- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Uholanzi: Semina Jijini Amsterdam “Gaza Yalilia Msaada!”
Kwa kuzingatia mauaji ya kikatili (mauaji ya halaiki) ambayo yamekuwa yakiendelea kwa zaidi ya miezi 18, yanayofanywa na umbile halifu la Kiyahudi dhidi ya Waislamu wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza uliozingirwa, ambayo yamesababisha kuuawa shahidi, kujeruhiwa, na kupoteza zaidi ya wanaume na wanawake wa Kiislamu 180,000 hadi sasa, Hizb ut Tahrir, Uholanzi iliandaa semina katika mji mkuu wa Uholanzi, Amsterdam yenye kichwa:
“Gaza Yalilia Msaada!”
Katika kuwanusuru watu wetu mjini Gaza, ambao wanakabiliwa na aina mbaya zaidi za mauaji ya halaiki: mauaji, njaa, na kuhamishwa kiserikali na umbile halifu la Kiyahudi, na kutelekezwa kwa kuchukiza na tawala shiriki, vibaraka za Kiarabu.
Semina ilianza kwa usomaji mzuri wa aya za Quran Tukufu. Kisha Ndugu Abdul Malik alitoa hotuba kuhusu kadhia ya ardhi iliyobarikiwa (Palestina) kwa mtazamo wa kihistoria, na jinsi nchi kafiri za kikoloni za Magharibi zilivyotengeneza umbile kwa ajili ya Mayahudi kuwa na msingi wa hali ya juu katika moyo wa ulimwengu wa Kiislamu na walinzi wa kuuzuia Umma usitilie maanani kadhia zake muhimu na kuzuia umoja wake kwa misingi ya Uislamu.
Hotuba ya pili ilitolewa na ndugu Bilal, ambaye alitaja kuwa suluhisho la kadhia ya Palestina haliko katika kusitisha vita, mazungumzo, kuleta misaada, au masuluhisho mengine ya muda, bali suluhisho liko katika kuikomboa ardhi yote iliyobarikiwa (Palestina), kwa kuyalazimisha majeshi katika nchi zinazoizunguka angalau kuelekea Palestina ili kuikomboa na kuwaangamiza Mayahudi na kuwafanya wawe mfano kwa watakaokuja baada yao, na hili kamwe halitapatikana kabla Waislamu kuinuka dhidi ya watawala vibaraka na wasaliti na kuregesha mamlaka yao juu ya nchi na majeshi yake. Semina hiyo ilihitimishwa kwa kutoa fursa kwa hadhira iliyojaa ukumbini kuuliza maswali kwa wahadhiri. Na dua yetu ya mwisho ni kwamba himdi zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.
Jumapili, 20 Dhu al-Qi'dah 1446 H sawia na 18 Mei 2025 M
https://www.hizb-ut-tahrir.info/sw/index.php/dawah/uholanzi/4667.html?print=1&tmpl=component#sigProId108ccbd4b3
#طوفان_الأقصى
#الجيوش_إلى_الأقصى
#الأقصى_يستصرخ_الجيوش
#ArmiesToAqsa
#AksaTufanı
#OrdularAksaya
#Aqsa_calls_armies
#AqsaCallsArmies
Kwa Maelezo zaidi, Tafadhali Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Uholanzi:
Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Uholanzi
Facebook: Hizb ut Tahrir / Uholanzi
Twitter: Hizb ut Tahrir / Uholanzi
Instagram: Hizb ut Tahrir / Uholanzi