Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
H. 25 Rabi' I 1447 | Na: HTS 1447 / 35 |
M. Jumatano, 17 Septemba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan
Yafanya Kisimamo katika eneo la Nile Mashariki
(Imetafsiriwa)
Leo, Jumatano, tarehe 25 Rabi’ al-Awwal 1447 H sawia na 17 Septemba 2025 M, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika eneo la Nile Mashariki walifanya kisimamo baada ya Swala ya Adhuhuri katika Msikiti Mkuu wa Souq Sitta Al-Wahda. Ndani yake, mabango yaliinuliwa kuwataka Waislamu kusimama kidete kuzuia njama ya kuichana Sudan kwa kuitenganisha Darfur.
Wakati wa kisimamo hicho, hotuba ilisomwa ikiwataka Waislamu watekeleze wajibu wao katika kuzuia njama hiyo, na kisimamo hicho kikapata maingiliano kutoka kwa hadhira ailiyokuwepo, huku idadi yao ikisimama kusikiliza hotuba hiyo.
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: 0912240143- 0912377707 http://www.hizb-sudan.org/ |
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com |