Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Halaqa ya Mjadala Mjini Kirikkale Kutafuta Suluhisho la Kiislamu kwa mgogoro wa kiuchumi

Ndani ya wigo wa msururu wa makongamano, semina na halaqa za mjadala zilizoandaliwa na Hizb ut-Tahrir / Wilayah Uturuki chini ya kichwa "Suluhisho la Kiislamu kwa Mgogoro wa Kiuchumi", sanjari na mnasaba wa kumbukumbu ya miaka 101 ya kuvunjwa Khilafah mnamo tarehe 28 Rajab 1342 H, Hizb ilikutana na wawakilishi wa vyama vya kisiasa, mashirika yasiyo ya kiserikali, wawakilishi wa vyombo vya habari vya ndani na walezi katika mji wa Kirikkale.

Katika mkutano huo uliofunguliwa na Ndugu Ali Karatiba, Ustadh Suleiman Ugarlua (Mhariri Mkuu wa Jarida la Kokludegisim), aliwasilisha utafiti kwa kichwa "Suluhisho la Kiislamu kwa Mgogoro wa Kiuchumi katika Nukta Kumi"

Baada ya uwasilishaji, kipindi cha maswali na majibu kilifanyika na maoni ya wageni yalisikilizwa juu ya suluhisho lililopendekezwa. Washiriki walitoa michango muhimu kwa maswali, na maoni yao, na ndugu Hakki Irin na Abdullah Imamoglu wote walijibu maswali kutoka kwa wahudhuriaji.

Kwa Mengi zaidi Bonyeza Hapa

Ijumaa, 01 Shaaban 1443 H - 04 Machi 2022 M

Kwa Maelezo Zaidi Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Ukurasa wa Twitter wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Akaunti ya Instagram ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Chaneli ya YouTube ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Tovuti ya Jarida la Kokludegisim

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.