Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Sudan: Mfano Mwengine wa Utaifa Uliofeli

(Imetafsiriwa)

Kulingana na sheria zinazoongoza mfumo wa sasa, kila taifa lina haki ya kuchagua sheria zinazoliongoza – na hivyo, kila taifa lina haki ya kuwa na serikali. Wazo hili lilisababisha wimbi la nchi mpya baada ya Vita vya pili vya Dunia, huku zilizopo zikigawanyika na kwa hivyo, tunayo vurugu tunaloliona leo.

Tangu 1945 kumekuwa na angalau nchi mpya 34 ambazo zimetambuliwa na Umoja wa Mataifa. Hili lilitokana na wimbi la utaifa ambalo lilienea kote ulimwenguni kwa miongo kadhaa tangu katikati ya miaka ya 1900. Mipaka ya kindoto ilichorwa ili kutoa uhuru kwa makundi mbalimbali na haki ya kutawala, kwani nchi kama vile Sudan iliyoungana hapo awali zilitumbukia ndani ya mizozo na machafuko.

Lakini migawanyiko mpya haikutatua matatizo yaliyopo – iliyafanya kuwa magumu zaidi. Katika kesi ya Sudan, njia moja ya kuelewa tatizo hili ni kuangalia viwanda vyao na sekta ya mafuta. Ilikuwa katikati ya nchi iliyoungana na ikawa uti wa mgongo wa uchumi mpya. Tatizo lilikuwa kwamba mipaka ilisambaratisha sekta ya mafuta ya Sudan iliyokuwa kuu hapo awali.

Katika dola mapya zilizoundwa, Kusini ilishikilia maeneo mengi ya mafuta lakini Kaskazini ilishikilia miundombinu ya usafirishaji, ikiwemo mabomba na mitambo ya kusafisha mafuta. Kwa hivyo, Sudan Kusini isiyo na bahari ilitegemea mabomba ya Sudan hadi Bahari Nyekundu. Mgawanyiko huu ulisababisha mizozo juu ya ada za usafirishaji, ambayo mara kwa mara imetatiza usafirishaji wa mafuta – mauzo ya nje ambayo nchi zote mbili bado zinategemea kwa uchumi wao. Kwa mfano, mwaka wa 2012, Sudan Kusini ilisitisha uzalishaji wa mafuta kutokana na kutoelewana huku, hatua ambayo iliathiri kwa kiasi kikubwa mapato ya nchi zote mbili. Huku makubaliano yakifanywa kuregesha mauzo ya nje, mivutano na matatizo ya kiuchumi yangaliko.

Kwa hiyo, tangu 2011, tulichokuwa nacho ni nchi mbili tofauti ambazo zinategemeana kwa kiasi kikubwa. Zina rasilimali, lakini hazina maendeleo zinazohitaji kuyatumia. Na hivyo, licha ya kuwa takriban mapipa bilioni 8 ya mafuta kati yao, wanateseka na umaskini uliokithiri.

Hili lingeweza kubadilika – ikiwa nchi hizi zingekuwa zimeungana, na kuwa na utulivu. Hili halitafanyika chini ya mfumo wa sasa wa Ubepari – mfumo huu umezidisha mizozo kati ya watu, na kisha kuwapa mfumo wa utawala unaoshajiisha mawazo kama vile ‘mwenye nguvu mpishe’, ambayo yamechochea uhasama ndani na baina ya nchi hizo.

Ili kubadilisha hali ya Sudan, na kuhakikisha kuwa nchi hiyo inapata utulivu wa kisiasa na kuweza kujiendeleza kiuchumi, inahitaji kuregeshwa chini ya bendera ya Uislamu. Kisha sekta yake ya mafuta inaweza kutumika ipasavyo, sekta yake ya kilimo inaweza kuendelezwa, sekta yake ya madini na viwanda inaweza kupanuka, na miundombinu yake ya biashara inaweza kuimarishwa.

Hili litafanywa chini ya muongozo wa Khalifa na idara wake – ambaye anafahamu wajibu wao wa kuhakikisha kwamba maeneo ndani ya Dola ya Kiislamu yanaendelezwa, na rasilimali zinatumika, kwa manufaa ya Umma wa Kiislamu. Watakuwa na dhambi kwa kupuuza jukumu hili.

Inawezekana kuendeleza eneo la Sudan. Ina uwezo wa kuwa mzalishaji mkuu wa chakula na msafirishaji nje ya nchi na ardhi yake kubwa inayoweza kulima—karibu hekta milioni 84, ingawa chini ya 20% inalimwa. Ina mazao muhimu, ambayo ni pamoja na pamba, njugu, ufuta, mtama, ngano na miwa. Pia ina rasilimali nyingi za madini kama vile dhahabu, asbesto, chromium, mica, kaolini, na shaba. Na ina miundombinu ya viwanda kadhaa vyepesi kama vile usindikaji wa kilimo, uunganishaji wa vifaa vya kielektroniki, plastiki, utengenezaji wa samani na utengenezaji wa nguo.

Ina uwezo wa kusambaza rasilimali kwa nchi zengine za Kiislamu, huku ikinufaika na kile wanachotoa. Kwa kuwa iko kimkakati kati ya Dola za Ghuba na Afrika Magharibi, na ina njia ya ufikiaji wa Bahari Nyekundu.

Bandari kuu baharini ya Sudan ni Port Sudan, bandari ya asili ya kina kirefu yenye uwezo wa kuhudumia meli kubwa. Pia inahimili mizigo mbalimbali ikiwemo makontena, bidhaa kubwa, na mafuta. Hii, pamoja na bandari zengine za Sudan, huipa nchi hiyo kiunganishi cha moja kwa moja kwa njia za kimataifa za meli kupitia Bahari Nyekundu. Hii haiunganishi tu Sudan na majirani zake wa Kiafrika lakini pia na masoko ya Mashariki ya Kati ikiwemo mji wa bandari wa Saudi Arabia wa Jeddah. Hii ni muhimu kwani majirani zake hawana bahari na wangehitaji ufikiaji wa Sudan kwenye bahari ili kufanya biashara na ardhi zengine za Waislamu. Ardhi ambazo hazikufungika tu kwa Afrika na Mashariki ya Kati lakini pia, ikiwezekana, zile za Asia, Ulaya na Ghuba ya Uajemi na pia kupitia eneo la kimkakati la Sudan kwenye Bahari Nyekundu na ukaribu na njia ya meli ya Mkondo wa Suez.

Licha ya msukosuko wa sasa, miundombinu inafanya kazi – ambapo Sudan kwa sasa inasafirisha mafuta yake ghafi kwa UAE na Malaysia kupitia Kituo cha Bahari cha Bashayer na Kituo cha Bahari cha PLOC. Mauzo haya yanatumwa kupitia miundombinu ya bandari ya Bahari Nyekundu ya Sudan na kwa kiasi kikubwa inajumuisha mafuta ghafi yanayozalishwa nchini Sudan Kusini.

Kwa hivyo, uwezekano upo kwa eneo hilo kuwa sehemu inayostawi ya Dola ya Kiislamu. Baada ya ardhi ya Waislamu kuunganishwa tena, Sudan itaweza kufanya biashara na Ummah wote wa Kiislamu. Hii ni muhimu kwa sababu Sudan sio nchi pekee iliyobarikiwa kuwa na maliasili ambayo inatosha kukidhi mahitaji mengi ya kimataifa leo – Afrika nzima imebarikiwa na rasilimali hizo; bara hilo lina takriban 30% ya hifadhi ya madini duniani ikiwa ni pamoja na cobalt, dhahabu, platinam na shaba. Pia ina takriban 8% ya hifadhi ya mafuta duniani na karibu 12% ya hifadhi ya gesi asilia duniani.

Ikiwa tutaangalia majirani wa Sudan, tunayo Misri, ambayo ina utajiri wa gesi asilia na mafuta. Pia ina njia ya ufikiaji Mto Nile, ambao ni rasilimali muhimu ya maji. Kuna Eritrea yenye rasilimali muhimu za madini ikiwa ni pamoja na dhahabu, shaba, na potashi, na Ethiopia yenye uwezo wake wa kufua umeme, ardhi ya kilimo na madini. Kisha kuna Jamhuri ya Afrika ya Kati yenye almasi, dhahabu, na urani, na Chad pamoja na Libya na rasilimali zao kubwa za mafuta.

Licha ya utajiri na uwezo huu wote, Afrika ni nyumbani kwa baadhi ya mataifa maskini zaidi duniani. Pamoja na Sudan na Sudan Kusini, dola zengine zimejaa mizozo na vifo. Rasilimali zao zinaibiwa na kunyonywa.

Chini ya Dola ya Khilafah, hii itabadilika. Dola ya Kiislamu itaanza tena wajibu wake wa kuendeleza rasilimali za ardhi, ili sisi (kama Ummah) tujitosheleze na tusitegemee au kunyonywa na dola adui. Hili ni muhimu, kwani hairuhusiwi kuwapa maadui wa Uislamu faida yoyote juu yetu. Na kama tunavyoona, inawezekana pia, iwapo tutakuwa na kiongozi wa kuwaunganisha Waislamu nchini Sudan na kuzima hali ya sintofahamu na misukosuko iliyopo sasa.

أزمة_السودان#                       #SudanCrisis

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Fatima Musab
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.