Jumapili, 29 Jumada al-thani 1441 | 2020/02/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Ahadi ya Mwenyezi Mungu na Matumaini Yanayon’garisha Ummah Wetu Na ni Vipi Kuomba Nusra Kama Ilivyoahidiwa na Mwenyezi Mungu kwa Kufuata Nyayo za Watu Adhimu kama Muhammad al-Fatih

“Itakapo kuja nusura ya Mwenyezi Mungu na ushindi. Na ukaona watu wanaingia katika Dini ya Mwenyezi Mungu kwa makundi. Zitakase sifa za Mola wako Mlezi, na umuombe msamaha; hakika Yeye ndiye anaye pokea toba”. [An-Nasr:1-3]

Soma zaidi...

Vipi Khilafah Itakavyo Unda Familia Imara

Nguvu na utulivu wa familia ya Waislamu wakati mmoja iliwahi kuwa sifa ya kipekee ya Ummah huu wa Kiislamu. Gaston Jezz, profesa wa Kiswizi wa kanuni ya familia aliye zuru Jamhuri ya Uturuki kufuatia kuvunjwa kwa Khilafah Uthmaniya alisema kuwa utulivu wa imani za kidini katika ardhi hii, “ulizalisha nyumba za familia imara zaidi ulimwenguni, na umbile hili liliasisi maisha ya umma ambayo kamwe hayajawahi kuonekana katika historia ya taifa lolote.”

Soma zaidi...

Vipi Khilafah Itakavyo Kuwa Dola Inayo Ongoza Katika Sayansi na Teknolojia

Mapinduzi ya kiviwanda 4.0 yalitangazwa kama ajenda ya kiulimwengu katika Kongamano la Kiuchumi la Kiulimwengu la mwaka 2016, yaliwasili kama mafuriko makubwa katika biladi nyingi za Waislamu. Kuanzia mapinduzi ya kiviwanda 1.0 ambayo yalijiri katikati mwa karne ya 18 ambapo kuzuka kwa mitambo ya kutumia bukhari yalibadilisha (matumizi ya) wanyama wakati huo na kufanya mabadiliko ya kimsingi, hususan kwa uchumi wa kiulimwengu.

Soma zaidi...

Vipi Khilafah Itakavyo Unda Nidhamu ya Elimu ya Daraja ya Juu Kabisa

Ili kuunda Nidhamu ya Elimu ya Daraja ya Juu Kabisa ya aina hiyo yahitaji nidhamu ya kisiasa ya daraja ya juu kabisa – nidhamu inayo kumbatia ruwaza ya kisiasa ya kipekee, ya hali juu na huru kwa dola yake na kwa ulimwengu, iliyo jengwa kwa msingi wa ayah hiyo ya juu – kuwatoa watu kutoka katika giza la ujinga wa ukafiri na kuwapelekea katika nuru ya Uislamu na uadilifu na mafanikio unayoleta kwa wanadamu katika kila nyanja ya maisha – kiroho, kiakili, kiakhlaqi, kisiasa, kiuchumi, na katika sayansi na teknolojia.

Soma zaidi...

Vipi Khilafah Itakavyo Hifadhi Haki za Kisiasa za Wanawake

  • Uislamu huwawajibisha wanawake kuwa na dori changamfu katika siasa za mujtama wao: kuchunga mambo ya Ummah wao, kuzungumza dhidi ya ukandamizaji na ufisadi, kuamrisha mema (Ma’ruf) na kukataza maovu (Munkar), na kuwahisabu watawala wao. Dalili za Kiislamu zinazo waamrisha Waislamu kuwa wachangamfu katika siasa zinawahusu wanaume na hali kadhalika wanawake.
Soma zaidi...

Vipi Khilafah Itakavyo Sitisha Ukoloni ndani ya Ardhi za Waislamu

Leo kuna zaidi ya dola hamsini za Waislamu, zote zikidai kuwa Uislamu ndio dini yao na chimbuko la utambulisho wao. Dola zote hizi daima ziko katika mchakato wa kujenga na kujenga upya matumaini ya kufaulu katika malengo ya maendeleo yaliyowekwa na Wamagharibi. Malengo haya yanakwenda kinyume na dini ambayo wengi wanatangaza kujifunga kwayo kama dini ya dola.

Soma zaidi...

Vipi Khilafah Italinda Uislamu na Ummah wa Kiislamu

Tangu Makafiri walipovunja Khilafah Ottomaniya kwa mikono ya Mustafa Kamal, vibaraka Waingereza tangu kubuniwa kwao miaka 94 miladia iliyopita, Ummah wa Kiislamu haujaona zuri lolote isipokuwa kuwa nyuma ya mataifa, ukiishi chini ya hali halisi iliyojaa machungu na fedheha, udhaifu na utumwa. Unaishi chini ya muongozo wa kikafiri na wanaopigia debe ukafiri. Na unaendelea kula makombo kutoka katika meza za dunia huku ukiendelea kulizwa na mataifa yote kutoka Mashariki na Magharibi.

Soma zaidi...

Vipi Khilafah Itakavyo Andaa Jeshi Lenye Nguvu Duniani Litakalo Pambana kwa Ajili ya Uislamu

• Tangu kuvunjwa kwa Khilafah 1924, usalama umekosekana ndani ya ulimwengu wa Waislamu, na kuwapelekea Waislamu kukosa mlinzi dhidi ya uvamizi wa madola ya kiulimwengu na kimaeneo, mapambano baina ya Waislamu yaliyo dhaminiwa kutoka nje na mabomu ya droni na kupelekea damu za Waislamu kukosa thamani. Fauka ya hayo, kuwepo kwa mashirika ya kiusalama ndani ya ardhi za Waislamu na matumizi ya majeshi ndani ya ardhi za Waislamu kupambana na watu wao inaonyesha wazi namna watawala walioko mamlakani hivi sasa ndani ya ulimwengu wa Waislamu walivyo telekeza jukumu la kulinda maisha ya watu wao wa kawaida.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu