Jumamosi, 11 Sha'aban 1441 | 2020/04/04
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afrika Mashariki

H.  16 Rajab 1436 Na: 1436/12 H
M.  Jumanne, 05 Mei 2015

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Bwana Kerry: Una Yapi ya Kutuambia Wakati Wewe na Nchi Yako Mnabeba Mfumo wa Maangamivu kwa Kenya na Ulimwengu Mzima kwa Jumla?!

Waziri wa Kigeni wa Amerika John Kerry alizuru Kenya na kukutana rasmi na Raisi Uhuru Kenyatta mnamo Jumatano 4 Mei 2015. Miongoni mwa kadhia muhimu zilizo jadiliwa na viongozi hao wawili zinahusu miamala ya kibiashara kati ya Kenya na Amerika, uovu wa ugaidi na kadhia ya amani na usalama hususan nchini Somalia na Sudan Kusini.  

Tungependa kutoa maoni juu ya ziara hii:

Utawala wa Amerika ni utawala wa kikoloni unaojichukulia kumiliki mamlaka ya kuiamulia Kenya na nchi zile zinazoitwa za ulimwengu wa tatu kadhia zao kuhusiana na nyanja zote za maisha iwe kisiasa, kiuchumi au kijamii. Ni dhahiri shahiri kuwa nchi zetu licha ya kupiga kelele kudai uhuru wao, kihakika bado zingali zinachukuliwa kuwa ni majimbo au maeneo ya nchi za Kimagharibi ambazo ni lazima ziitikie na kutii! Kuhusu yale yaliyoibuka kutokana na majadiliano hayo, huu hapa ufafanuzi wake,  

Kuhusu miamala ya kibiashara, ni wazi kuwa sababu iliyo nyuma ya miamala ya kibiashara kati ya Kenya na Amerika ni kuilazimisha Kenya kufungua kwa upana mlango wake kwa kampuni kubwa za kimataifa zinazo milikiwa na mabwenyenye wa Amerika. Amerika inalia ngowa kwa mabwenyenye Waingereza kuendesha sehemu kubwa ya biashara nchini Kenya na sasa ina penya ili kufikia sehemu yake. La muhimu zaidi ni kuwa mtu wa kawaida hana chochote anachopata, badala yake wataendelea kuwa wafanyakazi wa thamani duni katika kampuni hizo.

Ama kuhusu vita dhidi ya ugaidi, ni dhahiri kuwa Amerika ndio mfadhili mkuu wa vita hivi. Bwana Kerry anajaribu kimakusudi kuwasahaulisha raia wa Kenya historia chafu ya Amerika ambayo Amerika imekuwa ikitekeleza vitendo vya kigaidi kisha kuvitumia kufikia ajenda yao ya kinyama ya kikoloni. Mfano halisi ukiwa, ni mnamo 1960 kabla ya Amerika kuivamia Cuba, wanajeshi wa Amerika walizilipua ndege zao wenyewe kimakusudi kisha kuibwagia lawama Cuba. Amerika imekuwa ikiwafadhili wanamgambo katika nchi nyinginezo kwa maslahi yao wenyewe kisha kuwabandika jina la magaidi. Hivyo basi Amerika hana chochote cha kuhofia kuhusu usalama wa Kenya; badala yake ni Amerika yenyewe ndiyo iliyoitumbukiza Kenya katika ghasia za umwagaji damu ya watu wasio na hatia. Inapaswa kuhesabiwa waziwazi kuwa katika mvutano wake na Muungano wa Kisovieti, kwa ajili ya kung'ang'ania rasilimali za kiasili zilizo jaa barani Afrika, Amerika kwa ushirikiano na Ulaya ilikuwa ikidai kuwa utovu wa usalama na kuenea kwa umasikini barani Afrika ni natija pekee ya ukosefu wa demokrasia ya vyama vingi barani Afrika. Haya ndio matokeo yake sasa.

Afrika imekuwa uwanja wa mieleka na vita kabla na hata baada ya chaguzi za kidemokrasia. Sasa tunaweza kutambua kuwa tishio la ugaidi si chochote ila ni udhuru mpya wa kuendelea kufyonza rasilimali zetu za kiasili. Juu ya yote haya, ikiwa Kerry kweli amejitolea kushinda vita dhidi ya ugaidi kama anavyodai, ni lazima basi aanze na wanajeshi wake mwenyewe waliowachoma moto watu wasiokuwa na hatia mchana na usiku kwa ndege zake zisizokuwa na rubani (droni).       

Kuhusiana na suala la amani na usalama nchini Somalia na Sudan Kusini, swali ambalo ni lazima liulizwe kwanza ni, kabla ya kujadili amani katika nchi hizi, ni nani aliyezitia nchi hizi katika janga hili kama si ushindi wao juu ya Ulaya katika kinyang'anyiro chao kwa rasilimali asili za nchi hizi?

Hatimaye, tungependa kusema kuwa Amerika na mfumo wake wa kirasilimali ndio chanzo pekee cha matatizo yote ulimwenguni. Wapambe wake wanazurura ulimwengu mzima wakijaribu kuficha waziwazi aibu yao wenyewe, na janga, kufeli na dosari za mfumo wao. Ipo haja ya kuleta mwingine kama mbadala ya huu ambao kimsingi umefeli tangu kuanzishwa kwake. Mfumo ambao utauokoa ulimwengu mzima kutokana na majanga yanayochipuza kutokana na ukoloni wa Amerika.  Bila shaka, mfumo huo si mwingine ila ni Uislamu utokao kwa Muumba wa Ulimwengu. Huo ndio mfumo pekee unaohitajika ulimwenguni ambao utadhamini haki za watu, na uadilifu na utulivu. 

Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Afrika Mashariki

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afrika Mashariki
Address & Website
Tel: +254 717 606 667 / +254 737 606 667
www.hizb-ut-tahrir.info
E-Mail:  abuhusna84@yahoo.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu