na kuandamana kuelekea jihad.
Enyi Wanajeshi wa Ummah kwa ujumla, na Wanajeshi wa Kinanah hasa: Wajibu wenu ni kutangaza vita kamili dhidi ya umbile nyakuzi hadi ukombozi kamili wa Palestina. Na tuna hakika kuwa hili ndilo analotamani kila mwenye ikhlasi katika jeshi la Kinanah, lakini kinachozuieni kufikia kwake ni utawala wa khiyana, ambao umeligeuza jeshi kuwa walinzi wa umbile hilo linalokalia kwa mabavu na mtekelezaji wa malengo yake. Wajibu wenu ni kuung’oa utawala huu wa khiyana kutoka katika mizizi yake, pamoja na ala na vibaraka wake wote, na kuukabidhi utawala wa nchi kwa uongozi makini wa kisiasa unaobeba mradi wa Kiislamu na wenye uwezo wa kuutekeleza mara moja. Miongoni mwenu ni Hizb ut Tahrir uongozi wa kisiasa wa ikhlasi, wenye fahamu kutoka ndani ya Ummah, unaojua masuala yake, unaobeba hamu yake, na unaojitahidi pamoja nanyi kupata radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kutekeleza sheria yake na kuibeba duniani chini ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.
[وَمَا لَكُمْ لَا تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاءِ وَالْوِلْدَانِ الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْ هَذِهِ الْقَرْيَةِ الظَّالِمِ أَهْلُهَا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ وَلِيّاً وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ نَصِيراً]
“Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhaalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anaye toka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka kwako” [An-Nisa:75]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Misri
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Misri |
Address & Website Tel: http://hizb.net/ |
E-Mail: info@hizb.net |