Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  13 Jumada I 1447 Na: HTS 1447 / 48
M.  Jumanne, 04 Novemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan Wakutana na Idadi ya Watu Mashuhuri katika Mji wa Al-Obeid
(Imetafsiriwa)

Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan ulitembelea watu kadhaa mashuhuri katika mji wa Al-Obeid, mji mkuu wa Kordofan Kaskazini, mnamo Jumatatu, tarehe 3 Novemba 2025. Ujumbe huo uliongozwa na Ustadh Al-Nadhir Muhammad Hussein Abu Minhaj, mjumbe wa Baraza la Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan, akiandamana na Mhandisi Banga Hamid na Ustadh Muhammad Saeed Bokka, wanachama wa Hizb ut Tahrir.

Ujumbe huo ulikutana na:

• - Ustadh Khalid Hussein - Mwenyekiti wa Chama cha Muungano wa Kidemokrasia, kikundi cha Jalā’ Al-Azhari.

• - Dkt. Abdullah Yusuf Abu Seel - Wakili na Profesa wa Sheria katika vyuo vikuu.

• - Sheikh Abdul Rahim Jawda - Kutoka kundi la Ansar Al-Sunnah.

• - Bw. Ahmed Muhammad - Mwandishi wa Habari wa Shirika la SUNA.

Mikutano hiyo ilizungumzia suala la wakati huu, kuanguka kwa Al-Fashir na jinai zilizotekelezwa na wanamgambo dhidi ya watu wa mji huo, na usaliti wa viongozi wa jeshi ambao walishindwa kutekeleza wajibu wao kwa watu wa Al-Fashir na kuondoa mzingiro dhidi yao, licha ya uwezo wao wa kufanya hivyo katika kipindi chote cha mzingiro na mashambulizi zaidi ya 266 yaliyoanzishwa dhidi yao.

Kisha ujumbe huo ukawapa nakala ya toleo lililotolewa na Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan lenye kichwa: “Kuanguka kwa Al-Fashir Kunafungua Njia kwa Mpango wa Amerika wa Kutenganisha Eneo la Darfur na Kuimarisha Ushawishi Wake nchini Sudan. Mpaka Lini Tutakuwa Chachu ya Mgogoro wa Kimataifa?!”

Majibu yao yalikuwa ya kupongezwa, na walitaka mikutano kama hiyo iendelee.

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.