Jumanne, 14 Sha'aban 1441 | 2020/04/07
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Familia ya Kiislamu … Na Hatari za Kuvunjika

Kiungo cha familia, kilicho tawaliwa na mapenzi, mshikamano na utulivu, kiinje inaonekana kuwepo na umoja, lakini kindani imegawanyika, imeunganishwa tu na kuta za nyumba au meza ya chakula; nyumba ambamo mtu anaishi kama ambaye hajulikani miongoni mwa wengine na hawashirikishi katika hofu na matatizo yake binafsi! Kuvunjika huku kumewakumba wanafamilia na kuwapasua na kuwafanya waishi kibinafsi binafsi, wakiteseka kutokana na natija ya mfarakano, upweke, huzuni na kupoteza.  

Soma zaidi...

Ziara ya Haraka ya Trump ya Ulaya, Uingereza na Urusi

Ziara ya haraka ya Trump ya Ulaya, Uingereza na Urusi imeuacha ulimwengu ukishangaa ikiwa Amerika iko makini kuhifadhi mfumo wa uhuru ulioko kwa sasa. Trump kumsifu Merkel kuwa mateka wa Urusi na kushutumu wazi wazi mipango ya May ya kuiondoa Uingereza katika Muungano wa Ulaya (Brexit) inaashiria zaidi ya sintofahamu nyepesi katika kitovu cha muungano wa nchi zilizopakana na bahari ya Atlantiki. Kuongeza chumvi kwenye kidonda, Trump alisonga mbele na kuuita Muungano wa Ulaya adui huku akitarajia mkutano usiokuwa wa kawaida wa kirafiki na Putin mjini Helsinki.

Soma zaidi...

Hatari ya Uvivu na Ukosefu wa Motisha kwa Muislamu

Kila mmoja anaijua hali ambayo mtu anajihisi ulegevu fulani na kutokana na hisia hii inakuwa vigumu kwake kutekeleza majukumu fulani, licha ya kiwango cha umuhimu wa majukumu hayo kwake, ima iwe ni jukumu la Kiislamu, la kimaumbile, matamanio au ghariza, uchungaji watoto, faida ya kiuchumi, masomo au hata majukumu madogo madogo ya nyumbani.

Soma zaidi...

Je, Erdogan Anajitayarisha Kutangaza Khilafah Nchini Uturuki?

Waislamu kweli wanasubiri kwa hamu Khilafah. Miongoni mwa idhlali na maangamivu yanayoukumba ulimwengu wa Kiislamu, leo Waislamu wanasubiri tetemeko la ardhi, siku ambayo Waislamu nchini Uturuki, biladi za Kiarabu na biladi nyenginezo za Kiislamu watakapochukua msimamo walioupoteza, na kutupilia mbali utiifu wowote mwengine isipokuwa utiifu kwa Mola wao, na kutokana na nidhamu yoyote nyengine isipokuwa kwa Dini yao tukufu ya Uislamu.

Soma zaidi...

Nigeria Yakabiliana na Mustakbali Usiothabiti

Tangu uhuru mwaka wa 1960, historia ya kisiasa ya Nigeria imekuwa ya kuzongwa na matatizo kadhaa - vita vya kikabila, vita vya kidini, vita vya mafuta, mapinduzi ya kijeshi nk. Takribani asilimia 75 ya miaka baada ya uhuru ilitumiwa chini ya utawala wa kijeshi na udikteta. Hata hivyo, ghasia za Nigeria hazijawahi kufikia kiwango cha wenzao wa Afrika kama Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), na Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR).

Soma zaidi...

Je, Vijana wa Ummah Huu Waweza Kupatiliza Fursa ya Udhaifu wa Amerika na Kuurudisha Katika Nafasi Inayostahiki

 Vichwa vya habari kama “Je, Amerika Iko Katika Mporomoko?”, “Amerika Iko Katika Kasi Kubwa ya Kuporomoka…”, “Mustakbali: Kuinuka kwa China, Kuporomoka kwa Amerika”, na “Mporomoko Mkuu wa Amerika Huenda Ikawa ni Matumaini Bora ya Kuiokoa Demokrasia” vimekuwa vikijitokeza mara kwa mara pasi na utata.

Soma zaidi...

Maandamano Nchini Iran

Tangu kutokea kwa mapinduzi ya Iran mwaka wa 1979, viongozi wa kidini wa kishi'a wametumia hadhi yao inayo karibiana na ya kiwahyi miongoni mwa raia wa Iran kuwadhibiti na kuwalemaza kuamini kuwa serikali ya Iran imebeba bendera ya Uislamu dhidi ya njama za Kizayuni na Amerika katika kuchukua uongozi wa Mashariki ya Kati.

Soma zaidi...

Pindi Akili Inapokuwa Mtunzi wa Sheria, Taharuki Hutawala

Miaka mitano iliyopita, Profesa Miroslav Djordjevic, mtaalamu wa upasuaji na urekebishaji viungo vya uzazi anayeongoza duniani, alipokea mgonjwa katika kliniki yake ya Belgrade. Alikuwa ni mgonjwa aliyejibadilisha jinsia yake aliyefanyiwa upasuaji katika kliniki nyengine kuondoa uume wake – na tangu wakati huo amebadili mawazo yake.

Soma zaidi...

“Ni Nani Atakaye Komesha Mauaji ya Halaiki Dhidi ya Waislamu wa Rohingya?”

Kama mujuavyo, Waislamu wa Rohingya katika jimbo la Rakhine nchini Myanmar kwa sasa wanakabiliwa na kampeni katili ya mauaji ya halaiki mikononi mwa serikali katili ya Myanmar, wanaandamwa kwa kisingizio cha urongo cha kupambana na ugaidi. Jinamizi hili ambalo ndugu na dada zetu wa Rohingya wanateseka nalo halielezeki.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu