Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
| H. 17 Dhu al-Hijjah 1447 | Na: HTS 1447 / 125 |
| M. Jumatano, 03 Juni 2026 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Jibu kwa Mwandishi wa Makala (Usekula na Ugumu wa Historia ya Uislamu Iliyoghushiwa)
(Imetafsiriwa)
Tulikumbana na makala moja ya mwanahabari ambayo yalizua hisia tofauti kwenye mitandao ya kijamii. Makala hayo yalikuwa na kichwa: (Usekulariand na Ugumu wa Historia ya Uislamu Iliyoghushiwa)!
Kujibu baadhi ya hoja zilizotolewa katika makala hayo, tunasema:
Kwanza: Kauli za mwandishi zinadhihirisha kutoujua kwake Uislamu, na kumpelekea kutunga uongo kuhusu Uislamu na hukmu zake, na kusema ya batili. Ili kufanya uadilifu, hapa kuna andiko ambalo ndani yake alitunga uongo kuhusu Uislamu: (Katika historia yake yote, Uislamu haujawahi kufanya usawa baina ya watu wa imani tofauti katika dola yoyote iliyoanzishwa na Waislamu. Majeshi yangetembea kutoka Bara Arabu, yakiteka nchi za Asia, Ulaya, na Afrika, na kuwawasilishia wakaazi wa nchi hizo machaguo matatu tu: kusilimu, kulipa jizya (kodi) huku wakiwa madhalili, au vita, ambapo, ikiishia kwa ushindi wa Waislamu, hupelekea utumwa wa wanaume, kutekwa nyara kwa wanawake, na kuchukuliwa kwa mali kama ngawira za vita...)!
Kwanza, mwandishi anakiri kwamba vita vya Waislamu (jihad) vilikuwa ni ufunguzi, sio ukoloni au uvamizi. Zaidi ya hayo, machaguo hayo tatu yalikuwa kabla ya vita, sio baada ya ukombozi, kama alivyosema.
Aliyeamrisha kupigana na makafiri ni Mola Mlezi wa walimwengu wote, na Yeye ndiye aliyeweka jizya kwa wale ambao hawakuingia katika Uislamu, lakini wakatosheka kuishi na Waislamu chini ya hukmu za Uislamu. Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[قَاتِلُواْ الَّذِينَ لاَ يُؤْمِنُونَ بِاللّهِ وَلاَ بِالْيَوْمِ الآخِرِ وَلاَ يُحَرِّمُونَ مَا حَرَّمَ اللّهُ وَرَسُولُهُ وَلاَ يَدِينُونَ دِينَ الْحَقِّ مِنَ الَّذِينَ أُوتُواْ الْكِتَابَ حَتَّى يُعْطُواْ الْجِزْيَةَ عَن يَدٍ وَهُمْ صَاغِرُونَ]
“Piganeni na wasio muamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Mwisho, wala hawaharimishi alivyo harimisha Mwenyezi Mungu na Mtume, wala hawashiki Dini ya Haki, miongoni mwa walio pewa Kitabu, mpaka watoe kodi kwa khiari yao, hali wamet'ii.” [At-Tawbah 9:29]. Mwandishi huyu, anayedai kuwa ni Muislamu, anapinga neno na hukmu ya Mwenyezi Mungu!
Ama kauli yake: (Au vita ambavyo, vikiishia kwa ushindi wa Muislamu, inapelekea kuwafanya wanaume kuwa watumwa, kuwakamata wanawake na kunyakua mali...), hii ni kauli ya uongo ambayo hata maadui wakubwa wa Uislamu wasingeitamka! Endapo Waislamu walishinda katika ukombozi wao katika vita vyovyote dhidi ya makafiri, hukmu za Uislamu zilitekelezwa, na watu waliachwa kwenye imani na ibada zao wenyewe. Kama jambo hilo lingekuwa kama anavyodai mwandishi, ardhi zote za Waislamu zingekuwa watumwa leo. Bali, Uislamu ulikuja kuwakomboa watu kutoka katika utumwa wa watumwa kwenda kwenye utumwa wa Muumba wa watumwa.
Pili, mwandishi alisema: (Uislamu ni dini inayojumuisha mwongozo wa kiroho, maudhui ya kiakhlaki, na mtazamo wa kiujumla wa wanadamu na maisha upande wa maana na makusudio...nk.). Huu ni mkanganyiko wa wazi. Je, Uislamu unawezaje kuwa dini inayojumuisha mwongozo wa kiroho na maudhui ya kiakhlaki huku wakati huo huo ukitoa mtazamo kamili wa wanadamu na maisha kwa maana na madhumuni?
Uislamu ni itikadi ya kiroho na kisiasa ambayo ilikuja kushughulikia matatizo ya wanadamu, kwa kutambua kwamba wanadamu wana silika (ghariza) na mahitaji ya kimwili ambayo yanahitaji kushibishwa. Uislamu umebainisha jinsi mahitaji haya yanavyopaswa kukidhiwa bila ya ziada au upungufu, kupitia hukmu kutoka kwa Mwenye hekima, Mjuzi wa yote. Yeye aliyewaumba wanadamu anajua kipi kuna manufaa na kipi kina madhara kwao! Ukosefu wa elimu wa mwandishi juu ya hukmu hizi haumwondolei jukumu; badala yake, unasisitiza kutoujua kwake Uislamu.
Tatu: Mwandishi anasema katika makala yake: (Lazima tuache kurudia madai kwamba tuliitangulia Ulaya katika haki, uhuru, na usawa. Hizi ni propaganda tu, madai, na upendeleo wa kihisia, kifikra. Ulaya ilizalisha Azimio la Ulimwengu la Haki za Kibinadamu, ndege, treni, kompyuta, sayansi ya kisasa nk.). Je, mwandishi anazungumzia haki gani ya Ulaya?! Historia ya Ulaya, ya zamani na ya kisasa, ni historia ya ukoloni, iliyojaa dhulma dhidi ya watu walio madhaifu, haswa barani Afrika. Hakika, ulimwengu wa leo unatambua tu wenye nguvu. Maneno na matendo ya rais wa demokrasia kubwa zaidi duniani, na ujambazi anaofanya—ambao hata washirika wake hawajasalimika—ni ushahidi tosha. Ama kuhusu yale wanayosema juu ya uhuru, ni uhuru wa ufisadi na ukiukaji wa silika (ghariza) ya kimaumbile. Ni uhuru wa wanaume kuoa wanaume na wanawake kuoa wanawake. Ni uhuru wa Epstein—na Epstein alikuwa fedheha iliyoje!
Ama kuhusu dola ya kitaifa ya kisasa, ndiyo, ilikomesha kwa muda mfupi vita visivyokwisha vilivyokuwa vikiendelea kati yao.
Ama kuhusu sisi, dola za kitaifa tulizoundiwa ni dola vikaragosi tu, kusudi lao likiwa ni kutumikia maslahi ya wakoloni. Wanawapandikiza watawala na kuwaondoa, na watu wa nchi zote za Kiislamu wanakandamizwa. Kama sio makafiri, Magharibi ya kikoloni, watawala hawa wanaowakandamiza watu wao wasingebaki madarakani hata siku moja. Mfano wa kuridhika kwa watawala wa Magharibi na watawala wa Waislamu ni kile Trump alichosema kuhusu mtawala wa Misri, akimwita dikteta wake kipenzi! Hili linaakisi kikweli maoni ya watawala wote wa Magharibi, isipokuwa kwamba wengine ni wanafiki.
Ama kuhusu haki za binadamu, ni uzushi wa Magharibi. Kwao wanamaanisha haki za binadamu za Wazungu weupe, bila kujali viumbe vyengine vya Mwenyezi Mungu. Kile ambacho umbile la Kizayuni lilifanya mjini Gaza, kwa msaada wa demokrasia kubwa zaidi duniani, kinatosha, katikati ya kimya cha watawala wa ulimwengu unaoitwa uliostaarabika, wanaodai kutetea haki za binadamu. Zaidi ya hayo, mwandishi anaunganisha sayansi na matokeo yake na utawala pamoja na siasa, na hukmu pamoja na fikra. Ndege, treni, na sayansi ya kisasa zina uhusiano gani na utawala na siasa?! Cha kushangaza, anataja China, ambayo inawakandamiza Waislamu wa Uyghur huko Turkestan Mashariki!
Nne: Mwandishi alisema katika makala yake: (Sasa tuko nyuma, tunawezaje kuepuka kurudi nyuma huku...?), na katika jibu lake anasema: (Vivyo hivyo, lazima tusonge mbele zaidi ya wazo kwamba Uislamu ni dini na dola, yaani, tusonge mbele zaidi ya hadithi kuu ya ngano ambayo kwayo makundi ya kisiasa ya Kiislamu yameasisiwa).
Tunamwambia, ndio, tuko nyuma, si kwa sababu tunashikamana na Uislamu au kwa sababu tunatawala kwa sheria ya Kiislamu, lakini kinyume chake kabisa. Uislamu ni kujisalimisha na utiifu kwa Mwenyezi Mungu (swt), Mola wa Walimwengu, na mwandishi huyu na wale walio pamoja naye wanataka tujisalimishe na kutii viumbe vilivyoumbwa kama sisi, ambao pia ni makafiri. Na Mwenyezi Mungu (swt) anatuonya dhidi yao, hawa makafiri, akisema:
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ لاَ تَتَّخِذُواْ الْيَهُودَ وَالنَّصَارَى أَوْلِيَاء بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاء بَعْضٍ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ إِنَّ اللّهَ لاَ يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ]
“Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.” [Al-Ma'idah :51].
