Alhamisi, 09 Shawwal 1445 | 2024/04/18
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  26 Sha'aban 1441 Na: 1441/09
M.  Jumapili, 19 Aprili 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ramadhan inaingia huku Serikali za Kisekula zikifungua mafundo yaliyo salia ya Uislamu.

Huku umma unapoingia katika mwezi mtukufu wa Ramadhan, Hizb ut-Tahrir Kenya ingependa kutuma risala zake za dhati kuwapongeza Waislamu wa Kenya na ulimwengu kwa jumla. Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) atupe nguvu na afya za kuweza kuitekeleza ibada tukufu ya saumu ambayo licha ya kuwa ni faradhi bali pia ni miongoni mwa nguzo tano za Uislamu.

Kwa bahati mbaya, Ramadhan ya mwaka huu inaanza ikiwa Waislamu humu nchini na duniani kote wamezuiliwa kutekeleza ibada ya swala ya Ijumaa na Swala nyengine za Jamaa misikitini. Wanavyouni wa kiserikali kama ilivyo mazoea waliifunga misikiti kwa haraka hata kabla ya serikali kutoa ilani ya kuifunga. Kwa hakika hatua hiyo ya wanavyuoni sio ngeni ikizingatiwa kuwa tayari wamekuwa wakitoa fatwa zinazo gongana wazi na Quran na Sunnah. Lakutamausha zaidi, ni kwamba baadhi ya fatwa mbovu zimekuwa zikitolewa kwa kuunga mkono utiaji saini wa mikataba ya kidhulma ambayo bado ni yenye kuletea udhalilifu umma mtukufu wa Kiislamu. Tunasema kuwazuia Waumini kutotaja jina la Mwenyezi Mungu ni kitendo cha kidhulma kinacho kwenda kinyume na sheria ya Kiislamu.

وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن مَّنَعَ مَسَاجِدَ اللَّهِ أَن يُذْكَرَ فِيهَا اسْمُهُ وَسَعَىٰ فِي خَرَابِهَا ۚ أُولَٰئِكَ مَا كَانَ لَهُمْ أَن يَدْخُلُوهَا إِلَّا خَائِفِينَ ۚ لَهُمْ فِي الدُّنْيَا خِزْيٌ وَلَهُمْ فِي الْآخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٌ

“Na ni nani dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye zuia misikiti ya Mwenyezi Mungu kutajwa ndani yake jina lake na akajitahidi kuiharibu? Watu hao haitawafalia kuingia humo ila nao wanaogopa. Duniani watapata hizaya na Akhera watapata adhabu kubwa.” [Al-Baqara: 114]

Tunasema, katika kipindi cha mkurupuko wa maradhi, kinacho takikana na sheria ya Kiislamu sio kuzuia Waislamu wote kijumla kuswali swala za jamaa bali kinacho takikana ni kuwatenga na kuwazuia wale wagonjwa kuingia misikitini. Kinacho paswa kufanywa kuzuia maambukizi ya maradhi, ni kuweka mikakati ya kujikinga na maambukizi kama vile udumishwaji wa usafi, kuvaa vitanzua (vibarakoa) kupima watu na kuosha mikono. Dalili ya haya ni hadithi iliopo katika Mustadarak ya Al-haakim kutoka kwa Twariq bin Shihab aliye pokea kwa Abi Musa kutoka kwa Mtume (saw) kwamba alisema:

الْجُمُعَةُ حَقٌّ وَاجِبٌ عَلَى كُلِّ مُسْلِمٍ فِي جَمَاعَةٍ إِلَّا أَرْبَعَةٌ: عَبْدٌ مَمْلُوكٌ، أَوِ امْرَأَةٌ، أَوْ صَبِيٌّ، أَوْ مَرِيضٌ

((Swala ya Ijumaa ni haki ya uwajibu kwa kila Muislamu katika jamaa isipokuwa kwa watu wanne: mtumwa anaye milikiwa, au mwanamke, au mtoto au mgonjwa.))

Ama kuhusiana na swala za jamaa, Sheria imeeleza kwamba swala hiyo ni faradhi ya kutoshelezana (Fardhul kifaya). Abu Darda radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie amepokea kutoka kwa Mtume (saw) kwama alisema:

مَا ِمنْ ثَلَاثَةٍ فِي قَرْيَةٍ وَلَا بَدْوٍ لَا تُقَامُ فِيهِمْ الصَّلَاةُ إِلَّا قَدْ اسْتَحْوَذَ عَلَيْهِمْ الشَّيْطَانُ، عَلَيْكَ بِالْجَمَاعَةِ فَإِنَّمَا يَأْخُذُ الذِّئْبُ مِنَ الْغَنَمِ الْقَاصِيَةَ

Hawawi watu watatu katika mji wala mashamba ndani yao ikawa haisimamishwi swala isipokuwa Shetani huwa amewatawala, jilazimisheni na swala za jamaa kwani mbwa mwitu hula mbuzi aliye peke yake. [Abu Daud]

Kwa kweli Ramadhan huletea kheri umma mzima wa Kiislamu lakini umma kwa sasa unakumbwa na janga la Covid-19 ambalo kwa mara nyingine limefichua utepetetevu wa viongozi wa kirasilimali. Udhaifu wa mfumo wa kirasilimali umewekwa peupe kwa kila mtu kuona. Mfumo huu uko duni zaidi kama nyumba ya buibui nyumba duni zaidi – mfumo ambao hata kabla ya kutokea majanga wenyewe tayari ni majanga. Mikakati ya watawala wa kirasilimali ya kujaribu kuokoa uchumi si lolote ila majaribu ya kutaka kuzuia maovu ya mfumo wao maiti unaosubiria tu tangazo la tarehe ya mazishi yake.

Huku tunaposoma Quran ndani ya Mwezi huu wa kheri, Waislamu wanawajibika kuelewa kwamba maafa yote wanayokumbana nayo leo yataondoka ikiwa watatekeleza faradhi ya kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume katika mojawapo ya nchi kubwa za Kiislamu. Na ni kwa sababu ya kutoitekeleza/kutoitabikisha Quran katika maisha yao ndio Waislamu wanaonja maafa na majanga yote katika maisha yao jumla.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu