Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Syria

H.  16 Dhu al-Hijjah 1446 Na: 20 / 1446 H
M.  Jumamosi, 14 Juni 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Tahadharini kwamba Kuondelewa Vikwazo vya Marekani kunaweza kuwa Utangulizi wa Kupoteza Ubwana na Utangulizi wa Uhalalishaji Mahusiano na Mayahudi
(Imetafsiriwa)

Rais wa Syria Ahmed al-Sharaa alikutana na mwenzake wa Marekani, Donald Trump, katika mji mkuu wa Saudi, Riyadh, mnamo Jumatano, kando ya mkutano wa kilele wa Ghuba na Marekani. Mfalme matarajiwa wa Saudia Mohammed bin Salman alihudhuria mkutano huo, huku Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan akishiriki kwa njia ya video, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Saudia.

Ikulu ya White House ilifichua mnamo Jumatano sehemu ya mazungumzo yaliyofanyika kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na Rais wa Syria Ahmad Al-Sharaa wakati wa mkutano wao jijini Riyadh mnamo siku ya Jumatano. Msemaji wa Ikulu ya White House alisema kuwa Trump alitoa wito kwa Al-Sharaa kujiunga na Mkataba wa Abraham na umbile la Kiyahudi. Trump pia alitoa wito kwa al-Sharaa kuyatimua makundi ya Wapalestina ambayo Washington inayataja kama "magaidi" kutoka Syria na "kuisaidia Marekani kuzuia kuibuka tena kwa ISIS."

Kwa upande wake, Al-Sharaa ilimfahamisha Trump kwamba anakaribisha makampuni ya Marekani kuwekeza katika sekta ya mafuta na gesi ya Syria, kwa mujibu wa White House.

Trump alitangaza mnamo Jumanne nia yake ya kuondoa vikwazo vilivyowekwa na nchi yake dhidi ya Syria.

Tukianza na mada ya vikwazo, ingawa kila mtu mwenye ikhlasi atafurahi kupunguza mizigo ya kiuchumi (ikiwa itatokea) kwenye mabega ya watu wa Ash-Sham, tunakumbuka maneno ya Mwenyezi Mungu:

[مَّا يَوَدُّ الَّذِينَ كَفَرُواْ مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَلاَ الْمُشْرِكِينَ أَن يُنَزَّلَ عَلَيْكُم مِّنْ خَيْرٍ مِّن رَّبِّكُمْ]

“Walio kufuru miongoni mwa watu wa Kitabu na washirikina hawapendi mteremshiwe kheri yoyote kutoka kwa Mola wenu Mlezi.” [Al-Baqara 2:105]. Tunathibitisha kwamba kuendelea kwa vikwazo, kwenyewe kulikiwa kuko mara hakuko, uhalifu mkubwa dhidi ya watu wa Ash-Sham, na hata kama vilisababishwa na utawala wa uliopita, sababu ya hili imetoweka. Kwa hiyo, kuviondoa si neema inayotolewa na maadui wa Uislamu kwa watu wa Ash-Sham. Tunasisitiza kuwa Trump na nchi za Magharibi kwa jumla hazitoi chochote bila malipo. Wanachotaka kutoka Syria kinahusishwa na masuala ambayo yanaathiri moja kwa moja ubwana wake, kwani wanaweka maafikiano mengi ya: kiusalama, kisiasa na kiuchumi. Haya ni pamoja na masuala ya utegemezi, "Mkataba wa Abraham," kuhalalisha mahusiano na umbile la Kiyahudi, na "kupambana na itikadi kali na ugaidi." Wanatulazimishia mfumo wa kisekula na katiba juu yetu ambayo ni ngeni kwa imani yetu, na wananyonya mali ya nchi kutumikia maslahi yao na sio yetu.

Ni muhimu kutaja kwamba watawala wa tawala za kisekula katika nchi za Kiislamu, wanaofuja mamia ya mabilioni ya pesa za Ummah kwa kisingizio cha "uwekezaji," katika kuitumikia Amerika, ili kuifurahisha, kulinda maslahi yao, na kuhifadhi viti vyao vya utawala, hawatajali maslahi yetu, na kamwe hawajawahi kuyajali.

Mfalme mtarajiwa wa Saudia Mohammed bin Salman anauza mali na rasilimali za Syria, kama alivyofanya alipouza mali na rasilimali za Saudi Arabia. Anauza asichokimiliki kwa wasiostahiki, kwa sababu rasilimali hizi na mali nyingine za umma ni za Waislamu. Khilafah ya Kiislamu inasimamia uchimbaji na usambazaji wake kwa raia wa dola. Ni haramu kupeana manufaa au kuhitimisha mikataba inayohusiana na jambo lolote linalohusiana na mali ya umma, ikiwa ni pamoja na mafuta, gesi, madini na mali nyenginezo.

