Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
| H. 29 Jumada II 1447 | Na: HTS 1447 / 70 |
| M. Jumamosi, 20 Disemba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Taarifa ya Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Sudan katika Mkutano na Waandishi wa Habari Wenye Kichwa: “Usimamizi wa Amerika wa Mgogoro wa Sudan Unazidisha Majeraha na Kugawanya Nchi”
(Imetafsiriwa)
Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Naibu Katibu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Muawiya Othman, kufuatia ziara ya Mwenyekiti wa Baraza la Mpito la Utawala na Kamanda wa Jeshi, Luteni Jenerali Burhan, nchini Saudi Arabia, Muawiya alisema mnamo Jumatatu jioni, 15/12/2025: “Rais alielezea shukrani zake kamili kwa azimio la Rais wa Marekani Donald Trump la kushiriki katika juhudi za kufikia amani na kukomesha vita nchini humo, kwa ushiriki wa Ufalme wa Saudi Arabia. Mheshimiwa alithibitisha nia ya Sudan kufanya kazi na Rais Trump, Waziri wake wa Mambo ya Nje, na Mjumbe wake Maalum wa Amani nchini Sudan, ili kufikia lengo hili zuri bila shaka.”
Taarifa ya Burhan inathibitisha kuridhika kwake kikamilifu na Amerika kusimamia mgogoro wa Sudan, kazi ambayo kimsingi imekuwa mikononi mwake tangu mwanzo wa vita. Swali linalohitaji jibu dhahiri na la wazi ni: Je, Amerika ina nia ya dhati kuhusu kufikia amani na kukomesha vita nchini Sudan? Zaidi ya hayo, kama Waislamu, kwanza je, inaruhusiwa, kulingana na sheria ya Kiislamu, kwa dola ya kikafiri ya kikoloni kusimamia mambo yetu?
Ili kujibu maswali haya mawili, kwanza tutahutubia sehemu ya kwanza, tukifafanua kama Amerika imejitolea kweli kutatua mgogoro huo, kufikia amani, na kumaliza vita kupitia mkutano huu. Kisha, tutajibu swali la pili kwa dalili ya kisheria ya Kiislamu.
Inajulikana vyema kwamba vita hivi vilianzishwa na Amerika ili kuzuia kinachoitwa Muundo wa Makubaliano, ambao ungehamisha mamlaka kwa raia—watu wa Uingereza nchini Sudan—na kukomesha udhibiti wa jeshi linaloungwa mkono na Marekani. Kwa hivyo, tangu kuzuka kwa vita mnamo 15/4/2023, maafisa wa Marekani wamesema kwamba vita hivi havitakwisha kwa ushindi wa kijeshi kwa upande wowote ule. Licha ya ukweli kwamba Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) hapo awali havikuwa na uwezo wa kukabiliana na jeshi, walilazimisha usitishaji mapigano katika Mkutano wa Jeddah, ambao ulianza chini ya wiki moja baada ya vita kuanza. Hii iliwaruhusu kujipanga upya kupitia Imarati, kwa idhini kutoka Marekani. Marekani ilizuia Ulaya, haswa Uingereza, kuingilia kati katika mzozo huo na kudumisha udhibiti juu yake. Inasimamia mzozo huo ili kutumikia maslahi yake, hata ikitumia baadhi ya vibaraka wake wa kiraia kutekeleza majukumu fulani, pamoja na Muungano wa Afrika. Pia ilitumia Umoja wa Mataifa kwa kufanya vikao kadhaa vya Baraza la Usalama kuhusu Sudan, bila kutoa azimio lolote la kukomesha vita.
Amerika iliendelea kudai kutokuwa na uwezo wa kutatua mgogoro huo hadi RSF ilipoweza kutwaa udhibiti wa eneo lote la Darfur na maeneo makubwa ya Kordofan Magharibi na Kaskazini, walipoanza kufanya kazi kupitia kile kinachoitwa Quartet (Quad), ambayo ilijumuisha Imarati, Misri, na Saudi Arabia.
Ili kupata muda zaidi, jeshi liliagizwa kukataa Quad, kisha kumtuhumu Masaad Boulos kwa kupendelea Vikosi vya Msaada wa Haraka, ikifuatiwa na madai kwamba serikali haitakubali Quad maadamu Imarati inashiriki. Kisha ukaja udanganyifu wa Mfalme Mtarajiwa wa Saudi Arabia, ambaye alimwomba Trump kuingilia kati ili kutatua mgogoro huo nchini Sudan, na kumalizika katika ziara ya hivi karibuni ya Burhan nchini Saudi Arabia.
Kauli hizi, ambazo tulizitaja mwanzoni mwa mkutano huu, na katika kipindi hicho, Burhan alikutana kwa siri na Masaad Boulos huko Uswisi, kisha Misri, na hatimaye Saudi Arabia, bila kufichua yaliyotokea katika mikutano hii. Hii inathibitisha kwamba Amerika ina udhibiti mzuri wa faili, si kwa ajili ya kupata amani au kusimamisha vita, bali kwa ajili ya kutenganisha Darfur na Sudan, ikiwa tayari imeanzisha mandhari ya mtindo wa Libya huku kukiwa na serikali moja huko Darfur na nyengine katika sehemu iliyosalia ya Sudan.
