Ijumaa, 06 Rabi' al-awwal 1442 | 2020/10/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  14 Muharram 1442 Na: 1442 / 07
M.  Jumatano, 02 Septemba 2020

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Moto Unaowaka Karachi Utazimwa na Khilafah Pekee, na wala Kamwe Hautazimwa na Nidhamu ya Kimajimbo ya Kibunge ya Kidemokrasia au Jamhuri ya Kiraisi

Maeneo mengi ya Karachi bado yamezama katika mchanganyiko wa mvua na maji taka, na kukatika kukubwa kwa nguvu za umeme, baada ya siku kadhaa za mvua kubwa iliyoharibu miundombinu ya Karachi iliyopuuzwa kwa muda mrefu. Na katika kukabiliana na kuongezeka kwa hasira ya umma, serikali ya Bajwa / Imran iliamka kutoka katika usingizi wa miaka miwili kutangaza kwamba sasa inafanya kazi kwenye "Mpango wa Ujenzi wa Karachi". Pamoja na hivyo, shida za kina na nyingi za Karachi za miongo kadhaa haziwezi kusuluhishwa na kiraka cha kweli na cha kuijibu demokrasia ya kimajimbo fisidifu iliyofeli, sawa iwe katika upande wa kufuta Kifungu cha Marekebisho cha Kumi na Nane, kuweka mfumo wa urais, kuifanya Karachi kuwa mkoa uliotenganishwa au kuikabidhi Karachi kwa udhibiti wa jeshi.

Mfano wa serikali ya majimbo hujengwa juu ya mgawanyiko wa vikundi katika jamii, ikigawanya vikundi hivyo katika vyama vidogo vya kisiasa katika ngazi za mkoa na miji. Halafu inapeana vikundi hasimu fursa ya kufikia serikali iliyochaguliwa chini ya mfumo wa serikali tatu katika ngazi ya jimbo, mkoa na jiji. Kwa sababu ya utawala wa vyama pinzani katika viwango anuwai, demokrasia ya majimbo husababisha mapambano mabaya ya madaraka, pamoja na kupuuza kwa kiwango kikubwa sana mambo ya watu. Kwa kuongezea hilo, kwa jina la uwajibikaji, mfumo wa bunge na uraisi wa kidemokrasia hugawanya madaraka juu ya taasisi za serikali, ndani ya wizara, taasisi na viwango vya serikali, ambayo inasababisha kuundwa kwa mfumo wa pamoja wa utawala kati ya taasisi hizi. Ugavi huu wa mamlaka unasababisha machafuko serikalini na ukosefu wa uwajibikaji, kama ilivyodhihirika katika mgogoro wa hivi karibuni huko Karachi. Na wakati Karachi ilipokuwa inazama, kila afisa wa serikali katika ngazi ya jimbo, mkoa na jiji alilaumu wengine, hakuna mtu aliyewajibika kwa machafuko ambayo Karachi imejikuta ndani yake leo. Kufanya mambo kuwa mabaya zaidi, demokrasia inawapa wabunge haki ya kutunga sheria kulingana na matakwa na malengo yao, na hivyo kufungua njia ya kuendesha sheria ili kutimiza maslahi yao, huku wakipuuza mambo ya umma.

Kinyume na demokrasia, nidhamu ya Khilafah huweka jukumu kwa khalifa mwenyewe, na humchukulia kuwa ndiye mwenye kuwajibika moja kwa moja kwa vitendo vya magavana katika wilaya na miji. Khalifa ana mamlaka kamili ya kuwabadilisha na kuwaoondoa magavana watepetevu au wafanyikazi wenye uwezo na nguvu, ikiwa watu wanalalamika juu yao. Kama ambavyo Khilafah huitazama jamii kama kitengo kimoja, na kugawanya serikali kuwa wilaya na kata nyingi husaidia kuyatawala maeneo haya kama jamii moja, chini ya mfumo wa serikali kuu inayoongozwa na Khalifa. Licha ya kuwa mamlaka makuu ya utawala yako kwa Khilafah, idara ya utekelezaji haiko kwa utawala mkuu, ili kuhakikisha majibu ya haraka kwa mgogoro wowote unaowatokea watu. Khilafah hutenga rasilimali za kutosha kwa wilaya na kata, sio kwa msingi wa uwakilishi wao katika serikali, bali kulingana na hukmu za sheria na mahitaji ya jamii. Khalifa na magavana wanalazimika kutawala kwa yale yote yaliyoteremshwa na Mwenyezi Mungu katika Qur'an na Sunnah na yale yalichoongozwa nazo katika qiyas ya kisheria na Ijmaa ya Maswahaba, kama ambavyo haijuzu kwa Majlis al-Ummah au mabaraza ya wilaya kutunga sheria, lakini badala yake wawahesabu watawala kwa msingi wa Uislamu.

Hakika hadhara ya Kiislamu ni tukufu, ndiyo iliyojenga miji kama Samarkand, Bukhara, Granada, Baghdad, Cairo, Dameski na Istanbul, ambayo ilikuwa ni minara inayong'aa ya ustawi na maisha ya kistaarabu kwa ulimwengu kwa karne nyingi. Na, Mungu akipenda, Khilafah kwa Njia ya Utume, itakayo simama hivi karibuni kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, itaifufua miji ya Kiislamu kama Karachi, Lahore, Kabul, Tehran, Srinagar, Dhaka, Jakarta na Tunisia, mpaka irudi tena iwe ni minara ya ulimwenguni.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-pakistan.com/

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu