Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina

H.  6 Jumada II 1447 Na: BN/S 1447 / 09
M.  Alhamisi, 27 Novemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kampeni ya Umbile la Kizayuni katika Ukingo wa Kaskazini Magharibi ni Sehemu ya Mpango wake wa Kuimarisha Makaazi na Kuimarisha Udhibiti wake katika Eneo Hilo. Je, Hakuna Kiongozi Anayeongozwa na Mungu wa Kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa?!
(Imetafsiriwa)

Hawa hapa Mayahudi wakizidi kuwa wakali zaidi katika Ukingo wa Magharibi, wakitangaza “operesheni ya kijeshi” kaskazini mwake, wakibomoa nyumba na kuzigeuza zengine kuwa kambi za kijeshi, wakinyang'anya ardhi, wakikamata kundi la Wapalestina na kuua kundi jengine, wakiharibu mifereji ya maji na kung'oa miti, na operesheni yao ya kijeshi inaenea hadi sehemu iliyobaki ya Ukingo wa Magharibi, katikati yake na kusini yake, na hii inaendana na kile walowezi hao wanachofanya, kwa kuzingatia kutolewa kwa sheria inayowaruhusu kupata mali katika Ukingo wa Magharibi, ambayo ilitanguliwa na kufutiliwa mbali kwa sheria ya kutengwa kaskazini yake.

Jinai hizi zinasema bila shaka yoyote kwamba vitendo vyote vya Mayahudi na uvamizi wao vinalenga kuwashinikiza watu wa Ukingo wa Magharibi na kuwalazimisha kuhama, na vimegeuza maisha yao kuwa jehanamu ambayo moto wake unawaka, japokuwa kwa nguvu kidogo kuliko Gaza. Upande mwengine wa Palestina iliyojeruhiwa, watu wa Gaza wanauawa na Mayahudi kupitia njaa, kunyimwa dawa, na kuachwa uchi katika mahema ambayo hayatoi ulinzi wowote kutokana na baridi ya msimu wa baridi au joto la kiangazi. Mahema yamejaa maji kutoka juu na chini ya miguu yao, na mashambulizi ya mabomu, ubomoaji, mauaji, na mateso yamekuwa wenzi wao wa kudumu, kana kwamba yamewekwa kwenye chungu kinachochemka kwa moto wa chuki ambao umewashwa nyoyoni mwa watu wenye uadui mkubwa dhidi ya waumini.

Watu wa Gaza wote wamekabidhiwa kwa Mayahudi, na wale waliobaki katika Mujahidina kwenye mahandaki zaidi ya mstari wa manjano ambao Mayahudi walipewa (haki ya kuingia humo), baadhi yao wanauawa kwa risasi, baadhi yao wamemwagiwa zege juu ya mahandaki yao, na baadhi yao wanaachwa wafe kwa njaa kana kwamba wanapelekwa kwenye kifo kutoka pande zote, na hakuna faraja kwao na hakuna waombolezaji.

Ama kuhusu Amerika, mkuu wa ukafiri, na Magharibi pamoja nayo, ndio wahalifu wakuu. Kila uhalifu unaofanywa na umbile la Kiyahudi katika Ukingo wa Magharibi au Gaza unafanywa tu baada ya kushauriana na kituo cha Amerika huko Kiryat Gat. Misheni za upelelezi za Marekani na Uingereza bado zinafanywa Gaza ili kuunga mkono shughuli za umbile hili halifu, hadi kufikia hatua kwamba kuuawa kwa Gaza kumekuwa ni misheni ya pamoja inayoongozwa na Wamarekani, inayotekelezwa na Mayahudi na kusaidiwa na Uingereza. Al Jazeera Net hata ilichapisha ripoti iliyojadili ishara za ushiriki wa operesheni wa Wamarekani na Waingereza.

Enyi Waislamu: Palestina inakabidhiwa kwa Mayahudi bure, kwa idhini ya kimyakimya ya tawala katika nchi za Kiislamu zilizounga mkono mpango wa Trump na kisha kuunga mkono azimio la Baraza la Usalama lililoweka udhibiti wa Marekani juu ya Gaza. Walikuwa kiongozi wa mpango wa Trump, chombo kilichowarudisha wafungwa wa umbile la Kiyahudi baada ya kushindwa, mkono uliowafunga mujahidina hadi walipouawa, wabunge walioidhinisha kupokonya silaha zao na kuwalazimisha kujisalimisha, na waamuzi walioweka chakula, maji, dawa, na hata mahema mikononi mwa Netanyahu, wakimruhusu kuzuia zaidi ya kile kinachoingia. Walikuwa kikwazo cha kweli kinachowazuia Waislamu kunusuru Msikiti wao wa Al-Aqsa, na waliyafunga majeshi kuwasaidia watu na ndugu zao. Walikuwa na bado wangali ni wahalifu zaidi kwa watu wa Gaza. Hawakuwanusuru wala kuwatelekeza; badala yake, walisisitiza kuandika maangamizi yao pamoja na umbile la Kiyahudi.

Kisha Mamlaka ya Palestina, ambayo ni sawa na tawala hizi, ilifanya vitendo vibaya zaidi. Laiti ingekomea katika kulaani operesheni hiyo katika Ukingo wa Magharibi, na laiti ingekomea katika kuorodhesha makosa ya umbile la Kiyahudi. Badala yake, ilianzisha hatua kwa hoja ya kutunga sheria zinazozuia riziki za watu, kama vile sheria kuhusu mipaka ya sarafu, biashara ya mtandaoni, na deni la umma, nk. Hii ni pamoja na kutolipwa kwa mishahara ya wafanyikazi, ambayo imefanya maisha katika Ukingo wa Magharibi kuwa mapambano ya kuishi. Na hii ndiyo mamlaka ile ile iliyoidhinisha azimio la Baraza la Usalama na kutoa wito wa kupokonywa silaha kwa wapiganaji wa upinzani mjini Gaza!

Kwa kuzingatia hali hii ya kuzibwa pumzi katika Ukingo wa Magharibi, na zaidi huko Gaza, imekuwa wazi kabisa kwamba Palestina inaingia katika awamu mpya, kwamba Amerika inafanya kazi kama mlinzi wa ardhi, ikitekeleza uhalifu na mauaji ya halaiki, na kwamba tawala, ikiwa ni pamoja na Mamlaka ya Palestina, zinatoa ulinzi kwa kila uhalifu. Imekuwa wazi zaidi kuliko hapo awali kwamba mfumo wa kimataifa na Umoja wa Mataifa utawasukuma watu wa Palestina zaidi kuelekea shimoni. Ingawa ilikuwa wajibu wa Ummah na majeshi yake kuchukua hatua kwa uamuzi miaka miwili iliyopita, sasa kwa kuwa dunia na tawala zake zimeegemea upande wa Waisraeli kwa njia iliyo wazi na isiyofichwa, hatua ya taifa imekuwa muhimu zaidi na ya haraka.

Ulimwengu wa Kiislamu leo ​​unaelewa kikamilifu kwamba tawala hizi za vibaraka zimeweka rasilimali za Ummah kwa ajili ya maadui zake. Tawala hizi sasa ziko karibu zaidi kuliko hapo awali kukabidhi eneo lote—Syria, Iraq, Misri, na Bara Arabu—mikononi mwa Mayahudi na, nyuma yao, Amerika. Kimya kitasababisha tu udhalilifu zaidi, kunyeyekeshwa, na kupotea kwa eneo hili. Yote haya yanapaswa kutikisa ulimwengu wa Kiislamu hadi kwenye kiini chake, na kuulazimisha kuchukua hatua bila kuchelewa na kuangusha tawala hizi, ambazo zimepitiliza zaidi ya usaliti tu hadi uadui wa moja kwa moja dhidi ya Ummah wa Kiislamu.

Ni wakati sasa wa Ummah wa Kiislamu, pamoja na majeshi yake, kuchukua hatua kwa njia inayostahili itikadi ya Uislamu, kutafuta kimbilio kwa nusra ya Mwenyezi Mungu, ambaye kwaye hakuna kisichowezekana duniani au mbinguni. Ni wakati sasa wa kuwakumbusha maadui zake historia yake wakati ulipoongozwa na Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu na Sunnah ya Mtume Wake (saw) katika Khilafah, kuwakumbusha Hattin, Ain Jalut, Manzikert, Qadisiyah, na Yarmouk.

[قَاتِلُوهُمْ يُعَذِّبْهُمُ اللَّهُ بِأَيْدِيكُمْ وَيُخْزِهِمْ وَيَنْصُرْكُمْ عَلَيْهِمْ وَيَشْفِ صُدُورَ قَوْمٍ مُؤْمِنِينَ * وَيُذْهِبْ غَيْظَ قُلُوبِهِمْ وَيَتُوبُ اللَّهُ عَلَى مَنْ يَشَاءُ وَاللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ]

“Piganeni nao, Mwenyezi Mungu awaadhibu kwa mikono yenu, na awahizi na akunusuruni muwashinde, na avipoze vifua vya kaumu ya Waumini” [At-Tawbah 9:14]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
Address & Website
Tel: 0598819100
www.pal-tahrir.info
E-Mail: info@pal-tahrir.info

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.