Ahadi na Matumaini ya Serikali ya Iraq ni kama Mangati (Sarabi) ambayo Mwenye Kiu Huiona kuwa ni Maji!
- Imepeperushwa katika Iraq
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Baada ya Marekani kusisitiza kumweka Ali Al-Zaidi kama Waziri Mkuu wa Iraq na kumuunga mkono, huku ikimkataa mgombea wa Muungano wa Uratibu (Coordination Framework), Nouri al-Maliki, na kutishia kuweka vikwazo vya kiuchumi, na baada ya jambo hilo kufanikiwa kama ilivyotaka, ilifanya hatua kadhaa za kuboresha taswira yake na kuwashawishi wananchi wa Iraq kuwa yeye ndiye mtu sahihi kwa wakati huu, na mwenye uwezo wa kuiokoa Iraq na kuifikisha mahali salama. Hivyo, ilimwalika Washington kutangaza kuanza kwa awamu mpya kuhusu uchumi wa Iraq, jambo ambalo alianza kwa kampeni ya kuwawajibisha mafisadi.



