Jumatano, 20 Jumada al-thani 1447 | 2025/12/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi: Dkt. Muhammad Al-Umda Hammad

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, kwa nyoyo zilizoridhika na amri ya Mwenyezi Mungu, macho yanayobubujika machozi, na huzuni kubwa, inaomboleza mmoja wa mashababu wake aliyebeba ulinganizi wa kuregesha maisha kamili ya Kiislamu; kupitia kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, Mwenyezi Mungu amsamehe: Dkt. Muhammad Al-Umda Hammad

Soma zaidi...

Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan Wamzuru Katibu Mkuu wa Chama cha Wanasheria katika Jimbo la Al-Jazirah

Mnamo Jumanne, 2 Disemba 2025, ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, ukiongozwa na Mhandisi Mahdi Muhajir, mwanachama wa Hizb ut Tahrir, na akifuatana na Ustadh Omar Ibrahim, pia mwanachama wa Hizb ut Tahrir, na Mhandisi Walid Kamil, walimtembelea Ustadh Imad Ismail Muhammad Ahmad, Katibu Mkuu wa Chama cha Wanasheria katika Jimbo la Al-Jazirah, afisini kwake Wad Madani.

Soma zaidi...

Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan Wakutana na Mkuu wa Chama cha Wanasheria katika Jimbo la Bahari Nyekundu

Mnamo Jumatatu, 1 Disemba 2025, ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, ukiongozwa na Ustadh Nasser Ridha, Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan, akifuatana na Ustadh Abdullah Ismail, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan, walimtembelea Dkt. Imad al-Din Muhammad Hamdallah, mkuu wa Chama cha Wanasheria katika Jimbo la Bahari Nyekundu, afisini kwake Port Sudan.

Soma zaidi...

Mwaliko wa Kuhudhuria Muhadhara wa Kisiasa

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan inafuraha kuwaalika wataalamu wa vyombo vya habari, wanasiasa, na wale wote wanaopenda masuala ya umma kuhudhuria na kushiriki katika muhadhara mpya ya Kikao cha Kisiasa, ambao utawasilishwa na Ustadh Ibrahim Mushrif, mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan, wenye kichwa: Mzozo wa Kikoloni barani Afrika - Sudan kama Mfano

Soma zaidi...

Wanamgambo ni Tishio la Usalama kwa Umbo la Serikali, na Uwepo Wao ni Ukiukaji wa Sharia

Mapigano ya silaha yalitokea katika mji wa Dongola, mji mkuu wa Jimbo la Kaskazini, jioni ya Ijumaa, 21/11/2025, kati ya vikosi vya jeshi la Sudan na kikundi chenye silaha kinachojulikana kama Awlad Gamri, kaskazini mwa kituo cha usafiri wa miji. Kulingana na kile kilichoripotiwa katika habari, kiongozi wa kikundi hicho, anayeitwa Al-Tom Gamri, alijeruhiwa na kupelekwa hospitalini, na kuna habari za kuuawa kwa mlinzi wake binafsi.

Soma zaidi...

Enyi Watu wa Sudan, Amerika Inaharakisha Kuvuna Matunda ya Vita vyake nchini Sudan, Kwa hivyo Msiiruhusu Itenganishe Darfur

Wakati wa hotuba yake katika Kikao cha Uwekezaji kati ya Marekani na Saudi Arabia, Rais wa Marekani Donald Trump alisema kwamba Mfalme Mtarajiwa Mohammed bin Salman alikuwa ameomba azimio la mgogoro nchini Sudan, akiongeza kwamba alianza kusoma suala hilo nusu saa tu baada ya maelezo ya Mwanafalme huyo. Trump pia aliandika kwenye tovuti yake ya Kijamii ya Truth kwamba atatumia mamlaka ya urais kusimamisha vita mara moja.

Soma zaidi...

Ni Khilafah Rashida pekee kwa Njia ya Utume ndiyo itakayong'oa Mizizi ya Ukoloni wa Magharibi kutoka Ardhi Zetu

Kwa mwaliko wa Balozi wa Uingereza, Kumar Iyer, pamoja na Ujerumani, Ireland, Uholanzi, na Norway, Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa lilifanya kikao mnamo Ijumaa, 14/11/2025, kuhusu ukiukaji katika mji wa El-Fasher. Baraza hilo lilipitisha kwa kauli moja azimio linaloiamuru Misheni Huru ya Kutafuta Ukweli, ambayo Baraza lilikuwa limeianzisha mnamo 11/10/2023, kuchunguza ukiukaji uliofanywa katika mji huo, ambapo Baraza liliamuru kuwatambua wote waliohusika, ili kusaidia kuwafikisha mbele ya sheria. Na kama mwendelezo wa mbinu yake ya kukataa misheni hii tangu kuanzishwa kwake, Waziri wa Sheria, Abdullah Darf, alitangaza katika mahojiano na tovuti ya habari ya uchunguzi jana, Jumapili 16/11/2025, kwamba “Sudan inakataa kupeleka uchunguzi kuhusu uhalifu wa Vikosi vya Msaada wa Haraka huko Al-Fashir kwa Kamati ya Kutafuta Ukweli.”

Soma zaidi...

Hotuba ya Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan katika Mkutano na Waandishi wa Habari yenye kichwa: Makubaliano ya Nchi Nne (Quartet) ya Kusitisha Mapigano na Hatari ya Mazungumzo kwa Msingi wa Hadhara ya Kimagharibi

Tangu Quartet—ambayo inajumuisha sambamba na Amerika, Saudi Arabia na Misri na Imarati, ilipotangaza taarifa yake mnamo 12/9/2025 kuhusu mgogoro wa Sudan, watu wengi nchini Sudan wamegawanywa katika mikondo miwili: mkondo unaounga mkono taarifa ya Quartet inayotaka mazungumzo na suluhisho la kisiasa, kwa kisingizio kwamba inaleta amani, na mkondo mwengine unaosema unakataa kile kilichokuja katika taarifa ya Quartet, na kutaka kuendelea kwa vita. Na ijapokuwa pande zote mbili ni Waislamu, hawakuufanya Uislamu kuwa ndio msingi wa kutoka kwao katika kubainisha misimamo yao, wakati ilitakiwa hapo awali jambo hili litokee

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu