Al-Waqiyah TV: Kwa Mukhtasari “Je, Unamjua Yeye ni Nani?!"
- Imepeperushwa katika Al-Waqiyah TV
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Al-Waqiyah TV: Kwa Mukhtasari “Je, Unamjua Yeye ni Nani?!"
Al-Waqiyah TV: Kwa Mukhtasari “Je, Unamjua Yeye ni Nani?!"
Serikali ya Misri ilitangaza kusherehekea utekelezwaji wa mpango wa Trump mjini Gaza. Sisi alimwalika Rais wa Marekani kusherehekea kwa sababu yeye ndiye mwanzilishi wa mpango wa Gaza: [Rais Trump wa Marekani alisema mnamo Alhamisi kwamba mateka waliosalia wanaoshikiliwa na Hamas katika Ukanda wa Gaza wataachiliwa huru mnamo Jumatatu au Jumanne ya wiki ijayo, na kwamba bado analenga kuzuru eneo hilo kusherehekea hafla hii... “Ni muhimu kutaja kuwa Rais Sisi wa Misri alikuwa amemwalika Trump kushiriki katika sherehe ambazo zitafanywa nchini Misri ili kuadhimisha kutiwa saini kwa makubaliano, akiyachukulia kuwa makubaliano ya kihistoria ambayo yanazifisha taji juhudi za Misri, Marekani, na wapatanishi katika kipindi cha hivi karibuni.” (CNN Arabic, 9/10/2025)]
Al-Waqiyah TV: Lau Wangekuwa Wakweli kwa Mwenyezi Mungu ﷻ... watawala wetu hawangekuwa na kiburi!
Al-Waqiyah TV: Kwa Mukhtasari... Kuwadhibiti Wanaodhulumiwa... Kwa Dhulma Zaidi?!
Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir inafuraha kuwasilisha kwa wafuasi na wanaozuru kurasa za Afisi Kuu Habari DVD mpya katika lugha tatu yenye kichwa: “Nasheed za Khilafah 1447 H - 2025 M”
Trump alisema katika chapisho kwenye jukwaa lake la Kijamii la Ukweli: “Ninafuraha kuripoti kwamba tuna mazungumzo yenye msukumo na yenye natija na Jumuiya ya Mashariki ya Kati kuhusu Gaza,” na kuongeza kuwa, “mazungumzo makali yamekuwa yakiendelea kwa siku nne, na yataendelea kwa muda mrefu iwezekanavyo ili kupata Makubaliano Yanayokamilishwa kwa Mafanikio.” (Truth Social; TRT Kiarabu, 27/9/2025)
Al-Waqiyah TV: Trump ndiye Muungaji Mkono Mkuu wa Umbile la Kiyahudi katika Uhalifu wake wa Kutisha mjini Gaza na Palestina yote
Sudan kwa sasa iko katikati ya vita vya kipumbavu ambavyo vimesababisha vifo vya makumi ya maelfu ya raia na kuzua mgogoro mkubwa zaidi duniani wa njaa na kuhama makaazi. Wananchi wa Sudan wamekumbwa na mizozo mbalimbali pamoja na umaskini mkubwa, udikteta, migawanyiko ya kikabila na kitabaka na matatizo mengine mengi ya kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa miongo kadhaa chini ya uongozi, tawala na mifumo mtawalia.
Al-Waqiyah TV: Ukweli Uliofichuliwa na Matokeo ya Kimbunga cha Al-Aqsa!
Tunajua kwamba mkakati wa Marekani wa kuasisi umbile la Kiyahudi katika moyo wa nchi za Kiislamu, kwa sehemu kubwa, umeegemezwa kwenye suluhisho la dola mbili. Hata hivyo, chini ya Trump, mkakati huu umeanza kuatelekezwa, au angalau kunyamaziwa, jambo ambalo limezua maswali. Kwa mfano, Trump alisema, "Unapotazama ramani, ramani ya Mashariki ya Kati, 'Israel' ni sehemu ndogo sana ikilinganishwa na ardhi hizi kubwa mno. Kwa hakika nilisema: 'Je, kuna njia yoyote ya kupata zaidi? Ni ndogo..." (Sky News, 19/8/2024). Je, hii inamaanisha kuwa mradi wa suluhisho la dola mbili wa Amerika umekufa na kukamilika, au bado ungali hai?