Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 620
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Khilafah Pekee ndiyo Itakayohamasisha Vikosi vya Kijeshi Kuikomboa Palestina, Kutoka Mtoni hadi Baharini!
Umati mkubwa wa wanawake kutoka Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina waliitikia wito wa dada zao huko Khalil (Hebron) kwa mkutano wa kipekee wa kujadili hukmu za Kiislamu kuhusu wanawake na familia za Kiislamu. Lengo lilikuwa kuwalinda na kuwaelimisha dhidi ya kampeni za Magharibi na ufisadi zinazotaka kuwaangamiza, na hivyo, familia na jamii, kupitia mbinu na njia mbalimbali.
Mkusanyiko wa video zinazowahutubia Waislamu nchini Uswidi, zinazojadili hatari za kushiriki katika uchaguzi ujao wa bunge la Uswidi na jinsi hii inaweza kusababisha kuoanishwa kwa Waislamu ndani ya jamii ya Uswidi.