Jumanne, 16 Dhu al-Qi'dah 1441 | 2020/07/07
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kampeni ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
CEDAW ni Uhalifu wa Karne dhidi ya Mwanamke Muislamu

Kafiri Mmagharibi kwa makusudi anaendelea tokea hapo awali hadi sasa ili kuvunja familia, mujtma na Ummah wa Waislamu wote na kulichukua suala la mwanamke na kulitabban katika kueneza ustaarabu na fikra zao hususan katika nchi za Waislamu na kuelekeza vichwa vya habari muhimu na hatari ili kufikia ushindi dhidi ya vipengee vya Uislamu kama vile kubadilisha dini na kuleta maendeleo katika khutba za kidini na kubadilisha vipengee vya hukmu ili kuoana na madai yao ya usasa huku wakiilenga mishale yao ya sumu kuielekeza kwa wanawake Waislamu na jukumu lao msingi na stara yao ili kuhakikisha jukumu la muhimu katika maisha ya familia na mujtama. Hivyo basi, Umoja wa Mataifa ulitabban yote haya na kuzindua mikataba mingi na makongamano ya kimataifa kama vile Tangazo la Kuondosha Aina Zote za Unyanyasaji dhidi ya Wanawake (CEDAW) mnamo 1979, makubaliano hayo maovu ambayo yanayokaribiana katika uovu sawia na Tangazo la Balfour. Makubaliano juu ya "Kusitishwa kwa sheria na desturi pasina kuzingatia ni za dini na kuweka mahala pake sheria za kimataifa."
Hivyo basi, muendelezo wa makongamano ya kimataifa yalifanyika ili kuipa nguvu mikataba hiyo na kufanyakazi ili kuitekeleza na kuifaulisha. Kongamano la kwanza lilikuwa mnamo 1975, lililoitwa Mwaka wa Kimataifa wa Wanawake lililofanyika Mji wa Mexico, lililingania usawa, maendeleo na amani… Huu ulikuwa ni ulinganizi wa kiujanja ili kupatikane usawa baina ya wanawake na wanaume. Kampeni hii nia yake ni kuwaamsha Waislamu kwa ujumla na hususan wanawake Waislamu kuhusiana na hatari inayotokana na makubaliano hayo yaliyo na sumu hususan (Makubaliano juu ya Haki za Mtoto). Na hatari ya miungano ya wanawake ambayo inazunguka katika mzunguko wa Kafiri Mmagharibi mkoloni anayepigia debe thaqafa yake na fikra zake fisadi. Mwenyezi Mungu ni Muweza, wanapanga njama na Mwenyezi Mungu ni Mbora katika mipango.

Ijumaa, 18 Rabii' al-Awwal 1441 H sawa na Novemba 15, 2019 M

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 16 Februari 2020 13:34

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu