Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan:

Amali na Shughuli wakati wa Kipindi cha Mwezi wa Agosti 2026 M

Ikiendelea kuunywesha Umma kwa fikra na hukmu za Uislamu kuhusu maisha, Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan ilifanya amali nyingiza kithaqafa wakati wa mwezi wa Agosti 2026. Ilituma ujumbe kwa watu mashuhuri, viongozi wa kikabila, na viongozi wa jamii, na kutoa hotuba za kisiasa katika maeneo ya umma, misikitini na masokoni. Ilizungumza katika majukwaa kuhusu masuala ambayo watu wanakabiliwa nayo, na kufungua kikao chake cha kisiasa kwa wanafikra, wanahabari, na wanamaoni. Msemaji wake rasmi katika Wilayah ya Sudan, Ustadh Ibrahim Othman (Abu Khalil), alishughulikia matatizo yanayowakabili watu wa Sudan katika taarifa zake na mkutano wake na waandishi wa habari. Shughuli hizi, kwa jumla, zilikuwa amali njema, na ni kama ifuatavyo:

Kwanza: Wajumbe

Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan, chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Ustadh Nasser Ridha, ilifanya ziara kadhaa zikiwalenga baadhi ya viongozi wa makabila, ambao ni: (Nazir Ali Ibrahim Daqlal, Nazir wa kabila la Bani Amer, nyumbani kwake katika mji wa Kassala; Nazir wa Halanga, Mhandisi Alis Abdul Qadir nyumbani kwake, Shakilai Abdul Qadir naibu, Abdul Qadir Sayed Ahmed, Sheikh Hassan Ismail, na wengineo wa Al-Musallamiya, Sheikh Muhammad Mustafa Abdul Karim Mubarak, nyumbani kwake katika kijiji cha Ad Al-Tina, vijijini Al-Qadharif (moja ya matawi ya kabila la Bani Amer), Sheikh Hasab Allah Al-Tahir, katibu wa chama cha Muhammad Al-Tahir, Al-Qadarif; mji wa Nazir wa kabila la Habab, Sheikh Muhammad Ali Muhammad Saeed, nyumbani kwake katika mji wa Al-Qadharif; Msikiti wa Sufi huko Al-Qadharif, ambapo ujumbe huo ulikutana na Masheikh Othman Abdul Rahman Al-Azraq, Hamad Abdul Rahman Al-Azraq, na Ahmed Othman Abdul Rahman Al-Azraq; Nazir Awad Al-Karim Mahmoud Zayed (Wad Zayed); Msimamizi Mkuu wa kabila la Dabaina, na Makamu wa Rais wa Utawala wa Wenyeji nchini Sudan, afisini kwake katika soko la Qadharif - Ustadh Mujahid Muhammad Haroun, Mwenyekiti wa Baraza la Shura la kabila la Hausa nchini Sudan, na Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo na Mageuzi ya Utawala katika Jimbo la Bahari Nyekundu, afisini kwake Port Sudan.

Katika mikutano yake yote na wajumbe, Ustadh Nasser aliangazia hali ya kisiasa na kijeshi nchini Sudan na hatari ya kuanguka katika mtego uliowekwa na mkoloni kafiri, anayetaka kuichana nchi kupitia uhamasishaji wa kikabila na ubaguzi wa rangi. Alizungumzia matukio ya sasa, akibainisha kuwa kila kabila sasa linawaita vijana wake na kuunda harakati zake zenye silaha. Alidai kwamba huu ndio mradi wa mkoloni hasa wa kupanda ugomvi miongoni mwa watu na kuigawanya nchi, na kuipunguza hadi kuwa dola dhaifu na iliyogawanyika. Alifichua mipango ya Amerika ya kutenganisha Darfur na kuigawanya Sudan, akiuchukulia kama mpango wa zamani unaotekelezwa sasa na Amerika na watawala wake vibaraka. Alisisitiza kwamba jambo baya zaidi la hili ni utumiaji wao mbaya wa makabila fulani, wakiwapa silaha za kutumika kama farasi wa Trojan katika kugawanyika kwa Sudan. Ustadh Nasser aliwakumbusha viongozi hawa kuhusu misimamo iliyochukuliwa na viongozi wa makabila ambao Mwenyezi Mungu aliwasifu kwa kuunusuru Uislamu na kuanzishwa kwa jengo lake kubwa: dola ya Mtume Muhammad (saw). Alisisitiza kwamba ni wajibu wa viongozi wa makabila leo kuunusuru Uislamu ili waweze kuokoka kutokana na dhambi ya kifo cha kijahiliya.

Viongozi wa makabila waliwasifu na kuwatukuza wajumbe wa Hizb ut Tahrir, na walithamini dori ya utangulizi ya hizb katika kuhakiki hali ya Sudan. Baadhi yao walisema, “Maadamu hii ndio njia yenu, sisi tuko pamoja nanyi moyo na roho,” bila hata mmoja wao kusema, “Nihesabuni kuwa mimi ni mshiriki wa heshima pamoja nanyi.” Baadhi yao walionyesha matakwa yao ya kuanzishwa Khilafah leo kabla ya kesho, na baadhi yao walieleza kuunga mkono wazo hilo: “Sisi tuko pamoja nanyi na tunaunga mkono jitihada zenu za kukusanya safu, kuunganisha neno, na kusimamisha Khilafah”. Viongozi hao wamewashukuru wajumbe wa Hizb ut Tahrir, na wakasema wako tayari kuunga mkono Uislamu na kutekeleza Sharia yake. Walisema wanapinga mipango ya kuisambaratisha nchi na kupora utajiri wake, na wote walisisitiza kuendelea kwa mawasiliano na mikutano.

2/ Msemaji Rasmi katika Wilayah ya Sudan na Kadhia za Sudan

Msemaji wa kheri, Ustadh Ibrahim Othman Abu Khalil, alikabiliana na njama zilizokuwa zikipangwa kwa siri na hadharani. Alitoa taarifa baada ya taarifa akifichua mipango ya mkoloni kafiri nchini Sudan, akizingatia suala la kujitenga kwa Darfur na uhalifu mwingine uliofanywa dhidi ya Umma. Alitoa taarifa kwa vyombo vya habari yenye kichwa: "Shirika la IGAD, Baba wa Kujitenga kwa Sudan Kusini, Larudi Kuendelea na Dori Yake Chafu." Pia alitoa taarifa yenye kichwa cha habari: "Amerika na Hatua ya Kusonga Mbele ya Kuivunja Darfur Kupitia Eneo Lisiloruhusiwa Kuruka!" na taarifa kuhusu masaibu ya mji mkuu wa utawala, Port Sudan, kutoka giza linalodumu kwa masaa mingi mchana na usiku kutokana na kukatika kwa umeme mara kwa mara, miongoni mwa masuala mengine.

Pia alifanya mkutano na waandishi wa habari katika afisi ya hizb mjini Port Sudan yenye kichwa cha habari: "Mamlaka Kati ya Dhana za Kushiriki Nyara na Jukumu la Kisheria."

3/ Hotuba za Kisiasa

Hotuba za kisiasa zilishuhudiwa zilizofanywa mwezi huu na Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan katika Soko Kuu la Port Sudan, mji mkuu wa utawala, zilishughulikia mada kadhaa muhimu sana. Miongoni mwazo ilikuwa suala la ukabila, ambalo linagawanya Ummah. Katika hotuba moja, Ustadh Hussein al-Hadi alielezea jinsi amri na sheria za Uislamu zilivyoweza kuunganisha makabila na watu wa nchi ambazo Uislamu ulienea, na jinsi maingiliano ya Waislamu na wengine katika kuishi na kupitisha mitindo ya maisha ya Kiislamu yalivyowafanya wote kuwa ndugu wa upendo. Kisha akasema kwamba majaribio ya watu leo ​​ya kushikamana na nchi zao na makabila yao yanaongeza mgawanyiko tu na hayatawaunganisha kama Mwenyezi Mungu alivyoamuru.

Katika hotuba nyingine yenye kichwa, "Je, mnaamini baadhi Kitabu na mnakufuru baadhi?", Ustadh Ibrahim Musharraf alizungumzia baadhi ya dhana potofu zilizoenea miongoni mwa Waislamu, kama vile kuchagua ya hukmu za Kiislamu, kutenganisha siasa na ibada, na kusita kwa baadhi ya Waislamu kushiriki katika amali za kisiasa. Alifafanua kwamba siasa ni usimamizi wa mambo, kwamba ni wajibu kwa Waislamu, na kwamba ni miongoni mwa shughuli bora zaidi ambazo Ummah unapaswa kufanya.

Kisha kukaja mjadala kuhusu utawala katika Uislamu, ukisisitiza kwamba ni amana na jukumu kubwa, sio kinyang’anyiro kama inavyotokea leo, ambapo watu hushindania nafasi za madaraka, hata kwa gharama ya maisha. Jukumu hili linajidhihirisha katika usimamizi sahihi wa mambo na kuhakikisha kutimiza mahitaji msingi ya binadamu chini ya Khilafah Rashida kwa njia ya utume.

Mjadala kuhusu dhamana ya Uislamu ya mahitaji ya msingi. Mzungumzaji, Ustadh Adel Ibrahim, alibainisha mahitaji msingi ambayo Uislamu ulikuwa na hamu ya kuhakikisha kwa kila mtu binafsi: chakula, mavazi, malazi, usalama, huduma ya afya, na elimu. Mahitaji haya hayajatimizwa tangu kuanguka kwa Khilafah hadi leo kwa sababu mifumo ya sasa inafungamanisha upatikanaji wa mahitaji haya na utajiri, ambao watu wengi hawawezi kumudu.

Hotuba ya mwisho kati ya hizi ilikuwa mnamo Agosti 31, 2026, yenye kichwa: "Hukmu za Kiislamu kuhusu Miamala ya Kifedha." Mzungumzaji alielezea baadhi ya miamala ya riba kwa watu binafsi na benki, akifafanua kwamba kuwepo kwayo kunatokana na uhalisia kwamba jamii tunayoishi si ya Kiislamu, na mifumo yake si ya Kiislamu. Alieleza kwamba miamala hiyo haramu ya kifedha haina nafasi chini ya sheria ya Kiislamu, kwani watu binafsi na dola wanafungwa na hukmu za Kiislamu. Kisha akawasihi Waislamu kubadilisha uhalisia huu kwa kusimamisha Khilafah Rashida ulioongozwa kwa njia ya Utume, unaotekeleza Uislamu na kubeba ujumbe wake kwa walimwengu.

Katika mji mkuu, Khartoum, hizb ilitoa hotuba ya hadhara huko Omdurman katika Msikiti wa Sheikh Jaafar kuadhimisha siku ya kuzaliwa Mtume Muhammad (saw). Ustadh Ahmed Abkar, wakili, alihutubia mkutano huo, akielezea kwamba siku ya kuzaliwa Mtume si tukio la kupita tu lililo na shughuli chache katika baadhi ya misikiti na viwanja vya umma, bali ni tukio muhimu la kihistoria. Alisisitiza kwamba Mtume (saw) alileta ujumbe wa ulimwengu wote, akasimamisha dola, na kueneza da’wah ya Uislamu, misheni inayoendelezwa na warithi wake (Mwenyezi Mungu awe radhi nao). Na kwamba Umma leo lazima ufuate njia hiyo hiyo. Aliwapa jukumu la kufanya kazi ya kuregesha tena maisha kamili ya Kiislamu.

4/ Majukwaa ya Hizb ut Tahrir

A/ Jukwaa la Masuala ya Ummah Linajadili Athari Mbaya za Bwawa Kuu la An-Nahdha

Jukwaa la Masuala ya Ummah, lililofanyika katika afisi ya Hizb ut Tahrir jijini Port Sudan, lilijadili suala la Bwawa Kuu la An-Nahda la Ethiopia na athari zake mbaya kwa Sudan. Ustadh Ahmed Al-Khatib aliangazia matokeo mabaya ya hali ya sasa, ikiwa ni pamoja na kupungua kwa Mto Nile na uhaba wa maji unaosababishwa. Alibainisha kuwa Hizb ut Tahrir ilikuwa imeonya dhidi ya hili katika majukwaa mengi, taarifa, na katika kijitabu kilichochapishwa mnamo Septemba 2017. Pia alifafanua uzembe wa watawala wa Sudan na Misri kuhusu haki za Ummah. Kisha Ustadh Hussein Al-Hadi alizungumzia kanuni za kisheria za Kiislamu za kushughulika na mito kama mali ya umma, akisisitiza wajibu wa serikali kuitunza, kuilinda, na kuisafisha, na kuzuia uvamizi wowote juu yake. Alidai kwamba tishio hili lililotolewa na Ethiopia kuhusu bwawa hilo lisingetokea kama Waislamu wangekuwa na Khalifa anayewaongoza kwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah ya Mtume Wake (saw). Alihitimisha kwamba ni Khilafah pekee ndiyo inayoweza kulinda maslahi ya Waislamu, hata kama italazimika kutumia nguvu za kijeshi.

B/ Tatizo la Elimu katika Jukwaa la Al-Qadharif

Katika Jukwaa la Hizb ut Tahrir/Sudan mjini Al-Qadharif, matatizo ya elimu yalijadiliwa, yakizingatia tofauti kati ya Khilafah na kushindwa kwa dola za kizalendo. Waraka wa kwanza uliwasilishwa na Ustadh Maysara Yahya, mwanachama wa afisi ya habari ya hizb katika wilayah ya Sudan. Alizungumzia jinsi Wamagharibi makafiri, baada ya kuvunjwa Khilafah, walivyoweka lazimisha thaqafa yao na kuifanya kuwa sehemu ya mifumo ya elimu iliyopo katika nchi zetu, hivyo kutenganisha dini na dola na kuingiza fikra za kibepari. Kisha akaashiria dola kuachana na matumizi kwa ajili ya elimu na ubinafsishaji wake. Mzungumzaji wa pili kisha akafafanua misingi ya elimu ya kimfumo iliyoanzishwa na Mtume Muhammad (saw) na kufuatiwa na Makhalifa baada yake. Alibainisha kuwa misingi hii ilizalisha watu wenye ushawishi wa Kiislamu waliobadilisha ulimwengu.

5/ Saluni ya Kisiasa:

Dori ya Mashirika ya Kikanda katika Siasa za Sudan

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir nchini Sudan ilimkaribisha Ustadh Yaqoub Ibrahim, mwanachama wa Hizb ut Tahrir, katika Saluni yake ya Kisiasa, iliyofanyika katika afisi ya Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan jijini Port Sudan. Alijadili dori ya mashirika ya kikanda katika siasa za Sudan, akizingatia Muungano wa Afrika, IGAD, na Umoja wa Kiarabu, ambao alielezea kama zana za Marekani katika eneo hilo. Alielezea ulaghai wao na kuingilia kwao katika kugawanyika kwa Sudan, akielezea dori ya kila shirika katika kujitenga kwa Sudan Kusini kutoka Kaskazini, na dori yao ya sasa katika kutekeleza mpango wa Amerika wa kugawanya Darfur. Alihitimisha mazungumzo yake kwa hukmu ya kisheria ya Kiislamu inayohusiana na ushiriki katika mashirika haya na uwepo wao katika nchi yetu, akisisitiza uharamu wa kuyaruhusu kuingilia mambo ya Waislamu, akinukuu Kifungu cha 191 cha rasimu ya katiba ya dola ya Khilafah.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan

Jumatatu, 18 Rabi' al-Awwal 1448 H, sawia na 31 Agosti 2026 M

Kwa Maelezo Zaidi Tafadhali Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir/ Wilayah Sudan:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Chaneli ya YouTube ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.