Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mzunguko wa Migogoro ni Lazima Ukome kwa Umma

(Imetafsiriwa)

Ummah umekuwa katika mzunguko wa migogoro kwa miaka 105. Mzunguko wa migogoro ambao umeathiri Ummah ni ule ambao umekuwa wa kimakusudi na wenye shabaha katika kusababisha aina mbalimbali za ukandamizaji na mateso kwa watu na mazingira. Leo, tunashuhudia mauaji kadhaa ya halaiki: Gaza na Palestina, Kashmir, Turkistan Mashariki, Sudan, na vitendo vya vurugu vya kudumu nchini Nigeria, Ethiopia, Syria, Lebanon, Congo, na Venezuela. Orodha hii inaweza kuendelea kwa sababu kila siku mji au nchi mpya inasogezwa karibu na janga kubwa na Magharibi ya kikoloni, yaani Amerika, ambayo hupora na kuyumbisha nchi baada ya nchi ili kuhakikisha kwamba udhibiti wake unabaki imara.

Tunapoangalia kinachoendelea hivi sasa katika ardhi za Waislamu, hatuwezi kufikiria jinsi kinavyoweza kuwa kibaya zaidi. Hata hivyo, mjini Gaza pekee, katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, Ripota wa Umoja wa Mataifa Francesca Albanese hivi karibuni alisema kwamba takriban idadi ya vifo ina uwezekano kuwa 680,000 ikilinganishwa na idadi iliyotolewa rasmi ya 70,000. Vita nchini Syria vilifanya angalau watoto milioni 1.2 kuwa yatima. Viwango vikubwa vya njaa vinatokea Gaza, Sudan, na Yemen kwa sasa. Dada zetu kote nchini Sudan, Palestina, Kashmir, Turkestan Mashariki, Myanmar, India, na kwengineko wanaogopa kushambuliwa kingono au kubakwa. Siku chache tu zilizopita, mwanamke mmoja wa Kiislamu huko Mumbai alitishiwa na mtu mwenye msimamo mkali wa Hindutva ambaye, akiwa amesimama kando ya mkewe, alisema, “wewe ni mwanamke wa Kiislamu, sivyo? Toka nje, nitawaita wanaume na niwafanye wakubake” kutokana na ugomvi katika duka moja la mboga lililojaa watu! Hili ni tukio la kila siku nchini India. Kulingana na UNICEF, watoto 3 kati ya 5 walio chini ya umri wa miaka 5 katika eneo la MENA (Mashariki ya Kati Kaskazini mwa Afrika) wanakabiliwa na umaskini wa chakula. Kuongezeka kwa chuki dhidi ya Uislamu katika mataifa ya Magharibi pia ni jambo la kutisha. Waislamu nchini Amerika, Canada, Uingereza, Ulaya, na Australia wanakabiliwa na sheria zinazopiga marufuku hijab, matusi ya maneno, ugomvi wa kimwili, na uharibifu wa misikiti na vituo vya Kiislamu. Wanasiasa katika mataifa hayo wameridhia sana kuwafanya Waislamu na Uislamu kuwa chanzo cha vita visivyokwisha (yaani ugaidi) na usalama wa kiuchumi uliofeli katika nchi zao wenyewe na kusababisha ongezeko kubwa la matukio ya chuki dhidi ya Uislamu. Ili kuongeza mafuta kwenye moto huu uliotengenezwa na mwanadamu, tuna watawala katika nchi zetu ambao si wenzetu. Ni wanaume na wanawake wanaopendelea maisha ya dunia hii na kupinga ahkam za Mwenyezi Mungu (swt). Wamepandikizwa kufanya kazi ya Wamagharibi waovu ili kudumisha utawala wao na kujaza mifuko ya kipote cha mabepari. Baya zaidi, ni kwamba idadi hii na uhalifu huu ni ncha tu ya mlima wa barafu. Maumivu na mateso ambayo yamesababishwa kwa umma, haswa tangu 28 Rajab 1342 H, ni kwa sababu tulipoteza ngao yetu na Imam wetu, nguvu iliyounganisha ummah pamoja na kutetea heshima yetu na kulinda usalama wetu.

