Alhamisi, 18 Ramadan 1445 | 2024/03/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  3 Jumada II 1441 Na: 1441/011
M.  Jumanne, 28 Januari 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kuhitimisha Kampeni ya “Ukombozi wa Konstantinopoli Bishara Njema Ikatimia…inafuatiwa na Bishara Njema Nyingine!”
(Imetafsiriwa)

Leo tunahitimisha kampeni ya habari ya kiulimwengu iliyozinduliwa na afisi kuu ya habari ya Hizb ut Tahrir kwa kuagizwa na Amiri wa Hizb ut Tahrir, Mwanachuoni Mkubwa, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, Mwenyezi Mungu amlinde, ili Kukumbuka Tukio la Hijria la Ukombozi wa Konstantinopoli kwa anwani: “Ukombozi wa Konstantinopoli Bishara Njema Ikatimia... inafuatiwa na Bishara Njema Nyingine!Kampeni hii ilifanyika kwa ushirikiano na Shabab wa chama cha Hizb na wafuasi wa ulinganizi wa kusimamisha Khilafaha ya Uongofu ya pili kwa njia ya Utume duniani.

Mwanzo kampeni ilizinduliwa kwa hotuba iliyotolewa na Amiri wa Hizb ut Tahrir, Mwenyezi Mungu amlinde, ambapo alizungumzia kuhusu umuhimu wa tukio hili na sababu tatu ambazo kampeni hii ilizinduliwa , nazo ni:

- Kuwakumbusha watu kuhusu tukio hili na namna Ummah wa Kiislamu unavyoweza kuyashinda mataifa mengine lau utatekeleza Uislamu vizuri.

- Kukumbuka kwamba bishara njema ya ukombozi wa Konstantinopoli itafuatiwa na bishara njema ya kurudi kwa Khilafah, kisha kutimia kwa bishara ya ukombozi wa Roma na kupigana na Mayahudi na kuwashinda kwa uwezo mkubwa.

- Ulinganizi wa Hizb ut Tahrir wa kurudisha Khilafah tena unaendelea ndani ya Ummah, ukifufua ari yake licha ya usumbufu na uhadaifu kutoka kwa nchi za kikafiri na wale ambao ni wagonjwa moyoni.

Hili lilifuatiwa na msururu wa amali zilizotekelezwa na chama ndani ya nchi 24 ulimwenguni kote, ambazo zilifanyika kwa aina tofauti tofauti kuanzia makongamano, maandamano, jumbe za video, warsha na mazungumzo, mijadala misikitini, masokoni na sehemu za ummah, mahojiano ya moja kwa moja, makala na kauli na idadi kubwa ya vyombo vya habari vilichangamkia matukio haya. Matukio haya yalifanyika mbele ya maeneo mengi muhimu ya Kiislamu yanayohusiana na kampeni kama vile kuta za Konstantinopoli ndani ya Istanbul, kaburi la swahaba mkubwa Abu Ayyub al-Ansari (ra) na katika ngazi za Msikiti Al-Aqsa na kutoka katika mji wa Sfax, moja ya miji ya Khilafah ya Uthmaniya ndani ya Tunisia.

Kutoka katika mazungumzo, kulikuwepo na vitangulizi vya mafunzo yaliyopatikana kutokana na tukio hili kubwa kama vile baada ya bishara njema ya ukombozi wa Konstantinopoli kutakuwepo na bishara njema ya ukombozi wa Roma na ukombozi wa Jerusalem; na bishara njema hizi mbili hazitotimia isipokuwa mpaka baada ya kutimia kwa bishara ya kurudi kwa Khilafah ya Uongofu kwa njia ya Utume. Na kwamba Muhammad al-Fatih aliwekeza umakinifu wake juu ya suala msingi, nalo ni ukombozi wa Konstantinopoli. Kwa kuwa akili yake haikushughulishwa na suala jingine isipokuwa suala la ukombozi na hakuzungumza isipokuwa kulihusu hilo, wala hakutoa idhini kwa wenzake kuzungumza isipokuwa ni kuhusu hilo, kinyume na wale wanaodai urithi wa Uthmaniya kisha wakawatupa wanajeshi wao ndani ya NATO na kuwatoa muhanga ndani ya Libya kwa ajili ya Amerika! Kwa hakika ushindi hautapatikana kwa Dini hii wala miji haitofunguliwa na watawala wasaliti wasiokuwa na maana ambao wanatafuata msaada wa makafiri na kupeana mikono na wahalifu na majangili Warusi, Waingereza na Waamerika na kumsaliti Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na kuisaliti Amana yao.

Na kutoka katika ngazi za Msikiti Al-Aqsa, Hizb ut Tahrir ndani ya Ardhi yenye Baraka – Palestina pamoja na maelfu ya waliojumuika walituma mwito kwa majeshi ya Waislamu kuchukua hatua na kusimamisha Khilafah na kuikomboa Jerusalem. Kongamano lililofanywa na Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan juu ya tukio hili liliwalingania watu wenye uongozi na nguvu ndani ya Sudan kutoa ushindi kwa Hizb ut Tahrir ili kuwaokoa wao na Ummah kutokamana na utumwa wa ukoloni Ukafiri.

Pamoja na uongozi wake, Shabab wake na wafuasi wake, Hizb ut Tahrir ilitoa juhudi kubwa kufufua kumbukumbu hii kubwa, kuwakumbusha Ummah na watu wake walio na uongozi na nguvu kwamba kurudi kwa Khilafah kutarudisha utukufu utakaokuwa sawa na utukufu wa Muhammad al-Fatih na jeshi lake.

Nasi pia katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir tunatuma mwito maalum kwa kila Muislamu ambaye anaulinda Uislamu anayefanya kazi katika vyombo vya habari kushiriki katika kueneza juhudi hizi ambazo zimetolewa kwa ajili ya kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu Muweza, na kuchangia katika mwito wa kurudi kwa utukufu wa Waislamu, mwito wa kurudisha Khilafah ya Uongofu kwa njia ya Utume.

 [يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal: 24]

 

Mha. Salah Eddine Adada
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu