Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Watawala Wameitelekeza Al-Aqsa, Hivyo na Tuwalinganie Moja kwa Moja Maafisa wa Jeshi la Pakistan Kuhamasika Kuikomboa

(Imetafsiriwa)

Mnamo tarehe 10 Mei 2021, siku tatu baada ya kuanza mashambulizi ya umbile la Kiyahudi kwenye Qibla cha mwanzo cha Waislamu, al-Masjid al-Aqsa, Imran Khan alifanya Umra na aliswali mbele ya Qibla cha pili na cha mwisho, al-Masjid al-Haram. Aliweza pia kuruhusiwa kuingia Kaa’ba Tukufu, huku vikosi vya Kiyahudi vikikiuka utukufu wa al-Aqsa na kisha kuendelea kuvurumisha mabomu juu ya vichwa vya Waislamu wa Ardhi Tukufu ya Palestina. Swali linakuja: Ikiwa Makafiri wataivamia Kaa’ba, Mwenyezi Mungu (swt) atunusuru, wakiwa na viatu vyao vichafu na bunduki zao na kuwauwa wanaoabudu, wakakiteka Qibla, je Imran Khan, Erdogan na wengineo watashikamana na maneno matupu yanayoitwa shutuma? Watautaka Umoja wa Mataifa kutatua suala hili? Watazitaka taasisi za haki za binaadamu kufanya chochote kuhusu hili?  

Jawabu ni ndio. Hawatofanya chochote kukinusuru Qibla cha mwisho, kwa sababu wamekipuuza Qibla cha mwanzo, kituo cha Isra’a cha Mtume (saw). Hawafanyi hivyo kwa sababu wanaabudu sanamu la sheria za kimataifa zilizoundwa na wakoloni. Sheria za kimataifa na mlinzi wake, Umoja wa Mataifa, haziruhusu kabisa nchi yoyote ya Waislamu kutumia jeshi lake kulinda maslahi ya Uislamu. Muda umefika kwa majeshi yetu kukiuka sheria za kimataifa huku yakisonga mbele kwa ajili ya kuikomboa Al-Aqsa na Palestina yote, ya kabla ya mwaka 1948.

Mola wetu (swt) anataka wale wanaodhulumiwa kulindwa kupitia nguvu za kijeshi. Mwenyezi Mungu (swt) anasema, 

[وَمَا لَكُمْ لَا تُقَٰتِلُونَ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ وَٱلْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ ٱلرِّجَالِ وَٱلنِّسَآءِ وَٱلْوِلْدَٰنِ ٱلَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَآ أَخْرِجْنَا مِنْ هَٰذِهِ ٱلْقَرْيَةِ ٱلظَّالِمِ أَهْلُهَا وَٱجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ وَلِيًّا وَٱجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ نَصِيرًا]

“Mna nini msipigane katika njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanaoonewa, wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anayetoka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anayetoka kwako.” [An-Nisa: 75]. Mola wetu (swt) anataka mapigano ili kuwafukuza walipotufukuza. Mwenyezi Mungu (swt) anasema,

[وَاقْتُلُوهُمْ حَيْثُ ثَقِفْتُمُوهُمْ وَأَخْرِجُوهُم مِّنْ حَيْثُ أَخْرَجُوكُمْ وَالْفِتْنَةُ أَشَدُّ مِنَ الْقَتْلِ]

“Na wauweni popote muwakutapo, na muwatoe popote walipokutoweni; kwani fitna ni mbaya zaidi kuliko kuuwa.” [Al Baqarah: 192].

Je, umbile la Kiyahudi halikuwatoa Waislamu kwa makundi majumbani mwao tokea miaka ya 1940? Hawaendelei kutanua makaazi yao kwenye ardhi za Waislamu? Hivyo kwa nini Imran Khan hachukui hatua anapotoa madai kwa dola ya Madinah na Khilafah Rashida? Kwa sababu ni mwenye heshima sana iliyofungamana na uoga kwa maadili na mila za Kimagharibi, anayevutiwa mno na Umoja wa Mataifa na Sheria ya Kimataifa. Sheria hii fisidifu ya kikoloni ni muhimu zaidi kwa watawala hawa wasaliti kuliko Hukmu ya Mwenyezi Mungu (swt). Hivyo suala liko wazi. Makhaini hawa wamechagua sheria ya mwanaadamu dhidi ya Sheria ya Mwenyezi Mungu (swt) Muumba wa ulimwengu wote. Hakuna matumaini kwao na hivyo ni wakati sasa kwa Waislamu kuwageukia simba katika vikosi vyao vya jeshi.

Enyi Waislamu! Njia pekee ya kukilinda Qibla cha kwanza, ardhi ya Palestina na Ummah ni kusikiliza wito wa Mwenyezi Mungu (swt) na kupeleka majeshi kuikomboa kila shubiri moja ya ardhi ya Palestina, ya kabla ya mwaka 1967 na 1948. Makafiri huvunja sheria zao wenyewe na mikataba ya haki za binaadamu ili kufikia maslahi yao, kama ilivyofanya Dola ya Kibaniani katika Kashmir, kama ilivyofanya Amerika nchini Iraq na kama ilivyofanya dola ya Kiyahudi kwa kuivamia Al-Aqsa. Ikiwa Jeshi la Pakistan linaweza kupelekwa hadi Sierra Leone na Somalia, basi kwa nini haliwezi kupelekwa kuikomboa Al-Aqsa?

Enyi Waislamu! Msinyamazishwe na ukandamizaji wa watawala waovu. Jengeni ushujaa kutoka kwa Ulamaa na wanasiasa wa Kiislamu wanaonyanyua sauti zao kwa nguvu na kwa uwazi kwa ajili ya kuyahamasisha majeshi yetu, umoja wa Ummah, Khilafah na Jihad. Wachukueni kuwa ni viongozi wenu na muwasaidie kwa namna zote. Msipuuze jukumu lenu katika suala hili kwa kuwa halina mjadala na ni suala la kufa na kupona. Kwa kweli, Al-Aqsa ikiwa ni kituo cha Israa ni sehemu ya Aqida yetu. Jukumu letu ni kusimama kwa ajili ya Haqi, kuamrisha mema na kuwataka vijana wetu mashujaa katika vikosi vya majeshi ya Waislamu kujibu wito wa Ummah. Ni wazi kuwa watawala wa Waislamu hawatojibu, na hivyo ni jukumu la maafisa wa majeshi ya Waislamu kuwang'oa hao na kuwahamasika katika muda tunaowahitaji. Mwenyezi Mungu (swt) anasema,

     [يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِن تَنصُرُواْ ٱللَّهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ]

”Enyi mlioamini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.”  [Surah Muhammad 47: 7]

 #الأقصى_يستصرخ_الجيوش

#Aqsa_calls_armies

#AqsaCallsArmies

#AqsaYawaitaMajeshi

 Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Maryam Ansari

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.