Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi Salih bin Muhammad al-Shafrah
- Imepeperushwa katika Tunisia
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Tunisia inaomboleza mmoja wa Mashababu wake, ndugu Salih bin Muhammad al-Shafrah, aliyefariki mnamo Jumamosi, tarehe ishirini na moja ya Rabi’ al-Awwal 1447 H sawia na 13/09/2025 M. Alikuwa miongoni mwa Mashababu wa Hizb ut Tahrir katika eneo la al-Qayrawān, ambaye alifanya kazi katika safu zake wakati wa zama zenye giza kuu za ukandamizaji na dhulma. Hakika alikuwa ameshikilia imara da‘wah yake, akijitolea katika kuibeba, akilingania Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, mwenye kuiamini ahadi ya Mola wake Mlezi na bishara njema ya Mtume wake Mtukufu (saw), mpaka alipofariki dunia. Hivyo ndivyo tunavyomhisabu, na wala hatumtakasi yeyote mbele ya Mwenyezi Mungu.