Ni vibaya na jambo la kutisha tunapoangalia idadi hii na jinsi mateso yalivyo makubwa. Inaonekana kukaribia kuwa vigumu kupata njia ya kutokea, kutokana na wavamizi kutoka nje na walaji njama kutoka ndani waliojenga kuta kati yetu na kuziita mipaka. Waliambukiza akili zetu na utaifa ili kuvunja mafungamano yetu. Tulianza kuweka juhudi zetu katika mifumo iliyoundwa na Karl Marx - baba wa Ukomunisti - au Adam Smith - baba wa Ubepari - na matumaini yetu kwa viongozi kama Joe Biden, au hata kwa wale Waislamu ambao wanakuwa maafisa wa kuchaguliwa katika mifumo hii ya ukafiri. Badala yake, tunapaswa kukaa chini na kutafakari historia yetu tukufu na kujithibitishia wenyewe jinsi Uislamu ulivyokuja na sio tu kuwaunganisha Waislamu, bali pia kufuta ubaguzi wa rangi, ukabila, na chuki dhidi ya wanawake kutokana na kuota mizizi kimfumo katika jamii kama ilivyo chini ya mifumo iliyotengenezwa na mwanadamu.

Ilikuwa ni dola ya Khilafah ambayo ilitoa amani na usalama kwa Waislamu, ikiwaruhusu kuishi kwa amani pamoja kama dola moja, bila kujali lugha au rangi yao. Uislamu ulitufanya ndugu na dada - Waarabu, waajemi, weusi, au weupe - na kutuamuru kuishi pamoja kwa huruma na upole. Mtume Muhammed (saw) alisema, «المُسْلِمُ أَخُو المُسْلِمِ لَا يَظْلِمُهُ وَلَا يُسَلِّمُه»ُ “Muislamu ni ndugu ya Muislamu, hamdhulumu wala hamkabidhi kwa wengine” (Bukhari na Muslim). Khilafah iliwapa hifadhi wale walioteswa, kama vile Mayahudi walipokimbia Uhispania baada ya Ukombozi kwenye kivuli cha Dola ya Kiislamu. Khilafah ilikuwa dola inayoongoza duniani kwa zaidi ya miaka elfu moja katika sayansi na teknolojia. Majeshi yake yaliwalinda Waislamu waliposhambuliwa na kufungua ardhi mpya kwa ajili ya Dini ya Uislamu, tofauti na leo ambapo watawala wanyonge waliopandikizwa wa ardhi za Waislamu hukaza kamba kali kwa vikosi vya kijeshi, hivyo wanapuuza mauaji mengi ya halaiki, vilio vya watoto wetu wenye njaa, na maombi ya dada zetu ambao wanakiukwa mara kwa mara. Funga macho yako kwa muda ili kufikiria jinsi hali ya Waislamu ingekuwa ikiwa Khilafah ingeibuka tena katika miaka hii miwili iliyopita. Mipaka ya kikoloni ingeyeyuka – kama vile pia hisia yoyote ya utaifa iliyopo – na kutuunganisha bila pasipoti na visa. Khalifa, ambaye angetawala ardhi kubwa za Uislamu, angeongoza vikosi vyetu vyenye nguvu vya mamilioni kuwafukuza wavamizi wa Magharibi ili kuikomboa Palestina, Kashmir, na kwengineko. Rasilimali zilizoibiwa za ardhi zetu tajiri zingerudi mikononi mwa Waislamu ili zitumike kuhakikisha kwamba raia wetu hawatakuwa na njaa na kuishi kwa heshima. Watoto wetu wangekuwa shuleni, wakijifunza kuhusu Dini yao na kuwa maulamaa na wasomi ambao wangeongoza ulimwengu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt). Hili litakuwa tu baada ya kusimamishwa tena kwa mfumo wa Mwenyezi Mungu (swt) ambapo tutaona mzunguko wa mgogoro ukimalizika.

Ingawa leo inaweza kuonekana kama ndoto ya mbali, ni lazima tukumbuke kwamba hakuna kisichowezekana kwa Waislamu wanaoweka imani thabiti na kumtegemea Mwenyezi Mungu (swt). Mwenyezi Mungu (swt) alimfungulia milango Mtume wetu mpendwa (saw) ili kuweka misingi ya dola ya Khilafah mjini Madina, kwa Makhalifa wanne waongofu waliofungua ardhi dhidi ya himaya kubwa za wakati wao – Wafursi na Warumi – na Makhalifa waliofuata kwa miaka 1000 iliyofuata, ingawa sio kila wakati ni wakamilifu, lakini kwamba Mwenyezi Mungu (swt) aliimarisha Njia Yake ili kuleta Uislamu kote ulimwenguni na kuunusuru mfumo wa Uislamu.

[وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَىٰ لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُمْ مِنْ بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا]

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao.” [Surah An-Nur:55]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Sarah Mohammed – Amerika

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.