“Baada ya Kuibuka kwa (Israel) Tulikabiliana na Ulimwengu wa Kiarabu Ulioungana, na Polepole Tukaugawanya”
- Imepeperushwa katika Palestina
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Kwa maneno haya, Netanyahu anahutubia watu wake na ulimwengu, akijigamba kana kwamba amefanya hivyo. Kama ilivyo desturi ya watu wake, ni wachongezi, waongo na kudai wasichokuwa nacho! Kabla ya kuwepo kwa umbile la wale ambao Mwenyezi Mungu amewalaani na kabla ya kuvunjwa kwa Khilafah, “Ulimwengu wa Kiarabu” haukuunganishwa tu. Badala yake, ulikuwa ni umma mmoja chini ya dola moja. Umma huu haukugawanywa na nyinyi, bali mabwana zenu waliokubuni kwa uovu na hila. Mabwana wenu waliopigana na umma huu kwa karne nyingi, wakionja nguvu zake na kushuhudia kuanguka kwa miji yao mikuu mmoja baada ya mwingine. Konstantinopoli ilitekwa na dada yake (Roma) karibu kuanguka, lakini Mwenyezi Mungu akataka ibaki kuwa hifadhi kwa ushindi mpya ujao, Inshallah.