Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan: Amali za Kuhuisha Ibada za Dhu al-Hijjah za Mwaka 1447 H
- Imepeperushwa katika Sudan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Katika kuhuisha ibada za Dhul-Hijjah na kwa heshima ya Sunnah tukufu ya Mtume, Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan iliandaa maandamano ya takbira na tahlil mnamo Jumatatu, ya kwanza ya Dhul-Hijjah 1447 H. Maandamano yalianza kwenye lango la afisi ya hizb mjini Port Sudan, yakipita kwenye njia kuu, na kufikia Soko Kuu, ambapo yalifikia kilele chake katika ua wa Hoteli ya Al-Haramain, mahali pa mikutano ya kisiasa ya mji huo. Wakati wa maandamano hayo, umati mkubwa wa watu ulijiunga, wakipiga takbira na tahlil pamoja na ndugu zao, wakionyesha furaha yao kwa amali ya hizb na kusifu amali hii ya kipekee nchini, kwa mujibu wa maelezo yao.



