Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Syria

H.  18 Muharram 1447 Na: 01 / 1447 H
M.  Jumapili, 13 Julai 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ziara ya Azerbaijan: Hatua kuelekea Kusukuma Uhalalishaji Mahusiano na Umbile la Kiyahudi Ambayo Itakuwa ni Mchomo wa Kisu ndani ya Moyo wa Ummah

(Imetafsiriwa)

Chanzo cha kidiplomasia jijini Damascus kilisema mnamo Jumamosi kwamba mkutano wa moja kwa moja utafanyika kati ya afisa mmoja wa Syria na afisa mwengine wa 'Israel' huko Baku kando ya ziara ya Rais wa Syria Ahmad Al-Shara nchini Azerbaijan, kulingana na shirika la habari la Agence France-Presse (AFP).

Chanzo hicho ambacho kinafahamu mazungumzo hayo na ambacho hakikutajwa jina kilisema: “Kutakuwa na mkutano kati ya afisa wa Syria na afisa wa ‘Israel’ pembezoni mwa ziara ya Al-Shara mjini Baku,” kikibainisha kuwa Al-Shara hatashiriki ndani yake.

Alitaja kuwa mazungumzo hayo yatahusu "uwepo mpya wa kijeshi wa 'Israel' nchini Syria," akimaanisha maeneo ya kusini mwa Syria ambayo vikosi vya umbile la Kiyahudi vimepenya baada ya kuanguka kwa utawala wa Bashar al-Assad zaidi ya miezi saba iliyopita.

Huku Damascus ikiwa haijatangaza rasmi mazungumzo ya moja kwa moja, mamlaka za Syria zimekiri, tangu kuchukua mamlaka mwezi Disemba, kutokea kwa mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja na umbile la Kiyahudi, wakidai kuwa lengo lao ni kuzuia kuongezeka kwa uhasama, baada ya umbile la Kiyahudi kuanzisha mamia ya mashambulizi dhidi ya silaha za kijeshi za Syria.

Ishara nyingi na zinazoongezeka zinaonyesha hatua zinazochukuliwa kusukuma chaguo la kuhalalisha mahusiano kati ya utawala wa mpito na umbile la Kiyahudi. Kuna ajenda zilizofichika nyuma ya ziara hizo ambazo hukutana kwenye lengo kuu: kuhalalisha uwepo wa umbile la Kiyahudi linaloikalia kimabavu kama dola, pamoja na kutoa pigo kali kwa watu wetu katika Ardhi Iliyobarikiwa kwa jumla, na hasa mjini Gaza – wale ambao walitarajia kwamba watu wa Ash-Sham wangewanusuru baada ya Mwenyezi Mungu kuwatukuza kwa kuanguka kwa utawala wa Bashar.

Zaidi ya hayo yote ni kuhujumu ule uliobakia katika utashi wa Umma, ambao wakati fulani ulikuwa ukiyatazama mapinduzi hayo kwa heshima kubwa na kuvutiwa na kauli mbiu zake. Leo, unaona kwamba kile kinachotokea kiko mbali na matarajio, kauli mbiu, na msimamo wake.

Uhalalishaji mahusiano na umbile la Kiyahudi ni kuvunja utashi wa Ummah na mchomo hatari wa kisu ndani ya moyo wake.

Imedhihirika kwa kila mtu mwenye ufahamu na macho kwamba kuhalalisha mahusiano si "hitajio la kisiasa," wala "hatua ya busara," bali ni kuporomoka zaidi ya kuporomoka, na kuanguka kusiko kifani. Inaleta udhalilifu hapa duniani na hasara iliyo dhahiri kesho Akhera. Zaidi ya yote, ni kumsaliti Mwenyezi Mungu, Mtume wake, damu ya mashahidi, na kafara za wenye ikhlasi. Ni mgeuko kwa kanuni za Ummah na juhudi za kuufanya uwiane na Mkataba wa Abraham, kuugeuza mzozo na Mayahudi kutoka ule wa uwepo hadi ule wa mipaka na jiografia.

Hebu wale wanaotembea mteremko huu hatari na dimbwi la kina na watambue kwamba, katika kipindi chote cha miaka ya mapinduzi, wakati wakikabiliana na njama ya mauaji na uhalifu ambazo hazikuokoa binadamu wala mawe, umbile la Kiyahudi lilicheza dori muhimu kupitia usaidizi wa kiusalama na kijasusi kwa utawala uliokufa – hasa baada ya washirika wa utawala huo kufichua uhusiano uliowafungamanisha na Mayahudi.

Kwa hivyo, je, jibu kwa haya yote linapaswa kuwa maridhiano na uhalalishaji mahusiano, au tunapaswa kuharakisha kutii amri ya Mola wetu na kuwanusuru ndugu na dada zetu mjini Gaza?

Tunaonya juu ya hatari ya kile kinachotokea na tunatoa wito kwa watu wa mapinduzi huko Ash-Sham – wale ambao wametoa misafara ya mashahidi, wafungwa, na waliohamishwa, na ambao wameandika historia za ushujaa, subira, na kujitolea – wasikae kimya juu ya kuburutwa kwenye madimbwi ya kuhalalisha mahusiano, ambayo hata utawala mhalifu uliofurushwa haukusubutu kutangaza waziwazi kwa miongo mingi.

Uhalalishaji mahusiano ni uhaini. Ni mtego hatari na alama ya aibu kwenye paji la uso la wale wanaoufuata, kuuendeleza, au kukaa kimya kuuhusu. Kwa hiyo, watu wa mapinduzi ya Ash-Sham hasa, na wana wa Ummah kwa jumla, lazima waseme neno lao, watangaze kushikamana kwao na kanuni za Dini yao, ambayo inabainisha kwa uwazi kabisa jinsi mahusiano yanapaswa kuwa na wale wanaonyakua sehemu ya ardhi za Kiislamu na kuwachinja watu wake. Kila mtu lazima aseme na kwa uthabiti na kwa nguvu zote kukabiliana na miradi ya kufilisi (kadhia ya Palestina) na kuhalalisha mahusiano, kwa kuwa kukaa kimya dhidi ya hatari hii kubwa ni uhalifu mkubwa.

Tuna yakini kwamba mwisho wa umbile la Kiyahudi umekaribia, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu – na hilo halitatokea isipokuwa kwa mikono ya kiongozi mwenye ikhlasi wa Mwenyezi Mungu na askari wakweli wanaotafuta radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu na kusimamisha hukmu yake duniani. Hii itakuwa tu chini ya Rayah (bendera) ya Khilafah Rashida ya pili. Mpaka Mwenyezi Mungu atakaporuhusu jambo hili, jueni kwamba maisha yamejengwa kwa misimamo – na yeyote ambaye hatasimama leo dhidi ya kuhalalisha mahusiano, ataandikwa katika historia kuwa amekhini – khiyana ambayo muda hautaifuta.

[وَاللهُ غَالِبٌ عَلَى أَمْرِهِ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لا يَعْلَمُونَ]

“Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kushinda katika jambo lake, lakini watu wengi hawajui.” [Yusuf: 21]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Syria

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Syria
Address & Website
Tel: +8821644446132 Skype: TahrirSyria
www.tahrir-syria.info
E-Mail: media@tahrir-syria.info

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.