- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki:
Amali Kubwa “Iokoeni Al-Aqsa! Simameni dhidi ya Amerika!”
Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Uturuki, kupitia matembezi mikubwa na taarifa kwa vyombo vya habari zilizoandaliwa kote Uturuki chini ya kauli mbiu “Iokoeni Al-Aqsa! Simameni dhidi ya Amerika!”, ililaani ukandamizaji wa umbile nyakuzi la Kizayuni, kiburi cha mkoloni Amerika, na kimya cha watawala wa nchi za Kiislamu kuhusu udhalilishaji huu.
Amali hizo, zilizoanza jijini Mersin manmo Ijumaa, ziliendelea Jumapili jijini Adana, Ankara, Aydın, Bursa, Düzce, Gaziantep, Istanbul, İzmir, na Kocaeli, ambapo Waislamu walikusanyika katika viwanja na maeneo ya umma, wakiimba mbele ya ulimwengu mzima, “Ummah Mmoja, Dola Moja, Suluhisho Moja: Khilafah.”
Jumapili, 18 Shawwal 1447 H – 05 Aprili 2026 M

Wito kwa Majeshi kwa ajili ya Al-Aqsa
Katika Uwanja wa Ulus, jijini Ankara
Programu ilianza katika mji mkuu, Ankara, kwa matembezi hadi Uwanja wa Ulus baada ya swala ya adhuhuri katika Msikiti wa Hacı Bayram. Amali hii iliwasilishwa na İsa Aslan na Mustafa Ünük, na ilijumuisha taarifa kwa vyombo vya habari iliyosomwa na Emre Taş.
Taarifa hiyo ilisisitiza kwamba mauaji ya halaiki huko Gaza, yanayoendelea kwa zaidi ya miaka miwili, ni mojawapo ya sura zenye giza zaidi katika historia ya binadamu. Taarifa hiyo kwa vyombo vya habari ilisema yafuatayo:
“Umbile nyakuzi la Kizayuni linaendelea kufanya mauaji dhidi ya ndugu na dada zetu, bila kujali jinsia au umri, likilenga hospitali, misikiti, na shule. Imeelezwa kwamba juhudi za kidiplomasia zinazofanywa chini ya kivuli cha 'udanganyifu wa amani,' unaofadhiliwa na Amerika ya kibeberu, zinatumika tu kuhalalisha uvamizi huo.”
Taarifa hiyo kwa vyombo vya habari ilisisitiza zaidi kwamba usemi wa “mistari nyekundu” unaotumiwa na viongozi wa Waislamu ni mazungumzo matupu tu, na kwamba kushindwa kuchukua hatua madhubuti, hata ingawa Msikiti mtukufu wa Al-Aqsa bado umefungwa kwa waumini, ni tusi lisilo na kifani katika historia.
Ilisisitizwa kwamba chanzo kikuu cha migogoro inayoukumba ulimwengu wa Kiislamu ni kutokuwepo kwa utashi wa kisiasa, na kwamba ukombozi kutoka kwa fedheha hii unaweza kupatikana tu kupitia Khilafah Rashida iliyosimamishwa kwa njia ya Utume.

- Sehemu ya Amali za Jiji la Ankara -

Roho ya Izza na Upinzani
Huko Uskudar, Istanbul
Katika amali za jiji la Istanbul, Waislamu walitembea pamoja sako kwa bako kutoka Uwanja wa Festikka Ağaçı hadi Uwanja wa Üsküdar, wakionyesha kwamba ardhi iliyobarikiwa (Palestina) haiko peke yake. Taarifa kwa vyombo vya habari ilisomwa na Muhammad Amin Yıldırım, mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir nchini Uturuki.
Programu hiyo pia ilijumuisha hotuba za mtafiti na mwandishi Ahmet Farol na kiongozi wa Hamas Talal Nassar, ambao walisisitiza umuhimu wa umoja wa Waislamu na hitaji la viongozi kuhamasisha majeshi yao.
Kauli mbiu kama vile “Majeshi kwa Al-Aqsa,” “Kurcik, Incirlik, aibu iliyoje hii!” na “Suluhisho pekee ni Khilafah” ziliimbwa katika viwanja.
Amali hizo zilimalizika kwa dua: “Ewe Mwenyezi Mungu, turuzuku uwezo wa kusimamisha tena Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume. Na utujaaliye kuikomboa Al-Qudsi na Msikiti wa Al-Aqsa kwa majeshi ya Khilafah, na kusimama nyuma ya Khalifa mwema!”

- Sehemu ya Amali za Jiji la Istanbul -

- Angazo la Picha za Amali -

- Sehemu ya Amali za Semina na Mikutano -
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
https://www.hizb-ut-tahrir.info/sw/index.php/dawah/uturuki/5323.html?print=1&tmpl=component#sigProIdffbf77507b

- Alama Ishara -
#الجيوش_إلى_الأقصى
#الأقصى_يستصرخ_الجيوش
#OrdularAksaya
#ArmiesToAqsa
#AqsaCallsArmies

Kwa Maelezo zaidi Tafadhali Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki:
Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki
Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki
Ukurasa wa Twitter wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki
Akaunti ya Instagram ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki
Chaneli ya YouTube ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki
Tovuti ya Jarida la Kokludegisim
