Jumamosi, 13 Rabi' al-thani 1442 | 2020/11/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  28 Safar 1442 Na: 1442/07
M.  Alhamisi, 15 Oktoba 2020

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

[وَمَنْ أَحْسَنُ قَوْلاً مِمَّنْ دَعَا إِلَى اللَّهِ وَعَمِلَ صَالِحًا وَقَالَ إِنَّنِي مِنَ الْمُسْلِمِينَ]
“Na ni nani mbora wa kusema kuliko aitaye kwa Mwenyezi Mungu na akatenda mema, na akasema: Hakika mimi ni katika Waislamu?” [Surah Fussilat: 33]

Pindi Mwenyezi Mungu When Allah (swt) anapowasifu wabebaji dawah:

[وَمَنْ أَحْسَنُ قَوْلاً مِمَّنْ دَعَا إِلَى اللَّهِ وَعَمِلَ صَالِحًا وَقَالَ إِنَّنِي مِنَ الْمُسْلِمِينَ]

“Na ni nani mbora wa kusema kuliko aitaye kwa Mwenyezi Mungu na akatenda mema, na akasema: Hakika mimi ni katika Waislamu?” [Surah Fussilat: 33], huku kwa sababu tu mtu ni mtetezi wa Uislamu, majambazi katika vikosi vya usalama vya serikali ya Hasina vimemkamata mwanaharakati wa Hizb ut Tahrir, anayeitwa Abdullah ibn Yunus, na kumweka mahali pasipojulikana kwa zaidi ya miezi miwili. Mnamo Julai 22, 2020, mwanafunzi huyu wa jiografia wa Chuo cha Mohammadpur Kendriyo, Dhaka, alichukuliwa kwa nguvu na vikosi vya usalama vya vya wanaume kati ya 8 na 10 wakiwa wamevalia nguo za raia kutoka nyumbani kwa jamaa yake huko Mohammadpur, Dhaka. Halafu familia yake walikwenda kwa afisi ya polisi ya eneo hilo, afisi mbali mbali za RAB (Kitengo cha Kuchukua Maamuzi ya Haraka) na afisi za DB (Tawi la Upelelezi), lakini hakuna hata mmoja wao alikiri kumchukua. Wazazi wake waliugua kwa sababu ya kutojua yakini na wasiwasi. Hata magazeti mengi ya kitaifa yalichapisha habari za 'kutoweka kwake kwa nguvu' kupitia vikosi vya usalama, lakini bado wangali hawajamfikisha mahakamani wakionyesha amekamatwa wala hawajamwachilia.

Majambazi hawa katika vikosi vya usalama wamekuwa hawana wasiwasi juu ya mateso ya watu kwa sababu ya ukandamizaji wao wa muda mrefu wa watu kwamba, baada ya kumkamata mtu, wanaweza kumweka kwenye vifungo vyao kwa siku na miezi, na kumsahau, na kwa kutopata ratiba ya mamlaka ya juu ratiba na ukosefu wa uamuzi wanamuweka mtu siku baada ya siku katika mazingira yasiyo ya kibinadamu.

Tunataka kuwakumbusha wanachama wa vikosi vya usalama - ala za udhalimu wa utawala wa Hasina - kwamba viongozi na wanaharakati wa Hizb ut Tahrir wanafanya kazi kwa ajili ya Khilafah Rasidah ili kusimamisha Dini ya Mwenyezi Mungu (swt) hapa Duniani ili kupata radhi Zake (swt) pekee. Kwa upande mwingine, serikali ya Hasina inatumiwa kama ala za kuzuia kusimamishwa tena kwa Khilafah iliyo karibu ili kuwaridhisha mabwana zao mabeberu makafiri. Na kama sehemu ya hilo, serikali hii iliamuru kudhulumiwa na kuwateswa kwa viongozi na wanaharakati wa Hizb ut Tahrir. Hivyo basi mnapaswa kuziogopa hasira za Mwenyezi Mungu (swt) na muizingatie Hadithi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw):

«إِنَّ اللَّهَ قَالَ: مَنْ أَهَانَ لِي وَلِيًّا فَقَدْ بَارَزَنِي بِالْعَدَاوَةِ»

“Hakika, Mwenyezi Mungu (swt) amesema: Yeyote anayemdhalilisha kipenzi (Walii) changu amtenganza uadui na Mimi...” (at-Tabaraani).

Mwisho kwa kukumbusha uhalifu huu uliofanywa dhidi ya Uislamu, tunataka kuwaonya wanachama wa vikosi vya usalama na serikali ya Hasina ambao waliuamuru kwamba vitendo hivyo ni vya kinyama mno kwa Uislamu kwamba, licha ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kusema:

«الْإِسْلَامُ يَجُبُّ مَا قَبْلَهُ»

"Uislamu unaondoa lililokuja kabla yake" (Ahmad na Tabarani), yaani, kesi ambazo zilizotatuliwa wakati wa Ujahiliya zitazingatiwa kama kesi zilizotatuliwa, kutakuwa na baadhi ya tofauti; na, moja yao ni wale walioudhuru Uislamu na Waislamu - wametengwa kutokana na hadith hii. Hii ni kwa sababu Mtume (saw), alipoifungua Makkah, alitangaza kwamba damu ya watu wengine imwagwe bila kutojali chochote kwani walikuwa wakiudhuru Uislamu na Waislamu katika Ujahiliya. Aliagiza damu yao imwagwe hata ikiwa wanashikilia mapazia ya Kaaba. Lakini, Mtume (saw) aliwasamehe wengine wao (kama vile, Ikrimah ibn Abu Jahl) baadaye; kwa hivyo, Khilafah iliyo karibu itawasamehe wengine wao kwa kutathmini viwango vyao vya uhalifu na kuwaadhibu wengine kama mfano kwa wengine. Kwa hivyo, lazima mzingatie - msifanye dhambi zenu ziwe nzito, jiepusheni kuwatesa na kuwakandamiza wanachama na wanaharakati wa Hizb ut Tahrir, na muwaachilie mara moja wale mliowakamata.

]مَنْ عَمِلَ سَيِّئَةً فَلَا يُجْزَى إِلَّا مِثْلَهَا]

“Mwenye kutenda uovu hatalipwa ila sawa na huo uwovu wake” [surah ghafir:40]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu