Afisi ya Habari
Wilayah Misri
H. 19 Safar 1447 | Na: 1447/12 |
M. Jumatano, 13 Agosti 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kuundwa kwa cheo cha "Mufti Muongofu" katika Zama za Akili Bandia Kuunda Sheria Inayoafikiana na Magharibi na Watawala wake Vibaraka
(Imetafsiriwa)
Katikati ya mporomoko wa kisiasa na kifikra wa Umma wa Kiislamu, na wakati ambapo njama dhidi ya dini yake na hukmu zake zikiongezeka, serikali tawala na zana zao - taasisi rasmi za kidini - zinazindua makongamano yenye kauli mbiu za kustaajabisha na misamiati ya uchochezi ya kiteknolojia, wakikopesha mradi wao wa kupotosha kuwa dini ni kero kwa “usasa” na “maendeleo”. Hii ni pamoja na kongamano la "Kuunda cheo cha Mufti Sahihi Katika Zama za Akili Bandia,” lililoandaliwa na Dar al-Ifta ya Misri chini ya udhamini wa moja kwa moja wa Rais Abdel Fattah el-Sisi.
Kichwa hicho kinaweza kuashiria kwamba neno "mufti muongofu" linarejelea mtu aliye na ujuzi wa kina wa kidini, uchamungu, na kushikamana na maandiko ya kidini, na kwamba akili bandia ni chombo tu cha kumtumikia. Hata hivyo, neno “muongofu” hapa linarejelea tu mtu ambaye ni mtiifu kwa mtawala, anayedhibitiwa na ajenda yake, na aliyepangiliwa kutoa fatwa zinazowiana na sera zake na kutumikia maslahi ya mabwana zake wa Magharibi.
Zama za akili bandia hazilengi kutumia teknolojia katika kuunga mkono Uislamu, bali ni kuitumia ili kudhibiti fatwa ndani ya mfumo uliowekwa, na hivyo kudhibiti fatwa na kuondoa rai yoyote halali inayopinga matakwa ya serikali au kufichua uhaini wake.
Kongamano hilo linakuja katika wakati ambapo hasira za wananchi zinaongezeka juu ya sera za serikali katika nchi za Kiislamu, na mwamko unaoongezeka miongoni mwa Umma kuhusu usaliti wa watawala katika kanuni zake msingi, kama vile kadhia ya Palestina, miungano na maadui wa Uislamu, na utekelezaji wa ukafiri (mifumo ya kikafiri).
Serikali hizi zinatambua kwamba fatwa ya dhati inayosema ukweli inaleta tishio kwa uhai wao, kwani inafichua uharamu wa utawala wao na kuwafanya wawe chini ya demokrasia ya Magharibi kafiri. Kwa hiyo, wanafanya kazi ya kufafanua upya dori ya mufti, kutoka kuwa msemaji wa hukmu ya Mwenyezi Mungu kwa kuzingatia dalili za kidini zinazotokana na wahyi, hadi kuwa mfanyikazi wa serikali ambaye anahalalisha maamuzi na kutabanni maandiko ili kuwiana na sera za serikali. Kwa maana nyengine, fatwa yake inatokana na hawaa, sio wahyi.
Akili Bandia, katika muktadha wa kongamano hili, ni ala tu ya kuweka katikati na kudhibiti fatwa. Badala ya Waislamu kumuuliza mwanachuoni mwaminifu nyumbani au msikitini kwao, wanaelekezwa kwenye "jukwaa la kidijitali" chini ya usimamizi wa serikali, ambapo algoriti zinaundwa kulingana na vigezo vya kisiasa na usalama, na kutoa tu majibu yaliyoidhinishwa pekee.
Hii ina maana kwamba fatwa itakuwa chini ya uangalizi wa pande mbili: kwanza, uangalizi wa kibinadamu na taasisi rasmi iliyo chini ya mtawala; na pili, usimamizi wa kiufundi umepangiliwa ili kuchuja maudhui yoyote ambayo yanakiuka mpaka wa kisiasa, kulaani dhuluma, wito wa jihad dhidi ya mkaliaji kimabavu, au kutaka kutekelezwa kwa Sharia kwa maisha ya kila siku ya watu.
Kwa maoni yao, "mufti mwenye busara" ndiye anayeunganisha fatwa na sheria zilizotungwa na mwanadamu na kuzifanya kuwa na mamlaka ya juu kuliko hukmu aa Mwenyezi Mungu katika utekelezaji wa vitendo. Ndiye anayeepukana na jambo lolote linalomkera mtawala au linalotishia maslahi yake, hata kama limebainishwa waziwazi katika sheria ya Kiislamu. Yeye ndiye anayeidhinisha uhalalishaji mahusiano na makafiri na wakaliaji kimabavu kwa kisingizio cha maslahi na mizani. Yeye ndiye anayehalalisha mikataba ya kimataifa inayokiuka sheria za Kiislamu kwa kudai kuwa ni "mahitaji" au "majukumu ya kimataifa."
Makongamano haya, kwa dhati yake, yako chini ya kigawanyo cha kubadilisha na kuipotosha dini, kwa sababu lengo lao msingi si kutafuta hukmu ya Mwenyezi Mungu, bali ni kuififisha na kuidhibiti dini hii na kuunda hukmu badali ambazo zimejivika guo la kuwa ni sheria ya Kiislamu, lakini ambazo kidhati ni kujisalimisha kwa hawaa na kujitenga na njia ya Mwenyezi Mungu (swt). Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:
[وَأَنِ احْكُم بَيْنَهُم بِمَا أَنْزَلَ اللَّهُ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءهُمْ] “Na wahukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao.” [Al-Ma'idah: 49]. Kuhukumu na kutoa fatwa zisizokuwa alizoteremsha Mwenyezi Mungu ni mwendelezo wa hawaa na matamanio ya mtu, kuwaridhisha watawala na mabwana zao. Hili ni jambo ambalo Mwenyezi Mungu ameharamisha kabisa. Vile vile Mtume (saw) alionya dhidi ya wanavyuoni waovu wanaoiuza dini yao kwa ajili ya pato la kiduni, akisema:
«أَخْوَفُ مَا أَخَافُ عَلَى أُمَّتِي الْأَئِمَّةَ الْمُضِلُّونَ» “Kitu ninacho kihofia zaidi kwa Umma wangu ni viongozi wanaowapoteza watu.”
Kimsingi, akili bandia inaweza kuwa chombo chenye nguvu kwa sheria ya Kiislamu, kupitia kukusanya maandiko, kudondoa maoni, na kutoa taarifa kwa watafiti. Hata hivyo, serikali zinapoiweka kwenye mikono ya taasisi zilizo chini yazo, inakuwa ni chombo hatari cha kuwekea vikwazo fatwa na kuficha rai sahihi za Kiislamu. Katika muktadha huu, akili bandia inakuwa nyongeza ya huduma za usalama, lakini kwa sura ya kisayansi na kiteknolojia, hivi kwamba muulizaji swali anadhani anaamiliana na mashini isiyoegemea upande wowote, wakati kiuhalisia anaandaliwa kwa ajenda ya kisiasa.
Madhumuni ya halisi ya kongamano hili sio kuimarisha fatwa, bali ni:
1. Kukaza mshiko wa fatwa duniani kupitia Sekretarieti Kuu ya Mamlaka na Taasisi za Fatwa Duniani kote, na kuifanya kuwa kituo kinachoratibu misimamo ya kidini kwa namna ya kuwahudumia watawala.
2. Kukuza Uislamu uliodhibitiwa ambao unakubali mipaka bandia ya kisiasa, kushikamana na sheria zilizotungwa na mwanadamu, na kuhalalisha mahusiano na maadui.
3. Kuzitenganisha fatwa kutoka kwenye siasa halali na kuziweka mbali na masuala muhimu ya Ummah, kama vile ukombozi wa Palestina, kupinduliwa kwa tawala za kidhalimu, na kupinga udhibiti wa Kimagharibi.
4. Kuhalalisha maamuzi ya watawala, ili fatwa zipatikane kwa urahisi ili kuhalalisha kila mpango, makubaliano, au muungano, hata na adui anayekalia kwa mabavu.
Makongamano haya yanatoa tishio maradufu:
Kwanza, wanazichanganya fahamu, kwani haki na batili huchanganywa chini ya bendera ya "kati na kati" na "uongofu."
Pili, yanazalisha kizazi cha mamufti wasiosubutu kusema haki na badala yake wanaona dhamira yao ni kuhalalisha chochote kinachotakwa na mamlaka.
Tatu, yanaua roho ya ijtihad, kwa sababu jukwaa la kidijitali litafupisha njia kwa kutoa jibu la umoja ambalo haliko wazi kwa mjadala.
Ni wajibu wa Ummah, wanazuoni wake, wahubiri na vijana wake, kufichua makongamano haya, kubainisha maumbile yake halisi, na kuonya dhidi ya kuchukua dini kutoka kwenye taasisi rasmi zinazopotosha maana ya neno hilo. Suala la ijtihad na fatwa lazima pia liregeshwe kwenye sehemu yake ya asili: kusema neno la haki kwa mtawala dhalimu, na kutonyenyekea kwake. Mtume (saw) amesema:
«أَفْضَلُ الْجِهَادِ كَلِمَةُ حَقٍّ عِنْدَ سُلْطَانٍ جَائِرٍ» “Jihad bora kabisa ni pale mtu anapozungumza neno la haki mbele ya mtawala dhalimu.” Ummah unahitaji wanazuoni wachamungu, sio waajiriwa au "jukwaa" linaloendeshwa na nyuzi za siasa.
Tunawaonya Waislamu dhidi ya kudanganywa na mng'aro wa teknolojia au maneno ya maua. Kipimo cha haki ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu (swt) na Sunna za Mtume Wake (saw), sio yale yanayotolewa na majukwaa ya utawala au makongamano. Kila mtu ajue kwamba akili bandia, hata iwe na nguvu kiasi gani, haiwezi kuchukua nafasi ya moyo wenye imana unaomcha Mwenyezi Mungu (swt) na ulimi mkweli unaosema ukweli. Na kwamba fatwa ni sahihi tu ikiwa imeegemezwa juu ya hukmu ya sheria ya Mwenyezi Mungu (swt) pekee, sio juu ya maagizo ya mtawala au programu yake.
[إِذْ أَخَذَ اللَّهُ مِيثَاقَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ لَتُبَيِّنُنَّهُ لِلنَّاسِ وَلَا تَكْتُمُونَهُ فَنَبَذُوهُ وَرَاءَ ظُهُورِهِمْ وَاشْتَرَوْا بِهِ ثَمَناً قَلِيلاً ۖ فَبِئْسَ مَا يَشْتَرُونَ]
“Na pale Mwenyezi Mungu alipo fungamana na walio pewa Kitabu kuwa: Lazima mtawabainishia watu, wala hamtokificha, walikitupa nyuma ya migongo yao, na wakanunua kwacho thamani duni. Basi ni kiovu hicho walicho nunua.” [Ali-i 'Imran: 187]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Misri
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Misri |
Address & Website Tel: http://hizb.net/ |
E-Mail: info@hizb.net |