Katika mazingira haya, licha ya kauli kutoka kwa viongozi wa kijeshi kwamba wameazimia kuikomboa Kordofan yote na Darfur, hakuna hatua kali za kijeshi zinazochukuliwa. Hii ni kwa sababu, kama tulivyosema, Amerika haitaki jeshi lipate ushindi wa kijeshi dhidi ya Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF). Kwa hivyo, inasema mara kwa mara kwamba hakuna suluhisho la kijeshi kwa mzozo nchini Sudan. Kauli ya hivi karibuni kuhusu jambo hili ilikuwa mnamo Juni 2025, wakati msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Tammy Bruce alisema katika mkutano na waandishi wa habari: “Mzozo nchini Sudan hauwezi kumalizika kijeshi.” Zaidi ya hayo, Amerika, ambayo inalinganisha jeshi na RSF, haijachukua hatua yoyote dhidi ya uhalifu na ukatili uliofanywa na RSF, ikiwa ni pamoja na mauaji ya raia wasio na hatia, ukiukaji wa heshima, uporaji wa mali na pesa, na uharibifu wa miundombinu. Hii ni kwa sababu RSF ndiyo chombo ambacho Amerika itatenganisha Darfur. Zaidi ya hayo, Amerika ndiyo iliyotenganisha Sudan Kusini kwa jina la kinachoitwa amani, kama walivyokiri viongozi wa utawala wa zamani. Mazungumzo yake ya sasa kuhusu umoja na amani ya Sudan si chochote ila ni hadaa ili kufikia malengo yake katika vita hivi.
Simulizi hii, miongoni mwa nyenginezo, inatuthibitishia kwamba Amerika haipendi amani Sudan na kusimamisha vita.
Ama jibu la sehemu ya pili ya swali, hairuhusiwi kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu kuanzisha uhusiano nao, sembuse kusalimisha ubwana wetu kwao kwa kuwaruhusu kusimamia mgogoro katika nchi yetu. Mwenyezi Mungu (swt) anatwambia tusiwape makafiri mamlaka juu yetu. Yeye, Azza Wa Jal (Aliyetukuka) asema:
[وَلَن يَجْعَلَ اللَّهُ لِلْكَافِرِينَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ سَبِيلاً] “wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini.” [An-Nisa:141]. Zaidi ya hayo, Marekani, kwa kuwa ni taifa Kafiri, haiwezi kuleta kheri yoyote, kama Mwenyezi Mungu (swt) anavyosema:
[مَا يَوَدُّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَلَا الْمُشْرِكِينَ أَنْ يُنَزَّلَ عَلَيْكُمْ مِنْ خَيْرٍ مِنْ رَبِّكُمْ وَاللَّهُ يَخْتَصُّ بِرَحْمَتِهِ مَنْ يَشَاءُ وَاللَّهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ]
“Walio kufuru miongoni mwa watu wa Kitabu na washirikina hawapendi mteremshiwe kheri yoyote kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Na Mwenyezi Mungu humkusudia kumpa rehema yake ampendaye. Na Mwenyezi Mungu ni mwenye fadhila kubwa.” [Al-Baqarah:105]. Je, kheri inawezaje kutoka kwa mtu ambaye hatutakii kheri kutoka kwa Mola wetu Mlezi?! Zaidi ya hayo, Amerika ni adui, si rafiki, Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[إِنَّ الْكَافِرِينَ كَانُوا لَكُمْ عَدُواً مُبِيناً] “Hakika makafiri ni maadui zenu walio wazi wazi.” [An-Nisa: 101]. Kwa hivyo, hukmu ya kisheria ni kwamba Amerika ni dola adui na ya kivita, na ndiyo iliyowaua ndugu zetu nchini Iraq, Afghanistan, na hivi karibuni mjini Gaza.
Kifungu cha 189 cha Rasimu ya Katiba ya Dola ya Khilafah kinasema yafuatayo:
“3- Dola ambazo hatuna mikataba nayo, na dola halisi za kibeberu, kama vile Uingereza, Amerika na Ufaransa, na zile dola ambazo mipango juu ya Dola, kama vile Urusi zinachukuliwa kisheria kuwa dola za kivita. Tahadhari zote lazima zichukuliwe dhidi yao na itakuwa vibaya kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia nazo. Raia wao wanaweza kuingia katika Dola ya Kiislamu, lakini tu wakiwa na pasipoti na visa maalum kwa kila mtu, na kwa kila ziara, isipokuwa ziwe za kivita kivitendo.
4- Dola ambazo ni za kivita kivitendo kama vile Israel, kwa mfano hali ya kivita lazima ichukuliwe kama msingi wa miamala yote nazo. Lazima zishughulikiwe kana kwamba kuna vita halisi kati yetu, bila kujali kama kuna usitishaji wa mapigano kati yetu au la. Na raia wao wote wanazuiwa kuingia katika Dola.”
Suluhisho msingi kwa matatizo ya Ummah liko katika kusimamisha dola inayoweka haki na kulinda nchi kutokana na kusambaratika na mgawanyiko, dola inayokata mkono wa mkoloni kafiri anayeingilia nchi yetu, akitamani utajiri wetu, na kuharibu kitambulisho chetu. Ni dola ya Kiislamu ambayo Mtume wa Uislamu aliiamuru: Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: 0912240143- 0912377707 http://www.hizb-sudan.org/ |
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com |