Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kuunganisha Fikra na Wabebaji Wake Ndio Njia ya Mabadiliko ya Kweli
(Imetafsiriwa)

Ni wazi, kwa wale wanaofanya kazi kwa ikhlasi kwa ajili ya kuhuisha Umma wa Kiislamu kupitia Uislamu, kile ambacho hali ya Ummah imefikia, kushambuliwa na mataifa mengine kama mwindaji anapolenga kwenye mawindo yake. Vile vile, ni dhahiri kwa wachunguzi jinsi Ummah unavyoelewa kwa uwazi uhalisia wake na kutambua sababu za mateso na maumivu yake. Kinachojulikana kwa Ummah kwa kiasi kikubwa kimefungika kwa makafiri wakoloni, watawala vibaraka, na tawala zilizowekwa na dola hizi za kikoloni juu ya shingo za Ummah ili kuukandamiza, kupora rasilimali zake, na kuuzuia kujikomboa kutoka kwa mshiko wa wakoloni kwa kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume.

Matokeo yake, “wahubiri” na “washawishi” wengi wamejitokeza ndani ya Ummah kwenye mitandao ya kijamii, wakizungumza na watu kuhusu vyanzo vya masaibu na mateso. Wamepata wafuasi wengi, kwa sababu wanazungumzia machungu ya watu, wakitoa namna ya faraja na subira mbele ya dhiki zilizoupata Ummah. Hata hivyo, hawajawasilisha kwa watu suluhisho sahihi ambalo kweli lingewakomboa kutoka katika masaibu yao: yaani, kusimamisha Khilafah kama njia badali ya kihadhara, kisiasa, na kijamii ambayo itarudisha hadhi yao.

Mapungufu ya wahubiri hawa na waathiriwa yapo katika kushindwa kwao kuunganisha utambuzi wao, na utambuzi wa Ummah, juu ya uhalisia wake na mzizi wa mateso yake, unaowakilishwa na watawala na tawala, pamoja na suluhisho ambalo Umma unapaswa kujitahidi kulifikia. Pia wameshindwa kufafanua kwamba kubadili hali ya sasa na kuwa bora ni jukumu la Ummah peke yake, na kwamba halitatokea lenyewe, wala haliwezi kukabidhiwa kwa wengine, hata kwa pote la Ummah, maadamu hakuna juhudi za kutosha za wale ambao wameinuka kufikia mabadiliko haya.

Kufeli kukubwa kwa wahubiri hawa ni kwamba, pamoja na kujua kwamba Uislamu wa kisiasa, unaowakilishwa kwa kufanya kazi ya kusimamisha Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume, ni kitendo kinachowaondolea wao na Waislamu wote faradhi ya Shariah ya kutekeleza Sharia ya Mwenyezi Mungu duniani, hawajasisitiza kwamba kazi hii pekee inatosha kuleta mabadiliko kwa Ummah na kuleta mabadiliko yanayotamaniwa. Wakijua kwamba kundi pekee linalofanya kazi kuelekea lengo hili ni Hizb ut Tahrir, hawajashirikiana nalo, ingawa kufanya hivyo ni wajibu kwao zaidi kuliko kwa watu wa kawaida. Badala yake, walipendelea kufanya kazi kibinafsi, mbali na lengo na mradi huu, tofauti na kundi ambalo ni la kuibuka washindi, inshaaAllah. Wengi wao hata walichagua kutoitaja Hizb kama kiongozi wa kazi hii, achilia mbali kuwaalika watu kujiunga nayo, licha ya ukweli kwamba inawakilisha mashua yao ya kuokoa maisha. Hii ni kwa sababu walitamani kuendelea kufanya kazi ndani ya “mipaka iliyoruhusiwa” iliyoanzishwa na tawala ambazo zina ndoto ya ukombozi, wakichagua usalama wa kibinafsi badala ya uadilifu na utawala wa mfumo na utabikishaji wake.

Ufahamu wa uhalisia wa Ummah na mashaka yake unahitaji njia moja tu ya utekelezaji ili kuleta mfumo huo madarakani: kuunganisha suluhisho kwa wabebaji wake. Kinachokosekana Ummah hivi sasa ni kufanya kazi na Hizb ut Tahrir, kuizunguka, na kuikabidhi uongozi mpaka Hizb na Ummah viwe kitu kimoja na chombo kimoja. Kwa hiyo, juhudi za wahubiri, na wale wanaofanya matendo mema ndani ya Hizb ut Tahrir, lazima zilenge katika kuunganisha kwa ukaribu suluhisho na Hizb, ili Hizb, kupitia mwili wake na dhati yake, iweze kuuongoza Ummah katika mchakato wa mabadiliko, na kukamilisha hatua ya mwisho: kupindua tawala na kusimamisha Khilafah Rashida ya Pili kwa njia ya Utume.

Maana na umuhimu wa kuunganisha suluhisho kwa hizb na wahusika wake wa kisiasa unaweza kufupishwa kama ifuatavyo:

1. Kuangazia kipengee cha kivitendo cha suluhisho na kukiunganisha na wabebaji wake: Hizb inaamini kwamba fikra huwa hai na yenye nguvu pale tu inaponasibishwa na watu wakubwa wa kisiasa au mavuguvugu yanayoibeba na kujitolea mhanga kwa ajili yake. Fikra ya mabadiliko inapohusishwa na wanaume wanaojulikana kwa uadilifu wao, ujasiri, na unyoofu, huwa yenye kulazimisha na kuvutia zaidi, badala ya kubaki kuwa nadharia dhahania katika vitabu au katika akili za watu. Huu ulikuwa ni mwelekeo wa Mtume Muhammad (saw) ambaye alijidhihirisha waziwazi na kutetea fikra yake hadharani, bila kufichika, na akaendeleza njia yake ya wazi na ya moja kwa moja hata baada ya Maquraishi kumkataa na kumtesa yeye na Maswahaba zake (ra).

