Jumapili, 29 Jumada al-thani 1441 | 2020/02/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

“Kuyeyuka kwa Familia” za Mujatamaa wa Kisekula wa Kimagharibi SEHEMU 2: Sababu za Kuyeyuka kwa Familia Katika Dola za Kisekula za Kimagharibi

Serikali za Kimagharibi zimejaribu kuzindua miradi kadha wa kadha ili kuzuia wimbi la kuvunjika kwa familia ndani ya mujtamaa zao. Lakini, haya yameambulia patupu. Hii ni kwa sababu wameshindwa kutambua kwamba sababu msingi za kuyeyuka huku kwa familia ni maadili msingi ya kisekula na ukosefu jumla wa umuhimu unaopatiwa ndoa na maisha ya familia ndani mujtamaa huru za kirasilimali.

Soma zaidi...

Maisha haya ya dunia si chochote bali ni mafupi, kwa hiyo Tumcheni Mwenyezi Mungu (swt) kikamilifu

Uendaji mbio, uchangamfu, uchukuliaji mambo kwa udharura na upangaji mipango na ufuatiliaji katika kufanya da’wah tuliouona katika maisha ya Mtume (saw) ilikuwa sio eti ana “dhibiti wa wakati”. La, ilikuwa ni athari ya kukatikiwa juu ya maisha haya ya dunia, kama ilivyo pambanuliwa katika yale ambayo Mwenyezi Mungu (swt) aliyoyaeleza. Hakika, uhai umedhihirishwa kuwa ni mfupi, hata na wale ambao wameishi muda mrefu miongoni mwa watu.

Soma zaidi...

Utafutaji wa Shahada (Kifo katika Jihadi)

Utafutaji wa shahada imekuwa daima ni fahamu msingi ndani ya elimu ya kijeshi enzi za Uislamu. Pamoja na masomo juu ya zana za vita, mikakati na mbinu, utafutaji wa shahada ulitizamwa kama msingi wa fahamu za masomo, uelewaji na ujengaji wa nafsiyya. Utafutaji wa shahada ndio uliotia nishati majeshi ya Kiislamu katika vita, ukiwawezesha kufikia yale ambayo wengine walishindwa kuyafikia na wasingejaribu kuyafikia.

Soma zaidi...

Kujitoa Muhanga Nafsi yako, Fedha zako na Wakati wako, ni moja katika sifa muhimu za Mbebaji Da'wah

Kubeba Da'wah ni kazi kubwa mno na ni njia iliyojaa magumu na matatizo, njia ambayo ilipitiwa hapo awali na Mtume wetu (saw) na Maswahaba zake (ra) na kuikabidhi wale ambao wameiamini Da'wah hii baada yao; ili kumlingania mwanadamu kutoka katika kuabudu viumbe na kumuita katika kumuabudu Muumba pekee. Hakuna ambaye anaweza kuyabeba magumu na matatizo ya njia hii isipokuwa mtu ambaye amejifunga, amejirekebisha na kujikuza mwenyewe kwa sifa za uzuri ambazo ni lazima awe nazo mbebaji Da'wah na sifa kubwa katika hizo ni 'kujitoa muhanga.

Soma zaidi...

Yemen: Maswali ambayo kila mmoja anatakiwa kujiuliza!

Inawezekana vipi kujiandaa kila siku tukiwa na akili timamu, kuwaandalia chakula kizuri watoto wetu, kuwavisha mavazi mazuri na masafi na kuwalea kwa utulivu na mapenzi tukiwalaza, LAKINI tukitazama kiuzembe takribani watoto milioni 1.8 wa Ummah huu ndani ya Yemen wakidhoofika na kuangamizwa bila huruma? Inawezekana vipi sisi tuwe na furaha kwamba watoto wetu wanakuwa na kustawi, wakati takribani watoto 500,000 ndani ya Yemen hawataona siku ya kuzaliwa kwao kutokana na vita vya leo dhidi ya Uislamu?

Soma zaidi...

Talaka ni Halali Hata Kama ni Halali Inayo Chukiwa Zaidi

Kwa kuwa ni sheria kamili, imemsimamia mwanadamu na kumpatia njia za kumuwezesha kukidhi mahitaji yake ya kiviungo na kighariza pasina na kumsababishia majonzi yeye na wanadamu wengine. Na kuweka suluhisho mwanana na zilizo kamilika kwa matatizo na mazito yote anayo kumbana nayo. Huu ni Uislamu, Dini ambayo Muumba ameiidhinisha kwa watumwa Wake ili waweze kuishi kwa kufurahi, kutosheka na kutaka radhi za Mwenyezi Mungu wao.

Soma zaidi...

Je ni kweli wanakataa “ndoa za mapema”?!

“Ndoa ya mapema ni tabia ya aibu." "Ndoa ya mapema ni msiba kwa mvulana na msichana." "Ndoa za mapema hupelekea matatizo ya kiakili, kiafya na kifamilia na kupoteza haki za watoto." Kauli hizo ndizo zinazojirudia mara kwa mara katika semina na makongamano yanayofanywa na taasisi za wanawake au vituo vya haki za binadamu. Na hata katika mabunge ya nchi nyingi wanapotunga sheria za familia mara nyingi huwa wanaongeza umri wa kuoana au wanapendekeza sheria ya kuzuia ndoa kwa vikundi vya vijana kwa umri maalum.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu