Jumanne, 05 Safar 1442 | 2020/09/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mwito ... Mwito ... Mwito ... kwa Majeshi ndani ya Nchi za Waislamu Hakuna Mwanamume Mukhlisina Miongoni Mwenu Atakaye Nyanyuka na Silaha Zake ili Kuinusuru Al-Aqsa, Palestina na Wanawake wake?

(Imetafsiriwa)

Tarehe ishirini na saba ya Shawwal 1438 H ni Ijumaa ya pili ambayo Waislamu hawajaweza kutekeleza Salat ul-Juma'a ndani ya Msikiti wa Al-Aqsa, kwa kuongezea juu ya hiyo ni ile Ijumaa ambapo Mayahudi waliichoma Minbar ya Al-Aqsa mnamo 1389 H. Huu utakuwa ni mfano hatari tangu kukombolewa kwa Al-Quds na Salahudin kutoka kwa Watu wa Msalaba kisha kuswali Juma’a ya kwanza baada ya kusafishwa kwa Al-Quds kutokana na najisi ya Watu wa Msalaba mnamo 583 H. Hizi ndizo mara tatu ambazo Waislamu hawakuweza kutekeleza Salat ul-Juma'a kwa zaidi ya karne nane! Hii inaonyesha namna ya uadui ilionao umbile la Kiyahudi dhidi ya Uislamu na Waislamu. Hawakuwazuia tu kutotekeleza ibada bali pia waliwasha moto katika sehemu za sala za pamoja ndani ya kiwanja cha Al-Aqsa. Hakika, ndivyo walivyo kama walivyoelezewa na Mwenyezi Mungu, Al-Qawee, Al-Azeez:

[ لَتَجِدَنَّ أَشَدَّ النَّاسِ عَدَاوَةً لِّلَّذِينَ آمَنُوا الْيَهُودَ وَالَّذِينَ أَشْرَكُوا] “Hakika utawakuta walio shadidi kuliko watu wote katika uadui kwa walio amini ni Mayahudi na washirikina.” [Surah Al-Ma’ida: 5:82] ... Ilhali kwa upande mwingine, rais wa Misri aliwasiliana na Netanyahu, kama alivyofanya mfalme wa Jordan na rais wa Uturuki wote wakitoa mwito wa utulivu ilhali mfalme wa Saudi alitoa taarifa ya kuelezea kusikitishwa kwa na yale yanayoendelea sehemu za Msikiti wa Al-Aqsa. Msimamo wao ni kuliomba umbile la Kiyahudi kutoruhusu wanaoabudu kuswali ndani ya Al-Aqsa na kupunguza matumizi ya vipekuzi vya umeme katika milangoni, ilhali wadumishe mpangilio uliopo wa kupekuwa watu. Na msimamo kama huo ulikuwa wa watawala waliobakia ndani ya nchi za Waislamu kwa sauti za chini na hata kunongóneza kama ambaye kinachoendelea hakiwahusu wao kabisa, pasina kuona aibu mbele ya Mwenyezi Mungu (swt), Nabii Wake(saw) na waumini. Hakika, Nabii (saw) alisema ukweli pale aliposema:

«إنَّ مِمَّا أَدْرَكَ النَّاسُمِنْ كَلَامِ النُّبُوَّةِ الْأُولَى: إذَا لَمْ تَسْتَحِ فَاصْنَعْ مَا شِئْت» “Watu walitambua maneno yafuatayo kutoka kwa Mitume waliotangulia: Lau huoni aibu, basi fanya utakavyo.” (Al-Bukhari kutoka 'Abdulah Ibn Mas'oud)

Tatizo la Al-Aqsa haliwezi kutatulika kwa kuwa umbile la Mayahudi linaendelea kuivamia Palestina. Kubwa ambalo linaweza kuruhusiwa chini ya umbile hili ni kuruhusu watu kuswali ndani ya Al-Aqsa, chini ya silaha za Mayahudi kwa mujibu wa maamrisho na ruhusa yao. Waziri wao wa Usalama wa Ndani alisema kwamba “Al-Aqsa iko chini ya udhibiti wa (Israel) inao usemi wa mwanzo na wa mwisho katika kufunguliwa na kufungwa kwake.” Na hivyo anajigamba mbele ya wanaodhalilishwa kutokana na kujisalimisha kwa watawala ndani ya nchi za Waislamu. Mwanzo wa uhalifu ni siku ile ambayo watawala walikubaliana na baadhi ya wale ambayo mioyo yao imejaa maradhi kutoka kwa wanaoitwa watawala ndani ya Mamlaka ya Palestina kwamba suala la Palestina ni la watu wa Palestina pekee. Kisha watawala wakakaa na kuangalia matokeo yake wakiwa na majonzi au bila! Na wabora wao miongoni mwao ni wale wanaowasiliana na mkuu wa umbile la Kiyahudi, kutoa mwito wapunguze utumiaji wa nguvu za kupitiliza dhidi ya watu wa Palestina! Hao ndio watawala ambao wanaoinurusu Palestina kupitia kuitelekeza Palestina, kama yule anayewacha kufanyakazi baada ya kuweka juhudi kubwa ndani yake. Mwenyezi Mungu (swt):

[قَاتَلَهُمُ اللَّهُ أَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ] “Mwenyezi Mungu awaangamizilie mbali! Vipi wanapotoka na haki?” [Surah Al-Munafiqun 63: 4]

Ruwabidha, watawala wajinga wa nchi za Waislamu wanafahamu kuwa harakati za watu wa Palestina haziwezi kuondosha umbile la Kiyahudi. Pia wanafahamu kwamba tatizo la Al-Aqsa na Palestina yote haliwezi kutatuliwa isipokuwa kwa kuliondosha umbile bovu na kuliondosha kwake kunawezekana tu kupitia jeshi litakalo nyanyuka na silaha zake na kulingóa umbile hilo. Hivi ndivyo nussra inavyotakiwa kuwa kwa ajili ya Ardhi Tukufu, ya Bait ul Maqdis yenye baraka, kibla cha kwanza kati ya Vibla viwili na cha tatu katika Haramayn ambao Waislamu wanasafiri kwenda huko na hivi ndivyo ushindi utakavyopatikana kwa wanawake Waislamu ndani ya ardhi tukufu ya Palestina.

Hakuna mwanamume mukhlisina ndani ya majeshi ya Waislamu, mwanamume atakaye nyanyuka na silaha zake akifuatiwa na ndgu zake wakitamka Takbir wakuwanusuru wanawake wa Al-Aqsa ambao wanashambuliwa na wahalifu ndani ya sehemu za Al-Aqsa na pembezoni mwa Al-Aqsa? Hakuna mwanamume mukhlisina ndani ya majeshi ya Waislamu ambaye damu yake yachemka ndani ya mishipa yake na kumsukuma kukiongoza kikosi chake kuelekea Al-Aqsa na kuwangóa watawala wanaosimama mbeleni mwao? Hakuna ndani ya majeshi ya Waislamu mwanamume mukhlisina anayeongozwa na njia ya Ansar wa Mwenyezi Mungu na Nabii Wake, watakaotoa ushindi kwa Wabebaji Da’wah mukhlisina na kuwaunga mkono Hizb ut Tahrir, ili kuwaondosha watawala hawa na kusimamisha hukmu ya Uislam, Khilafah Rashidah (Khilafah ya Uongofu), ikiongoza jeshi la Khilafah katika kuling’oa umbile ovu ili kufaulisha bishara njema ya Nabii wa Mwenyezi Mungu? Muslim alisema katika Saheeh yake kutoka kwa Abu Hurayrah: Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw) alisema:

«...لَا تَقُومُ السَّاعَةُ حَتَّى يُقَاتِلَ الْمُسْلِمُونَ الْيَهُودَ، فَيَقْتُلُهُمُ الْمُسْلِمُونَ»“Kiyama hakitosimama mpaka pale Waislamu watakapo wapiga vita Mayahudi, Waislamu watawaua...” Na katika simulizi nyingine, yeye (saw) alisema:

«تُقَاتِلُكُمُ يَهُودُ، فَتُسَلَّطُونَ عَلَيْهِمْ» “Mayahudi watawapiga vita nanyi mutawashinda.”

Enyi Waislamu: Majeshi ya Waislamu yako miongoni mwenu, ni vijana wenu, ndugu na jamaa zenu kwa hiyo wasukumeni katika ukweli ambao Mwenyezi Mungu ameuleta, wang’azieni nuru ya Uislamu ili watoe ushindi kwa Dini ya Mwenyezi Mungu na warudishe hadhi ya wanajeshi wa Uislamu ambao waling’oa Watu wa Msalaba kutoka katika ardhi ya Palestina na ardhi ya Ash-Sham na kuwang’oa Matartar kutoka katika ardhi za Uislamu. Walikuwa ndio mfano wa kuigwa duniani, kutokana na kheri waliyoieneza na uadilfu waliousimamisha.

Lau majeshi ya Waislamu yanataka kuwa tena wanajeshi wakubwa watajika kwa mara nyingine, wanahitaji tu kuinusuru Dini ya Mwenyezi Mungu na kuinusuru Al-Aqsa na maeneo yake na kuwasambaratisha watawala kwa kuwaondosha kutoka katika njia zao. Mwenyezi Mungu atawataja katika “kurasa za nuru” na watakuwa na nguvu duniani na Akhera watakuwa katika kiti cha Haki kwa Mfalme Mwenye uweza (swt):

[إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي جَنَّاتٍ وَنَهَرٍ * فِي مَقْعَدِ صِدْقٍ عِندَ مَلِيكٍ مُّقْتَدِرٍ] “Hakika wachamungu watakuwa katika Mabustani na mito. Katika makalio ya haki kwa Mfalme Mwenye uweza.” [Surah Al-Qamar: 54-55]

Enyi Majeshi ndani ya Ardhi za Waislamu: Al-Aqsa inalia kutaka msaada na maeneo ya Al-Aqsa yanalia yakitaka msaada. Al-Aqsa haitokombolewa kutoka katika uvamizi wake isipokuwa kwa kuliondosha umbile la Mayahudi. Harakati za watu wa Palestina licha ya kuwa ni za ushujaa mkubwa hazitoliondoa umbile la Mayahudi hata kama wanatekeleza jukumu lao kwa kadri ya ubora wao, lakini wanawapa mwito wa kuomba msaada na muwanusuru, kwa hiyo wasaidieni na wapeni nussra na muitikieni Mwenyezi Mungu Al-Aziz, Al-Hakeem:
[...وَإِنِ اسْتَنصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ] “Na wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia.” [Al-Anfal: 72]

Enyi Majeshi ndani ya Ardhi za Waislamu: Enyi Waislamu:
Tunauhakika kwamba tutaling’oa umbile la Kiyahudi, liwe ni jeshi lenye baraka litakalo ling’oa.
Tunauhakika kwamba Khilafah itarudi baada ya utawala huu wa kikatili, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, Mtume (saw) alisema:

«ثُمَّ تَكُونُ مُلْكًا جَبْرِيَّةً، فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ خِلاَفَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةٍ ثُمَّ سَكَتَ»
“Kisha kutakuwepo na utawala wa kikatili, kwa muda ambao Mwenyezi Mungu anataka uwepo, kisha Mwenyezi Mungu atauondosha atakapotaka kuuondosha, kisha kutakuwepo na Khilafah kwa Njia ya Utume, na kisha (saw) akanyamaza.” (Imesimuliwa na Imam Ahmad kutoka kwa Hudhayfah ibn al-Yaman.) Kwa hiyo liwe ni jeshi lenye baraka litakaloipa nussra Hizb ut Tahrir ambayo inafanyakazi kuirudisha.

Tunauhakika kuwa Ash-Sham na vito vyake, Al-Quds (Jerusalem) zitarudishwa kupitia Jeshi la Uislamu katika Dar Al-Islam. Imam Ahmad amesimulia katika Musnad yake kutoka kwa Hadith ya Salamah Ibn Nafil (ra) kwamba Mtume (saw) alisema:

«أَلَا إِنَّ عُقْرَ دَارِ الْمُؤْمِنِينَ الشَّامُ» “Nyumba ya Waumini ni Ash-Sham.” Katika simulizi ya Na’im Bin Hammad ndani ya Kitabu cha Fitan cha Katheer Bin Murrah: «عُقْرُ دَارِ الإِسْلامِ بِالشَّامِ» “Nyumba ya Uislamu ipo Ash-Sham” ... Na Ash-Sham na kito chake Al-Quds zitarudishwa kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu zikiwa na hadhi na nguvu, kwa hiyo jeshi litakaloirudisha litakuwa ni jeshi lenye baraka.

Enyi Majeshi ya Waislamu na Jamaa za Wanajeshi Waislamu: Fanyeni haraka kuinusuru Dini ya Mwenyezi Mungu… Fanyeni haraka kuinusuru Bait ul Maqdis na maeneo yake… Fanyeni haraka kuwanusuru wanawake wa Ardhi Tukufu… Fanyeni haraka kuling’oa umbile la Kiyahudi… Fanyeni haraka kuwanusuru wafanyikazi wa kusimamisha Khilafah ya uongofu… Fanyeni haraka kuirudisha Ash-Sham na kito chake Al-Quds katika nyumba ya Uislamu… Fanyeni haraka kupata utukufu wa dunia hii na Akhera… na hili ni bora kwenu kuliko yale wanayo (kupangilieni). Mwenyezi Mungu Al-Aziz Al Hakeem (mwenye Nguvu, mwenye Busara) alisema:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ] “Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal: 24]

H. 27 Shawwal 1438
M. : Ijumaa, 21 Julai 2017

Hizb-ut-Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu