Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir/ Uholanzi

Kongamano la Kila Mwaka:

Kuamiliana na Watu wenye Mawazo Tofauti Tofauti ndani ya Dola ya Khilafah

Hizb ut Tahrir / Uholanzi iliandaa kongamano lake la Khilafah la kila mwaka kwa anwani: "Kuamiliana na Watu wenye Mawazo Tofauti Tofauti ndani ya Dola ya Khilafah" kwa mnasaba wa kumbukumbu ya miaka 101 ya kuvunjwa Dola ya Kiislamu (Khilafah)

Jumamosi, 02 Shaban 1443 H sawia na 5 Machi 2022 M

Hotuba za Kongamano

"Historia ya Sera ya Uoanishaji Inayofuatwa na Serikali ya Uholanzi"

Iliyotolewa na Ustadh Kamal Abu Zaid

Ustadh Kamal Abu Zaid alieleza kuwa sera hii haikuzaliwa leo, bali ni ya zamani tangu miaka ya sitini ya karne iliyopita, na ilianza kwa kuwataka Waislamu kuoanishwa katika jamii, na kuendelezwa hadi kila Muislamu machoni mwa serikali akawa mtuhumiwa mpaka kutokuwa kwake na hatia kuthibitishwe, na misikiti na shule zikawekwa chini ya uangalizi.

“Kampeni dhidi ya Uislamu Haikufunguka kwa dola bila ya kuwepo dola”

Iliyotolewa na Dkt. Abdul Wahid / Uingereza

Dkt. Abdul Wahid alijadili kile ambacho serikali ya Uingereza inafanya kuwatia usekula watoto wa Kiislamu na kuwaoanisha katika jamii za Magharibi, na kwamba sera iliyotangazwa na Tony Blair baada ya shambulizi la bomu lililotokea jijini London mwaka 2005 ni sera hiyo hiyo anayoilingania Macro leo nchini Ufaransa na serikali ya Austria na hata ya China inailingania kwa ndugu zetu Waislamu katika Turkestan Mashariki.

Ugumba wa Hadhara ya Kimagharibi na kuitokubali kwake nyengine

Iliyotolewa na Ustadh Okay Pala

Ustadh Okay Pala alizungumzia kushindwa vibaya kuamiliana na Waislamu, na jinsi fahamu ya wengi huwatawala wachache, iliyoibuka baada ya kuasisiwa kwa dola ya kikanda, ilipelekea mizozo na ushindani kutokana na imani tofauti tofauti na kile kinachotokamana nazo. Ama Uislamu uliwaacha wasiokuwa Waislamu na yale waliyoyaamini, na ukazuia kulazimishwa kwao kubadili imani makinaifu haya, na ukawafanyia uadilifu na haukuwapokonya haki zao.

Link za Ziada

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Uholanzi

Facebook: Hizb ut Tahrir / Uholanzi

Twitter: Hizb ut Tahrir / Uholanzi

Instagram: Hizb ut Tahrir / Uholanzi

أقيموا_الخلافة#

 #الخلافة_101

#Time4Khilafah

#ReturnTheKhilafah

#YenidenHilafet

#TurudisheniKhilafah

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.