Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki

H.  19 Rabi' II 1443 Na: 1443 / 05
M.  Jumatano, 24 Novemba 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Chanzo cha Mgogoro ni Mfumo wa Kikafiri wa Kirasilimali, sio Muundo wa Mamlaka au Usimamizi
(Imetafsiriwa)

Ajenda ya Uturuki inatikiswa na kuporomoka kwa kiasi kikubwa kwa lira ya Uturuki dhidi ya dolari ya Amerika. Dolari ya Amerika, ambayo ilikuwa sawa na takriban lira 6 za Uturuki kipindi hiki mwaka jana, imevuka kiwango cha lira 13 za Uturuki. Kupanda kwa kiwango cha ubadilishaji kwa kawaida husababisha kupanda kwa bei za bidhaa zote zinazoagizwa kutoka nje na pembejeo za uzalishaji zinazotegemea fedha za kigeni, ambayo huathiri moja kwa moja uchumi halisi kutokana na kupungua kwa uwezo wa kununua. Maafisa wa serikali na wafuasi wao wako kwenye harakati za kujihami katika kukabiliana na hali inayozidi kuzorota, wakiwataka wananchi kuchukua hatua za kubana matumizi, wakihusisha uharibifu unaofanywa na mapambano dhidi ya ugaidi, na kuwalaumu wengine kila mara, haswa dola za nje. Kwa upande mwingine, upinzani unalaumu usimamizi mbovu wa serikali, ufisadi na mfumo wa urais.

Hata hivyo, katika hotuba moja maarufu, Erdogan anafafanua mgogoro huu wa kiuchumi na kifedha kama "vita vya uhuru wa kiuchumi", akipuuza ukweli kwamba tatizo linatokana na mfumo wa kikafiri wa kirasilimali. Na huku ukoloni wa kimataifa ukiufanya ulimwengu mzima kuwa watumwa kwa mfumo huu, ni vita gani vya uhuru vinavyozungumziwa wakati Uturuki ni sehemu ya mfumo huu?! Pamoja na kwamba Rais wa Jamhuri amekwama kwenye mkono wa vyombo vya fedha, riba, fedha za kigeni, mfumko wa bei, gharama za maisha na ukosefu wa ajira unaohusishwa na mfumo wa kirasilimali, na mazingira maovu, kamwe hatambui ufisadi wa mfumo mbovu wa kikoloni unaoingizwa nchini kutoka Magharibi.

Pia, Rais Erdogan, ambaye anarudia msemo wake wa "riba ndio sababu, mfumko wa bei ndio matokeo" na kauli mbiu zake maarufu kwamba Uturuki ni "taifa la kizalendo" na Uturuki ni "nguvu-kubwa", alienda mbali zaidi wakati huu akisema kuwa kuna andiko halali katika suala hili. Ni kana kwamba anakusudia Aya tukufu inayozungumzia kuhusu uharamu wa riba na kuwakisha vita dhidi ya Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake. Hata hivyo, hakuna andiko hilo pekee la kisheria kuhusu riba, bali kuna mamia ya maandiko ya kisheria na vilevile yanayoamuru kukomeshwa kwa mfumo mzima wa kikafiri wa kirasilimali na ubadilishaji dola itakayotabikisha hukmu za Kiislamu pamoja nayo.

 [إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الظَّالِمُونَ]

“…Hakika madhaalimu hawafanikiwi” [Al-An’am: 21].

Isipokuwa mfumo wa kirasilimali ung'olewe kutoka katika ardhi hizi na kusimamishwa Dola ya Khilafah Rashida, inayotabikisha mfumo pekee utokao kwa Mola wa walimwengu wote,  Waislamu hawataweza kuiondoa mifumo ya kikafiri. Kwa kuwa wokovu halisi ni kwa kuanza tena kwa maisha kamili ya Kiislamu. Migogoro haitakwisha maadamu madhalimu wanafumba macho yao na kuziba masikio yao wasisikie ukweli huu, na maadamu nyoyo zao ni nyeusi na akili zao zimekodishwa kwa mabwana zao, haitamalizika.

 [وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكاً وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَى]

“Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu.” [Taha: 124]

 Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Uturuki

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki
Address & Website
Tel: 

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.