Mamia ya mabilioni ya dolari ambazo Bin Salman alimkabidhi Trump bila yeye kupepesa macho, lau zingetumika kwa Waislamu na maslahi yao, zingetosha kuwaletea ustawi na maendeleo.

Kilichotokea leo nchini Saudi Arabia ni jambo zito ambalo haliwezi kupuuzwa. Yeyote anayejua umbile halisi la Amerika na fikra zake kwa jumla, na yeyote anayejua mawazo ya Trump na jinsi anavyokabiliana nayo, ataelewa uzito wa kile kilichotokea. Trump ni bepari anayejua jambo moja tu: kupora mali na rasilimali za watu na kuimarisha udhibiti wa Amerika juu yao.

Kujisalimisha kwa majaribio ya Amerika ya kulazimisha makubaliano ya kuhalalisha mahusiano na umbile la Kiyahudi na "Mkataba wa Abraham" ni kosa la hatari na kubwa ambalo halipaswi kufanywa. Bali, ni lazima likabiliwe kwa nguvu zote. Kadhia ya Palestina ni suala la imani na dini, na ni jambo la Waislamu wote. Chini ya hali yoyote hawawezi kuiacha kuwa thamani ya kiti kibovu cha mamlaka, ambacho kiongozi wake ataruhusiwa tu kubaki imara kwa muda mchache pekee.

Sera za kiburi za Rais Trump wa Marekani haziwezi kukabiliwa na jibu lile lile kutoka kwa watawala wa nchi za Waislamu, wanaonyenyekea na kufuja mali, rasilimali na mamlaka ya Waislamu, wakifanya wanavyoamrishwa. Bali, ni lazima tuchukue misimamo yenye maadili iliyowekwa juu yetu na imani ya Kiislamu na hukmu za kisheria zinazochipuza kutokana nayo, bila ya kuogopa lawama za yeyote kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.

Yeyote anayetafakari yaliyotokea Saudi Arabia, mbele ya Bin Salman na kwa baraka za Erdogan, ambaye anashikilia mkono wa juu na mwenye usemi wa mwisho juu ya serikali mpya ya Syria, na sisi, ambao tumepitia sera zake katika kipindi chote cha miaka duni ya mapinduzi, tutaelewa kikamilifu ukubwa wa mtelezo hatari na shimo kubwa ambalo wametutumbukiza ndani yake, na jinsi walivyouza nchi yetu na watapora rasilimali zetu, haswa gesi na mafuta, ambazo ni mali ya wananchi na hakuna mwenye haki ya kuzitumia atakavyo.

Kukubali Mkataba wa Abraham na kuhalalisha mahusiano na umbile la Kiyahudi, ambalo linawaua watu wetu huko Gaza na kwengineko, kukalia kimabavu maeneo yetu matakatifu, na kunyakua Msikiti wetu wa Al-Aqsa, ni janga kubwa na jinai kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu na waja wake waaminifu.

Kilichotokea ni jambo zito sana katika vipimo na nyanja zake zote. Hatupaswi kutumbukia ndani yake. Bali, ni lazima tupinge na kuonya dhidi ya kuendelea nalo, hasa hivi sasa kwa kuwa tumejua kuhusu pande zake husika, historia yao kwetu, na dori yao ya hatari katika mapinduzi yetu na ash-Sham yetu.

Enyi Watu Wakweli wa Ardhi ya Ash-Sham: Jambo hili ni zito sana, na ni lazima tuwe macho na waangalifu, na tusisaliti damu ya mashahidi wetu na mihanga ya watu wetu, ambao walijitolea tu kusimamisha utawala wa Uislamu juu ya magofu ya utawala uliokufa. Hebu na tuwe wastahiki wa damu iliyomwagika na mihanga iliyotolewa, kabla ya siku ambayo majuto hayatakuwa na faida.

Mwenyezi Mungu asema:

[وَلَا تَرْكَنُوا إِلَى الَّذِينَ ظَلَمُوا فَتَمَسَّكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللَّهِ مِنْ أَوْلِيَاءَ ثُمَّ لَا تُنصَرُونَ]

“Wala msiwategemee wanao dhulumu, usije ukakuguseni Moto. Wala nyinyi hamna walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, wala tena hamtasaidiwa.” [Hud 11:113]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Syria

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Syria
Address & Website
Tel: +8821644446132 Skype: TahrirSyria
www.tahrir-syria.info
E-Mail: media@tahrir-syria.info

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.