Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
| H. 7 Jumada I 1447 | Na: BN/S 1447 / 06 |
| M. Jumatano, 29 Oktoba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Uvamizi wa Waliolaaniwa Haukomi
Je, kuna kiongozi anayeongozwa na Mungu ambaye atakomesha uvamizi wao na kuliondoa umbile lao?
(Imetafsiriwa)
Uvamizi dhidi ya Gaza unajirudia kama kile ambacho afisi ya mhalifu Netanyahu ilikiita “mashambulizi makali katika Ukanda wa Gaza” (Al Jazeera), ikidai kwamba Hamas ilifanya shambulizi dhidi ya wanajeshi wake katika Ukanda wa Gaza na kujibu uvunjaji wa makubaliano ya kuregesha miili - ingawa Hamas ilikana uhusiano wake na tukio la ufyatuaji risasi (Al Jazeera). Umbile hilo liliwaua zaidi ya mashahidi hamsini ndani ya masaa, huku likidai kwamba mashambulizi hayo hayamaanishi kuvunjika kwa makubaliano ya kusitisha mapigano! Na Trump anathibitisha kwamba mashambulizi ya Mayahudi hayatahujumu usitishaji mapigano!
Umbile hili la uhalifu kiasili ni la hila, linasaliti na kuifisidi dunia; lilivunja makubaliano ya amani mara mamia na limesababisha takriban mashahidi mia moja na takriban mia nne kujeruhiwa tangu kutangazwa kwa mpango muovu wa Trump ambao serikali za usaliti na ushirikiano katika ardhi za Waislamu – kutoka Uturuki hadi Pakistan na kutoka Misri hadi Hijaz – ziliukaribisha na kuusherehekea, huku zikikiri kwamba hakuna uhakika wa kusitisha uvamizi huo isipokuwa kwa kauli kama wito wa utawala wa Uturuki wa kulizuia umbile hilo kutokana na kurudi vitani!
Mandhari hiyo inaonya kuhusu kile kinachokuja katika Ukanda wa Gaza, na kwamba uvamizi wa Mayahudi hautakoma, kama inavyotokea nchini Lebanon au kile kinachotokea katika Ukingo wa Magharibi; hii ndiyo sifa yao kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema:
[أَوَكُلَّمَا عَاهَدُوا عَهْداً نَبَذَهُ فَرِيقٌ مِنْهُمْ]
“Je! Ati ndio kila wanapo funga ahadi huwapo kikundi miongoni mwao kikaivunja? Bali wengi wao hawaamini.” [Al-Baqara:100].
Na akasema Mwenyezi Mungu (swt):
[أَمْ لَهُمْ نَصِيبٌ مِنَ الْمُلْكِ فَإِذاً لَا يُؤْتُونَ النَّاسَ نَقِيراً]
“Au wanayo sehemu ya utawala? Basi hapo wasingewapa watu hata tundu ya kokwa ya tende.” [An-Nisa:53].
Aya hizi zinafichua uso wa tawala zilizoharakisha kuwaokoa mateka wa umbile hilo na miili ya askari wake, na kuwapokonya silaha mujahidina, na kupanua udhibiti wake juu ya Gaza, hata kutaka kuleta uvamizi wa kimataifa ndani ya Gaza; Kwa kumfuata Trump katika mpango wake kwa ajili ya umbile hilo halifu, serikali dhalimu zilifanikisha kwa ajili yake kile ambacho hazikufanikiwa kwa vita, na zikafanikisha kwa ajili yake kile ambacho hazikuweza kufikia kwa kupigana – kana kwamba zinaliambia: kile ambacho huwezi kufanya kwa nguvu tunakuletea kwa udanganyifu na khiyana. Hakika, waliliokoa kutoka kwenye kimbunga kilichousomba ulimwengu na kuifanya sura yake kuwa taswira ya mhalifu aliyetengwa na ulimwengu mzima; walielekeza umakini wa ulimwengu kwenye usitishaji mapigano na athari zake, na kupunguza moto wa hasira katika Ummah – hasira ambayo inakaribia kulipuka kama volkano na kuwaunguza watawala.
Yote haya yalipewa umbile la adui bila dhamana kwa watu wa Gaza kwamba kuua au kubomoa nyumba au hata kuruhusu msaada kuingia kungekoma, na bila dhamana yoyote kwamba Trump hatafanya kazi kuwahamisha watu wa Gaza – wazo ambalo anataja mara kwa mara mara kwa mara.
Usaliti na kisha ushirikiano na umbile halifu katika kuzingira Gaza na kulipa njia ya kuzingira na kuwaua watu wake, na kisha kufuata mpango wa Trump kuelekea hilo, na kuwakabidhi watu wake kwa waliolaaniwa na Wamarekani ili wawatendee wapendavyo, hurudisha kadhia hiyo mwanzo kabisa. Watu wa Gaza hawasaidiwi na malori ya misaada ambayo Mayahudi wanawahesabu dhidi yao, wala na madaktari ambao kuingia kwao kunategemea ruhusa yao, wala na ujenzi mpya ambao hivi karibuni utaharibiwa tena vichwani mwa wakaazi wake, wala na kusitisha mapigano ambayo dhamana zake zinashikiliwa na wale ambao hawatimizi maagano, na ambayo mdhamini wake ni Trump – ambaye anamwona Netanyahu kama matumizi bora ya silaha ya Amerika katika kuwaua watu wa Gaza – wala kwa makubaliano yanayofadhiliwa na wapatanishi ambao si wapatanishi bali ni washirika wa Mayahudi na walio karibu nao kuliko watu wa Gaza na mujahidina wao.
Hali ya Gaza haitarekebishwa isipokuwa na mtu atakayeregesha hatima ya Saad kwa Mayahudi katika kuwashughulikia kwake watangulizi wao kutoka Banu Quraydha — kwa kukata mizizi yao na kuzima moto wao na kung'oa ufisadi wao. Hawatasaidiwa isipokuwa na mtu anayemuiga Mtume (saw) siku ya Ushindi wa Khaybar wakati Mayahudi “محمد والخميس” waliposema “Muhammad na Jeshi Kubwa” — atakayesema kama Mtume (saw) alivyosema:
«إِنَّا إِذَا نَزَلْنَا بِسَاحَةِ قَوْمٍ فَسَاءَ صَبَاحُ الْمُنْذَرِينَ»
“Pindi tutakapofika katika uwanja wa watu, asubuhi ya walioonywa itakuwa mbaya.”
Hali ya Palestina haitarekebishwa, wala watu wake hawataokolewa au kusaidiwa isipokuwa kwa harakati za majeshi ya Uislamu – kwa kilio cha vita cha jihad na kelele za takbira, na kusonga mbele kwa vikosi vya ufunguzi; ndipo watu wa Gaza watakuwa salama na Msikiti wa Al-Aqsa na wale walio ndani yake watafurahi huku wakiinuka juu ya magofu ya viti vya utawala vya wakandamizaji. Kheri na kazi hii kubwa itafanywa tu na wale walio na ikhlasi kwa Mwenyezi Mungu miongoni mwa Ummah wa Uislamu na majeshi yake. Mwenyezi Mungu aziongoze nyoyo zao na kupanua vifua vyao ili kuinusuru Dini Yake na hilo ni jepesi kwa Mwenyezi Mungu.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Ardhi ya Baraka-Palestina |
Address & Website Tel: |