Alhamisi, 18 Ramadan 1445 | 2024/03/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ahadi Tupu kwa Wanawake wa Afghan

Ujumbe wa Afghan kwa Umoja wa Mataifa (UN) umeunda “Kundi la Marafiki,” linalosimamiwa na Uingereza na kujumuisha wawakilishi wa wanawake kwa UN na maafisa wakuu wa UN. Kundi hilo lilibuniwa kuwanusuru wanawake katika nyanja zote za maisha.

Ujumbe wa UN ndani ya Afghanistan (UNAMA) ulisema kupitia taarifa kwa vyombo vya habari mnamo Jumapili, 18 Novemba 2019 kwamba Kundi hili litaangazia umuhimu wa kulinda na kuboresha haki na dori ya wanawake ambayo wanaweza kucheza ndani ya mujtama na serikali kwa ujumla ikijumuisha juhudi za amani. Lengo la “Kundi la Marafiki” ni kuwawezesha na kutambua dori muhimu ya wanawake katika mustakbal wa Afghanistan. Malengo yao pia ni kuunnga mipango ya serikali ya Afghanistan na washirika wa kimataifa katika utekelezaji Maamuzi 1325 ya Baraza la Usalama la UN juu ya “Wanawake, Amani na Usalama.” Adela Raz, Mwakilishi wa Kudumu wa UN ndani ya Afghanistan, alisema katika sherehe ya uzinduzi wa Kundi: “Katika kipindi cha miaka 18 iliyopita, wanawake wa Afghan wamenyanyuka kama viongozi wa mabadiliko na wameanza kubadilisha hadithi kutoka kuwa ni waathiriwa na kuwa washirika. Ni sehemu ya hadithi yetu ya kufaulu, ni sehemu ya Afghanistan mpya, ambapo sote tunashirikiana ili kuhakikisha kuwa hakuna mwanamke anapigwa mawe hadi kufa; na kwamba anakatazwa kupewa elimu, na halazimishwi kubakia nyumbani. Ni wakati muhimu katika historia yetu ya kisiasa ambapo tumepanuka zaidi na uwekezaji wetu kwa wanawake wa Afghan lazima uendelee na uimarishwe.”

Kwa kuweka mipango hiyo, UN na wafanyikazi wake wanajaribu kuwaongoza wanawake wa Afghan kuamini kwamba kuna mustakbal mzuri ndani ya Afghanistan mpya. Kiasili ukweli uliochungu umefichika kwa wanawake na unawasilishwa kama ambaye wako njiani kuelekea kufaulu. Inawezaje kusemwa kwamba kuna kunyanyuka kwa ukweli kupitia tu serikali kuwapa viti baadhi ya wanawake ndani ya bunge au kuwapa baadhi nafasi ya kuingia katika soko la kisekula la ajira duniani au kuwaorodhesha baadhi yao kuwepo katika mashirika ya haki za wanawake; je yote haya ni kuionyesha dunia kwamba wanawake wa Afghan sasa wamekombolewa na kupata uhuru?

Je ni vipi kuhusu vifo vingi (kuanzia 1 Januari hadi 30 Juni 2019, mzozo wa kisilaha umesababisha wanawake 430 kuwa waathiriwa (vifo 144 na 286 kujeruhiwa), ni kupungua kwa asilimia 22 ikilinganishwa na kipindi sawia mnamo 2018 UNAMA), ukame (takribani wa Afghan milioni 5 wanauwezo mdogo au hawana kabisa wa kupata chakula, Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa), ukosefu wa usalama wa kiuchumi na kiwango cha umasikini (asilimia 54 cha watu wanaishi ndani ya umasikini, wengi wao ni wanawake na watoto, Shirika Kuu la Takwimu la Afghanistan), maelfu ya wanawake ambao hawana elimu (asilimia 84 ya wanawake wa Afghan bado hawajui kusoma na kuandika na ni asilimia mbili ya wanawake ambao wanapata nafasi ya elimu ya juu, Shirika Kuu la Takwimu), kuhangaishwa katika sehemu za kazi (asilimia 87 wamepitia kuhangaishwa katika sehemu za kazi na asilimia 91 ndani ya taasisi za elimu, Wakfu wa Utafiti wa Sheria ya Wanawake na Watoto), wajane (idadi ya wajane ndani ya Afghanistan inakadiriwa kuanza 600,000 hadi milioni mbili, moja ya viwango vya juu duniani, Wizara ya Afghanistan ya Usimamizi wa Mambo ya Mujtama), wanawake wanalazimishwa kuingia ukahaba na matumizi ya madawa ya kulevya (wako wanawake milioni 1 waliotekwa na madawa ndani ya Afghanistan, Wizara ya Afya ya Ummah), ufurushwaji wa wanawake (zaidi ya wa Afghan milioni 1.5 hivi sasa wamefurushwa kutokana na vita na mizozo, wengi wao ni wanawake na watoto, Kitengo cha Kufuatilia Ufurushwaji wa Ndani), wanawake ambao hawapati huduma muhimu (zaidi ya asilimia 50 ya wanawake wajawazito ndani ya Afghanistan hawapati huduma muhimu, Wizara ya Afya Ummah) na maelfu ya wanawake ambao wangelikimbia nje ya nchi lau wangelipata nafasi (karibia asilimia 50 ya wanawake wote wa Afghanistan wangeli kimbia nje ya nchi yao iliyokithiri vita lau wangeliweza, taarifa za Wakimbizi).

Kwa hiyo nukta ambazo zimetajwa katika hotuba ya Adela Raz, Mwakilishi wa Kudumu wa UN ndani ya Afghanistan ziko kinyume na uhalisia wa Afghan wanawake. Wanawake wa Afghan sio viongozi wa mabadiliko na sio washirika bali ni waathiriwa wa mipango fisadi ya Amerika na serikali ya Afghan. Leo wanapigwa mawe hadi kufa lakini wanauliwa kwa mamia kwa vita vya utawala. Wao hawajakatazwa kupata elimu lakini serikali haiwajali na kuwapa fursa hii. Leo hawalazimishwi kubakia nyumbani bali maelfu ya wanawake wa Afghan lazima watoke nje ili kwenda kuombaomba ili kupata mkate wao wa siku. Je hiyo ndio dori ya wanawake ndani ya Afghanistan mpya?

Kwa kuongezea sehemu ya jamii ya kimataifa, Afghanistan imejifunga na matangazo, mikataba na maamuzi ya UN inayojumuisha kushughulikia haki za wanawake na wanadamu. Miongoni mwa hizi ni Maamuzi ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa 1325 (UNSCR 1325) na Makubaliano ya Kuondosha Aina Zote za Unyanyasaji Dhidi ya Wanawake (CEDAW). “Kundi la Marafiki” linataka kunusuru utekelezaji wa mipango aina hiyo ambayo ni uhalifu mwingine dhidi ya wa Afghan wanawake kwa sababu mipango hii msingi wake ni mtazamo wa kidunia wa kisekula ambao unakwenda kinyume na maumbile ya Uislamu. Mipango yote hii inawasilisha kinadharia kwamba wanasimama nyuma ya usawa wa wanawake kushiriki katika kila nyanja ya maisha, wakitia mkazo kuzidisha idadi ya wanawake na kushiriki katika uongozi, kusitisha vurugu dhidi ya wanawake, kuwashirikisha wanawake katika michakato yote ya amani na usalama, kupanua uwezeshaji wa wanawake kiuchumi na kuufanya usawa wa kijinsia kuwa ndio suala kuu katika kupangilia na kujenga maendeleo ya kitaifa n.k… Lakini kivitendo, nukta hizi zinahusishwa na matatizo ya kiutekelezaji na hivyo mpaka sasa hakuna natija ya kufaulu kiukweli kunakoweza kuonekana ndani ya nchi yoyote na ndiyo maana wanawake bado wanapambana na ukosefu wa usawa katika saa za kufanyakazi, ajira na mishahara, umilikaji, kupendelea jinsia katika usambazaji wa elimu na afya, ukosefu wa usawa wa kijinsia katika uhuru wa maoni, ukosefu wa kijinsia kuhusiana na vurugu na kuathriwa n.k.
UNSCR 1325, CEDAW na mipango mingine sawia inaeneza sumu ambayo inawabadilisha wanawake wa mujtama kuwa watumwa wa matumizi na serikali za kisekula za kirasilimali. Wamo katika mzozo wa kudumu na wa kuchosha dhidi ya wanaume ili kwamba wasiwakandamize haki zao nao pia wanayo ruwaza kwamba mwanamume lazima daima awe anapata ridhaa ya mwanamke ili aweze kuwa na sura ya kisasa ya mwanamume aliyezindushwa na demokrasia.

Kiufupi, je imo ndani ya mipango hii ishara yoyote ya ulinzi, uhuru na usalama wa Afghan wanawake ambao “Kundi la Marafiki” jipya linataka kuinusuru serikali katika kuyatekeleza? Hakika hakuna!!! Yote haya ni ahadi tupu ambazo zimerudiwa kuwasilishwa kwa kipindi cha miaka 18 kwa sura mpya!
Ummah umepokea baraka kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt), ambapo Mwenyezi Mungu (swt) ameupa suluhisho la matatizo yao yote. Badala ya kuweka nguvu katika miungano iliyofeli ya kidemokrasia na kupigania haki za wanawake zisizoweza kupatikana, wanawake Waislamu lazima wachukue suluhisho lililo tayari la Kiislamu. Uislamu umempa mwanamke haki ya kushiriki kisiasa, haki ya kusimamia mambo ya kiuchumi, haki ya kufanyakazi, haki ya kuhusishwa katika amali za kijamii, haki ya kupata kiwango cha juu cha elimu na karibia zote. Uislamu unampa mwanamke heshima, hadhi na usalama kama mwanadamu! Haki zote hizo zinaweza kudhaminiwa lau Shari’ah ya Mwenyezi Mungu (swt) inatawala. Hivyo basi, wanawake Waislamu wawekeze nguvu zao katika kunusuru kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume. Dola ambayo inawapa wao na wanawake wote duniani haki zao za kweli na hatimaye kuwatibu sumu ya demokrasia.

[فَاحْكُم بَيْنَهُم بِمَا أَنزَلَ اللّهُ وَلاَ تَتَّبِعْ أَهْوَاءهُمْ عَمَّا جَاءكَ مِنَ الْحَقِّ] "Basi hukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu wala usifuate matamanio yao ukaacha Haki iliyo kujia.” [al-Ma'idah: 48]

Imeandikwa kwa ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Amanah Abed

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 10 Mei 2020 11:45

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu