Hizb ut Tahrir / Indonesia: Matembezi Makubwa ya Kukumbusha Ulimwengu “Palestina ingali chini ya Uvamizi”
- Imepeperushwa katika Indonesia
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Maelfu ya Waislamu katika miji mbalimbali ya Indonesia walifanya matembezi yanayounga mkono Palestina mnamo Oktoba 18 na 19, 2025, chini ya kauli mbiu “Palestinaingali chini ya Uvamizi.” Huko Bandung, zaidi ya waandamanaji 15,000 walikusanyika mbele ya jengo la Gedung Sati, wakinyanyua bendera za Rayah zenye tamko la Tawhid na mabango yenye kauli mbiu kama vile “Tumeni majeshi ya Kiislamu, yakomboe Palestina!”, na “Suluhisho la mwisho kwa Palestina ni kupitia jihad na Khilafah,” na “Palestina itakombolewa kupitia Khilafah na Jihad.”