Wazo kwamba Uislamu ni dini ambayo kwayo dola inatoka ni kanuni kuu ya Uislamu. Kwani yeyote anayetabikisha hukmu za Uislamu, kimsingi, ni dola inayotekeleza sheria za utawala, siasa, uchumi, jamii, na nyanja nyenginezo. Na Mwenyezi Mungu (swt) ametuamrisha kutekeleza sharia yake, kama alivyosema Yeye (swt):
[فَلاَ وَرَبِّكَ لاَ يُؤْمِنُونَ حَتَّىَ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لاَ يَجِدُواْ فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجاً مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُواْ تَسْلِيماً]
“La! Naapa kwa Mola wako Mlezi! Hawataamini mpaka wakufanye wewe ndiye muamuzi katika yale wanayo khitalifiana, kisha wasione uzito katika nyoyo zao juu ya hukumu utayo toa, na wanyenykee kabisa.” [An-Nisa 4:65]. Mtume Mtukufu (saw) ndiye aliyetunasihi, tukitaka kuokoka, tufuate Sunnah zake katika utawala na siasa, na Sunnah za Khulafaa Rashidun (Makhalifa waongofu) baada yake, akisema: «فَإِنَّهُ مَنْ يَعِشْ مِنْكُمْ فَسَيَرَى اخْتِلَافاً كَثِيراً، فَعَلَيْكُمْ بِسُنَّتِي وَسُنَّةِ الْخُلَفَاءِ الرَّاشِدِينَ الْمَهْدِيِّينَ، فَتَمَسَّكُوا بِهَا وَعَضُّوا عَلَيْهَا بِالنَّوَاجِذِ، وَإِيَّاكُمْ وَمُحْدَثَاتِ الْأُمُورِ فَإِنَّ كُلَّ مُحْدَثَةٍ بِدْعَةٌ، وَكُلَّ بِدْعَةٍ ضَلَالَةٌ» “Yeyote miongoni mwenu atakayeishi ataona khitilafu nyingi. Basi shikamaneni na Sunnah zangu na Sunnah za Makhalifa walioongoka na zikamateni kwa majego yenu, na jihadharini na mambo mapya yaliyozushwa, na kila jambo lililozushwa ni uzushi, na kila uzushi ni upotovu.” Baada ya onyo hili, mwandishi anatutaka tuuache mfumo wa Kiislamu na hukmu zake, na tufuate fikra potofu za makafiri, kama vile usekula, demokrasia, ubepari, ukomunisti na matamanio mengine ya makafiri?!
Tano: Mwandishi anahitimisha makala yake kwa kusema: (Hakuna mtu barani Ulaya anayeota kurudisha Baraza la Kuhukumu Wazushi, kwa mfano, au biashara ya utumwa, lakini baadhi ya Waislamu wanaota kutekeleza adhabu ya uasi, kurudi kwa enzi ya ufunguzi wa Kiislamu, masuria, mateka, na kurudi kwa Khilafah). Tunamwambia kwamba Khilafah, ambayo hutaki Waislamu watawaliwe nayo, ndiyo njia pekee ya kuwaokoa kutokana na tawala dhalimu na udhalimu wa watawala wa dola za dhulma. Zaidi ya hayo, ni faradhi, si matamanio au ndoto tu, na itakuja licha ya ukafiri wa Magharibi na washirika wake, kwani ni ahadi ya Mwenyezi Mungu (swt), ambaye amesema:
[وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُم فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْناً يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئاً وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَلِكَ فَأُوْلَئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ]
“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [An-Nur 24:55]. Hii ni bishara njema ya Mtume (saw) ya kurudi kwa Khilafah Rashida kwa njia ya Utume baada ya utawala wa kidhalimu tunaoishi ndani yake zama hizi. Yeye (saw) asema katika hadith iliyosimuliwa na Imam Ahmad: «ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ. ثُمَّ سَكَتَ» “Kisha utakuwepo utawala wa kutenza nguvu, na utakuwepo kwa muda apendao Mwenyezi Mungu uwepo kisha atauondoa apendapo kuuondoa. Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume. Kisha akanyamaza.”
Kwa kumalizia, tunamwambia mwandishi: Ndiyo, historia ya Uislamu imepotoshwa, lakini si, kama unavyodai, kwa ajili ya Uislamu. Badala yake, imepotoshwa kwa ajili ya maadui zake. Wale walioandika historia ya Uislamu walikuwa Orientalisti, maadui wa Uislamu—na unajua nini kuhusu Orientalisti? Kwa bahati mbaya, baadhi ya Waislamu walioandika historia wamechukua kutoka kwao, na wewe pia unachukua kutoka kwao! Zaidi ya hayo, Uislamu hautokani na historia, wala kutoka kwa tafsiri za kibinadamu, bali kutoka kwa vyanzo vyake: wahyi, Kitabu cha Mwenyezi Mungu (swt) na Sunnah ya Mtume Wake (saw).
Tunamwomba Mwenyezi Mungu atuongoze sisi na mwandishi, kwani Yeye ndiye Mlinzi wa hilo na ana uwezo wa kufanya hivyo.
Wa Assalamu alaikum wa Rahmatullah wa Barakatahu
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: 0912240143- 0912377707 http://www.hizb-sudan.org/ |
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com |