2. Kubadilisha fikra kutoka katika Dawah hadi katika utekelezaji wa kivitendo: Hizb inaona fikra ya kutawala kwa Uislamu si mada ya hotuba au mitandao ya kijamii pekee, bali ni mradi wa kutekeleza mashinani. Kwa hivyo, fikra lazima iunganishwe na uongozi halisi wa kisiasa, kama vile Hizb, ambayo inafanya kazi ya kuigeuza kuwa uhalisia wa kisiasa unaoonekana, na wanaume na wanawake (mashababu) wanaojulikana kwa uhusiano wao. Hizb na wabebaji wake hawasiti kutaka uongozi wa Ummah na utawala kwa jina lake, kwa kufuata mfano wa Mtume Muhammad (saw), ambaye hakukubali kushiriki uongozi na Maquraishi.

3. Kulinda fikra dhidi ya upotoshaji na chaguo-shirikishi: Iwapo fikra itasalia kuwa dhahania au mbebaji wake hajulikani, serikali au wapinzani wanaweza kuitabanni kijuujuu, na kisha kuiondoa katika maudhui yake. Kitu mithili ya hicho kilitokea kwa lile linaloitwa tangazo la Khilafah la ISIS. Hata hivyo, fikra hiyo inapounganishwa na wabebaji da’wah wake wa asili, hudhihirika kwa watu wanaoiwakilisha na wanaotaka kuiondoa katika dhati yake, hivyo uaminifu kwa fikra hiyo hubakia kufungika na wabebaji wake wenye ikhlasi.

4. Kuunda rai jumla ya umma (ar-rai al-aam) kwa msingi wa ufahamu jumla (al-waie al-aam): Rai jumla ya umma juu ya msingi wa ufahamu hujitokeza pale tu fikra inapounganishwa na wale wanaoibeba na kuiwakilisha kisiasa. Watu hawahamasiki nyuma ya fikra katika ombwe. Wanakusanyika pambizoni mwa wanaume au maumbo ya kisiasa ambayo yanajumuisha na kutetea fikra hizi.

5. Kutofautisha wabebaji Da’wah wa kimfumo kutoka kwa wapatilizaji fursa: Uhusiano huu unafichua wale wanaojaribu kudandia wimbi la mabadiliko kwa manufaa ya kibinafsi, au kutumikia ajenda za tawala nyengine. Ni lazima watu waone waziwazi kwamba fikra hii inahusishwa na Hizb na wanachama wake, hivyo wasidanganywe na badali ghushi.

Kazi ya mtu binafsi, au kazi isiyofungamana na wabebaji wanaojitahidi kwa ajili ya Khilafah na Hizb inayowaunganisha, inaruhusiwa kisheria, kwani tawala zinatambua juhudi hizo hazina tishio lolote kwao. Haijalishi juhudi hizi ni kubwa au nyingi kiasi gani, hazitafikia lengo kuu la mabadiliko. Hata wafuasi wengi wa wale wanaozungumza na watu kuhusu mateso yao hawataleta ulinganizi huo madarakani. Ikiwa wahubiri watazingatia kusherehekea idadi kubwa ya wafuasi, wafuasi hawa watatawanyika haraka wanapoombwa kujihusisha na kazi ya kisiasa na kisheria inayohitajika kuleta wito huo mamlakani. Shauku yao inafifia wanapokabiliwa na jukumu na hatua ya kweli, kama Mwenyezi Mungu (swt) anavyosema:

[يَحْسَبُهُ الظَّمْآنُ مَاءً حَتَّى إِذَا جَاءَهُ لَمْ يَجِدْهُ شَيْئًا]

“Mwenye kiu huyadhania ni maji. Hata akiyaendea hapati chochote.” [Surah Al-Nur: 39].

Kwa hivyo, Hizb inaamini kwamba kuunganisha fikra yake nayo na wabebaji Da’wah wake wa kweli kunaifanya kuwa na ushawishi, vitendo, kulindwa dhidi ya kupotoshwa, na kuunganishwa na uongozi wa kisiasa wenye utambuzi. Hii ndiyo njia ya kutambua jambo hilo uwanjani, tofauti na fikra zilizoachwa zikielea au kutekwa nyara na nguvu za uadui, ujinga, au upotofu. Kwa hivyo, kazi yote inayofanywa na wenye ikhlasi, ikiwemo wabebaji Da’wah, lazima iwe na asili na chanzo kilicho wazi, kwa mujibu wa Maneno ya Mwenyezi Mungu,

[قُلْ هَذِهِ سَبِيلِي أَدْعُو إِلَى اللَّهِ عَلَى بَصِيرَةٍ أَنَا وَمَنِ اتَّبَعَنِي وَسُبْحَانَ اللَّهِ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُشْرِكِينَ]

“Sema: Hii ndiyo Njia yangu - ninalingania kwa Mwenyezi Mungu kwa kujua - mimi na wanao nifuata. Na ametakasika Mwenyezi Mungu! Wala mimi si katika washirikina.’” [Surah Yusuf 108].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Bilal Al-Muhajir – Wilayah Pakistan

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.