Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
| H. 15 Jumada I 1447 | Na: HTS 1447 / 49 |
| M. Alhamisi, 06 Novemba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Amerika, Kutafuta Kuiondoa Darfur, Yaibua Suala la Abyei na Kutishia na Kuonya!
(Imetafsiriwa)
Baada ya kutenganishwa kwa Sudan Kusini na kaskazini mwaka wa 2011, eneo la Abyei liliachwa na utata na kutokuwa la upande wowote — Kusini au Kaskazini — hakukutatuliwa, ilhali kura ya maoni ilitakiwa kufanyika Abyei mwaka wa 2011, sambamba na kura ya maoni ya Sudan Kusini, ili kubaini uhusiano wa eneo hilo na Kaskazini au Kusini, lakini kura ya maoni haikufanyika kwa sababu ya mzozo wa dola hizo mbili kuhusu nani ana haki ya kupiga kura katika kura ya maoni! Eneo hilo linakaliwa na makabila ambayo ni ya Kusini, yaani kabila la Dinka Ngok, na mengine ambayo ni ya Kaskazini, yaani kabila la Misseriya, na bila shaka Wadinka hawatakubali kutenganishwa na mazingira yao ya kikabila ili kuwa na dola ya Kaskazini kwa sababu wangekuwa kiungo dhaifu zaidi katika Dola ya Sudan, na vivyo hivyo Wamisseriya hawatakubali kutenganishwa na mazingira yao ya kikabila ili kuwa na dola ya Kusini kwa sababu wao pia wangekuwa kiungo dhaifu zaidi katika dola hiyo.
Kisha vita vifupi vilianza katika eneo hilo mwaka wa 2012, lakini vilitatuliwa kwa kuanzishwa kwa Kikosi cha Usalama cha Muda cha Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Abyei (UNISFA), na mnamo Novemba 2020 Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilifanya mkutano kuhusu utekelezaji wa Azimio lake Nambari 2046 linalohusiana na masuala muhimu ya pande mbili kati ya Sudan na Sudan Kusini, na hali katika majimbo ya Kordofan Kusini na Blue Nile, bila kutoa uamuzi wazi kuhusu Abyei.
Kisha mkutano wa hivi karibuni ulikuwa jana, Jumatano 5/11/2025, ambapo balozi wa Marekani Michael Wathiz alitishia Sudan Kaskazini na Kusini kwamba angepinga kuongezwa kwa mamlaka ya vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa (UNISFA), ambayo yataisha mnamo tarehe 15 Novemba sasa, ikiwa pande hizo mbili hazitajitolea kwa majukumu yao chini ya Mkataba wa Amani ambao Sudan Kusini ilitenganishwa.
Sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan tulikuwa tumeonya kupitia taarifa kwa vyombo vya habari mnamo 21/5/2011 kuhusu hatari ya Mkataba wa Naivasha, na tulithibitisha kwamba eneo la Abyei litakuwa “Kashmir ya Sudan”; suala la mpaka linaloendelea, na sasa zaidi ya miaka 14 imepita tangu tuseme hivi, na suala la Abyei bado liko. Hili si jambo la ajabu kwa dola za kikoloni, kwani kuna maeneo yenye migogoro miongoni mwa nchi za Kiislamu; hasa eneo la Kiarabu, ambalo liligawanywa mwaka wa 1916 na Mkataba uliolaaniwa wa Sykes-Picot, na suala la mgogoro juu yake halikutatuliwa kwa sababu ni la makusudi kwa ajili yake lenyewe, na mfano mzuri wa hilo ni mgogoro kuhusu Halayib na Shalateen kati ya Misri na Sudan.
Masuala haya, ambayo kiasili yako ndani ya mipaka ya ardhi za Waislamu, hayatatatuliwa isipokuwa kwa kusimamishwa kwa dola ya Khilafah, ambayo itaunganisha ardhi zote za Waislamu, ambapo hakutakuwa na mzozo kuhusu mipaka, kwani ardhi hiyo ni ardhi ya Kiislamu chini ya kharaj au ushr, na hii inalazimisha Ummah kutaharaki ili kuisimamisha Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume, ili kukata mkono wa kafiri mkoloni anayeingilia kati ndani ya ardhi zetu.
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: 0912240143- 0912377707 http://www.hizb-sudan.org/ |
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com |